UDENYE
JF-Expert Member
- Mar 17, 2016
- 327
- 214
Tunamshukuru kwa dhati Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema na Mwingi wa Hekima, kwa kutuneemesha amani, utulivu na mafanikio katika uchaguzi uliomalizika hapa Tanzania.
Ni kwa fadhila Zake pekee tumeona uchaguzi ukifanyika kwa amani, pamoja na changamoto za hapa na pale za lakini kiujumla tumemalizika kwa mafanikio makubwa.
Tunamshukuru Mwenyezi Mungu na tunawapongeza kwa ushindi Dk. Hussein Ali Mwinyi kule Zanzibar na Mheshimiwa Dr Samia Suluhu Hassan kwa Tanzania. Tunamuomba Mola wetu mlezi Awape hekima, busara na moyo wa uadilifu katika kuongoza taifa letu kwa misingi ya HAKI, utu na maendeleo endelevu.
Vilevile, tunamshukuru MUNGU wetu aliye hai, mmoja pekee yake asiye na mshirika kwa kuvunja njama za wale wote waliokusudia kuiingiza Tanzania katika giza la mafarakano na umwagaji wa damu. Mwenyezi Mungu wetu mlezi Amezidhalilisha hila zao na kuyalinda maisha ya wananchi wake wapenda amani.
Tunaomba Molawetu mlezi aendelee kulilinda taifa letu dhidi ya fitna, chuki na mipango ya waovu na mahasidi. Awape wanaoipenda Tanzania moyo wa kuijenga, si kuibomoa.
Ewe Mola wetu, mlezi, Mungu wa Isaka na Yakobo.
Mungu wa Ibrahim, Musa na Yesu na Muhammad, na mitume na manabii wote uliowatuma, tujaalie daima kuwa taifa la amani, umoja na upendo.
Waongoze hawa viongozi wetu kwa nuru ya haki na hekima,
Walainishe nyoyo zao wawe na huruma na upendo kwa watanzania wenzao na binaadam kwa ujumla.
Wape nyoyo za kupenda haki na ewe mola wetu wamiminie uadilifu ili waongoze kama unavyotaka.
Waongoze na wajazo wananchi nuru ya kuwa na subira, mshikamano na heshima kwa mamlaka.
“رَبَّنَا آتِنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً وَهَيِّئْ لَنَا مِنْ أَمْرِنَا رَشَدًا”
“Rabbana ātinā min ladunka rahmah, wa hayyi’ lanā min amrinā rashadā.” (Al-Kahf: 10)
Ewe Mola wetu, tupe kutoka kwako rehema, na Ututengenezee njia sahihi katika mambo yetu.
Tanzania ni ya amani.
na kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, itaendelea kuwa hivyo milele. 🇹🇿
Udenye mchuuzi wa mikassava.