kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Kuna wakati watanzania wa kawaida wanashindwa kuchagua kipi Bora kati ya Sheria kwa upande mmoja na amani na utulivu kwa upande wa pili. Mh. Mwabukusi, Rais mteule wa TLS anahubiri Sheria Sheria Sheria Sheria mwanzo mwisho kwenye taifa ambalo watu wake wanajiona kuwa wako huru, Wana amani na utulivu. Mwabukusi anataka kuwaambia watanzania kuwa hapanaaa, hamko huru, hamna amani na hamna utulivu twendeni tukatafute amani na utulivu kupitia TLS.
Kwa maoni yangu mm amani na utulivu wetu hautokani na Sheria peke yake, bali ni pamoja na utamaduni, mazoea, uvumilivu, woga, sera, hulka ya watanzania na sheria. Kama ingekuwa ni sheria tu basi Kenya wangekuwa na amani na maendeleo zaidi kuliko sisi. Sheria iko hata DRC, Ethiopia, Somalia, Sudan na Ukraine.
Twendeni polepole na hiki kilichopo ambacho kinatuhakikishia kuimaliza Leo yetu na kutufikisha kesho na keshokuta kuliko watu wa Congo, Sudan, Somalia au Palestine na Israel. Present is known and secure.
Watu wetu Bado ni maskini sana kiuchumi na kielimu, hakuna sheria na demokrasia inayoweza kufua dafu 100% katikati ya watu maskini, wajinga na wenye njaa. Lazima tuinue elimu yao na kuondoa njaa zao kwanza kabla ya kuwaletea demokrasia na Sheria. (Abram Maslow's)