Uchaguzi una raha yake, mpaka PAYE imepunguzwa

CHEF

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2013
Posts
222
Reaction score
122
SIku chache tu baada ya kampeni kuanza PAYE (pay as you earn) imepunguzwa na mishahara kuongezeka automatically, unafikiri nani hajui umuhimu wa demokrasia ya vyama vingi.

Jamani Demokrasia ya vyama vingi ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi, tusijiloge kufuta vyama vingi.
 
Unadhani Wafanyakazi kwa sasa wanadanganyika kirahisi kama huko nyuma! Tunahitaji haki itendeke, ikiwemo ya kupanda madaraja kwa wakati. Huu upuuzi unaofanywa na hii awamu ya tano tumeuvumilia mpaka sasa tunaelekea kuchoka.

Haiwezekani mtu mmoja tu ajivishe vyeo vyote! Tunahitaji mabadiliko na ikibidi CCM na watu wake watuachie nchi yetu.
 
Walla sijakuelewa
kama umeajiriwa na unalipwa mshahara kwa mwezi fungua link hapo chini halafu weka mshahara wako ili ujue kiasi gani unatakiwa kupata baada ya PAYE kupunguzwa
PAYEE Calculator
1598871483104.png
 
Wafanyakazi wanataka mambo mazuri, si ndio haya sasa au unataka nini?
 
Mmeshatudanganya sana mpaka tumezoea mnasema mwezi huu unapita kimya, na Uccm wangu wote nimeishiwa pozi kabisa, najua siwezi kuwapa kura yangu Chadema lakini bora iharibike
Kaangalie vizuri mshahara wako wa kuanzia mwezi huu
 
Wafanyakazi wanataka mambo mazuri, si ndio haya sasa au unataka nini ?

Enzi za Kikwete, madaraja ya wafanyakazi yalipanda kila baada ya miaka mitatu! Huyu mzee tangu alipoingia, ameuvuruga utaratibu wote kwa visingizio visivyoisha! Mara uhakiki, mara tumsubiri anunue ndege kwanza!

Hiyo payee iliyopunguzwa, au hata kama angewaongezea wafanyakazi kiasi cha sh. laki 1 kwenye mishahara yao, bado ingekua ni kazi bure! Daraja kwenye muundo wa kiutumishi, ndiyo kila kitu!

Na hii ndiyo changamoto inayotukera wafanyakazi tulio wengi! Haiwezekani tangu enzi za JK mpaka leo, wafanyakazi wanaishi kwa muundo ule ule wa mshahara!

Kiufupi, tu huyu mzee si msaada na si chochote kwa wafanyakazi wa nchi hii! Sidhani kwa mwenendo wake huu, kama atakuja kukumbukwa na mfanyakazi yeyote yule! Labda hao alio waajiri yeye mwenyewe, wale wa TRA na vyombo vya dola
 
Wewe unafikiri kujenga nchi ni kitu cha kitoto, huoni kila kitu kinafufuliwa, yaani ulalamike barabara mbovu, ulalamike hakuna shirika la ndege , ulalamike shirika la reli limekufa, ulalamike elimu ni ghali ulalamike mishahara midogo, sasa kiongozi anaanza na kimoja baada ya kingine unalalamika tena, kwa hiyo wewe ni kulalamika tu! haya endelea kulalamika.
 
Kaangalie vizuri mshahara wako wa kuanzia mwezi huu
Mshahara ni ile basic salary, na ndio itakayotumika kukokotolea mafao yako. Kama haijaongezeka hiyo, usijidanganye kusema kwamba mshahara umeongezeka
 
Wewe unafikiri kujenga nchi ni kitu cha kitoto, huoni kila kitu kinafufuliwa, yaani ulalamike barabara mbovu, ulalamike hakuna shirika la ndege , ulalamike shirika la reli limekufa, ulalamike elimu ni ghali ulalamike mishahara midogo, sasa kiongozi anaanza na kimoja baada ya kingine unalalamika tena, kwa hiyo wewe ni kulalamika tu! haya endelea kulalamika.
Nchi haiwezi kuusha kujengwa na magufuli.

Miundombinu ni suala la mwendelezo, halitakiwi kusababisha maisha mengine yasimame.
 
Back
Top Bottom