Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Angetumia vyombo vya dola kulazimisha (kuiba) ushindi kama pacha wake alivyofanya huko Tanzania!What's your point?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Angetumia vyombo vya dola kulazimisha (kuiba) ushindi kama pacha wake alivyofanya huko Tanzania!What's your point?
Weka ushahidi, TL mwenyewe alisema uchaguzi ulikuwa huru na haki lakini alipoona ameshindwa akabadili gia angani .... .... Aibu!Angetumia vyombo vya dola kulazimisha (kuiba) ushindi kama pacha wake alivyofanya huko Tanzania!
Ndio maana nakushangaa kwa nini wenzako wote huku Tanzania wamesikitika Trump kushindwa na bado wanamtakia kila la heri katika madai yake lakini wewe Wacha1 unaonekana umepotea njia. You are either with the devil or you are not...huwezi kutaka huku na huko. Je ni kweli unaamini kutoka moyoni kuwa Magufuli angekuwa anagombea huko Marekani angeshinda? Unaruhusiwa kuwa mnafiki.Weka ushahidi, TL mwenyewe alisema uchaguzi ulikuwa huru na haki lakini alipoona ameshindwa akabadili gia angani .... .... Aibu!
How?Ndio maana nakushangaa kwa nini wenzako wote huko Tanzania wamesikitika Trump kushindwa na bado wanamtakia kila la heri katika madai yake lakini wewe Wacha1 unaonekana umepotea njia. You are either with the devil or you are not...huwezi kutaka huku na huko. Je ni kweli unaamini kutoka moyoni kuwa Maufuli angekuwa anagombea Marekani angeshinda? Unaruhusiwa kuwa mnafiki.
Kwamba angeweza kuvitumia vyombo vya dola kujihakikishia ushindi! Kwamba angeweza kuwakamata wapinzani wake na kuwasweka ndani! Kwamba angeweza kuwatisha wanaosimamia uchaguzi kuwachukulia hatua wakimtangaza mpinzani kashinda. Kwamba mikutano ya wapinzani ingeshambuliwa kwa mabomu n.kHow?
''Kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji.'' Huyo huyo Lisu alipokwenda kupiga kura kwenye Jimbo lake alisema mambo shwari, lakini matokeo yalipotangazwa akaanza kulialia kama kasuku. JPM kashinda kihalali na ndio sababu Wananchi walimchagua na nchi ipo shwari. Kama unafuatilia michango yangu siku zote nimekuwa nikisema Tanzania ni baba lao labda kama ulikuwa hulifahamu hilo itabidi ulizingatie. Why? Tanzania single handily ndio taifa ambalo lilifanikisha utawala wote wa nchi za kusini mwa Afrika kuwa huru (majority). Tanzania kwa nchi za Europe, na USA pamoja na washiriki wakubwa Japan China, India etc ipo more strategically na ina position ya kipekee. Kama hulifahamu hilo kalagabaho!Kwamba angeweza kuvitumia vyombo vya dola kujihakikishia ushindi! Kwamba angeweza kuwakamata wapinzani wake na kuwasweka ndani! Kwamba angeweza kuwatisha wanaosimamia uchaguzi kuwachukulia hatua wakimtangaza mpinzani kashinda. Kwamba mikutano ya wapinzani ingeshambuliwa kwa mabomu n.k




Kuna somo kubwa katika chaguzi zilizopigia hatua.Nakuapia kwamba kama ingekuwa ni Tanzania, Trump angeweza kupata ushindi hata wa asilimia 99% na hakuna mbunge wa upinzani angetangazwa kashinda na Biden angeiota tu Ikulu.
Ndio maana namshangaa mtu kama Wacha1...nashindwa kuelewa kwa nini anafurahia uchaguzi uliowezesha kuangushwa kwa Trump na hapo hapo akisifia uchafuzi tulioushuhudia nyumbani kwetu Tanzania. Watu kama Wacha1 nashindwa kabisa kujua kiwango cha uelewa wao kinasukumwa na nini...unafiki, ujinga, uoga au hila.Kuna somo kubwa katika chaguzi zilizopigia hatua.
Rais Trump anajulikana kuharibu norms and tradition nyingi za US.
Trump amejaribu kuharibu institutions za Marekani katika kila eneo la nchi.
Kwa US, nchi iliyosimama katika institutions na si personality kwa mara nyingine tena kama ilivyokuwa kwa Richard Nixon n.k nguvu ya umma imetamalaki. Kwamba, US hakuna mkubwa zaidi ya nchi na taasisi zake
Tumeshuhudia raia asiye na kitu anaitwa kituo cha kupiga kura ili athibitishe utata wa kura yake ili ihesabiwe.
Tumeshuhudia wakuu wa vituo 'county' wakiwa na maamuzi ya mwisho ya kura zilizopigwa na ndio waliojibu maswali na kuwajibika pale palipokuwa na utata bila kutishwa na chama chochote au polisi n.k.
Tumeshuhudia mawaka na kuhesabu kura kwa uwazi kila upande ukitia saini matokeo hata kama ni watu 2
Tumeshuhudia wagombea wakiheshimu uhesabu wa kura.
Katika furstration ya juu Joe Biden alijizuia kujitangaza.
Ni tofauti na Trump aliyetaka kuufanya uchaguzi wa Marekani kama wa 'third word'' ambako hakuna haki, uwazi wala uhalali wa kinachofanyika.
Mathalani, kwanini kura ipigwe kituo X na watu 100 halafu matokeo yasubiri kura hiyo iende wilayani, mkoani hadi ngazi ya Taifa ili kuhesabiwa? Hilo linachagiza rigging kitu ambacho mataifa makubwa hayafanyi.
Kura inahesabiwa pale pale ilipopigwa na kutangazwa pale pale.
Katika uchaguzi wa Marekani, tumeona pande zote zikipewa haki sawa za kisheria.
Hivi sasa timu ya Trump inakwenda mahakamani na hiyo ni haki, si fadhila.
Mahakama itasimama na kueleza nini kifanyike na haki itendeke. Dhana kwamba kuna majaji wengi aliowateua ina limitation zake. Katika masuala yenye masilahi na Taifa hilo hali si kama alivyofikiri
Katika hatua za awali, Trump alikwenda mahakamani akitaka kusimamisha uhesabu wa kura za commonwealth PA.
Mahakama ikasema kura zitakazosimamishwa kuhesabiwa ni zile zenye utata za eneo husika tu.
Trump na Republican walijaribu sana ' voter suppression' ili kuwatenga watu wa rangi kwa hoja moja kwamba majority ya Waamerika ni weupe.
Walichotaka ni watu wa rangi kusimama katika mistari wakiwa na vituo vichache na hivyo wengi kushindwa kupiga kura au vituo kufungwa kabla ya upigaji kura.Hii ndiyo sababu kubwa Trump hakutaka 'vote by mail''
Jaribio la kwanza lilikuwa kumweka Postmaster general na kumwagiza ahujumu usafirishaji wa masnduku.
Njia ilishindwa kwasababu mbili, kwanza kulikuwa na mbadala wa masanduku ya kutumbukiza kura na pili kulikuwa na fursa ya kupiga kura za awali.
Muhimu zaidi, viongozi wa taasisi wakisimama na kuzitetea taasisi za Kitaifa dhidi ya hujuma.
Kuna 'Trumpism' ambayo imeharibu Republican lakini sasa wengi watakuwa huru. Tatizo linalowakabili watetezi wa Trump ni historia. Mtu kama Seneta Rubio atalamba matapishi yake na Urais atausikia kama ilivyo kwa Lindsey
Kwa waliofuatilia uchaguzi wa Marekani kuna mengi ya kujifunza.
Kwamba, Taifa hilo si kamalilifu na bado lina mambo ya kurekebisha. Hata hivyo, uthabiti wa Taasisi za Marekani ni nguzo kubwa kuliko nguvu za majeshi yake. Kwamba Demokrasi inalindwa na Taasisi na si vyombo vya dola vya US.
Kwamba nguvu ya umma ndiyo kubwa kuliko mabomu, bunduki za kisasa na mitambo ya nyuklia ya Marekani.
Kwamba wananchi ndio wanaoamua hatma ya nchi yao, taasisi zikilinda haki za wananchi na vyombo vya dola vikihakikisha haki za Wamarekani zinasimamiwa kwa mujibu wa sheria.
Wamarekani wanaiishi kauli ya Rais Lincoln
'' Government of the people, by the people , for the people''
Tusemezane
Sasa utaelewa vipi? Wewe unasukumwa na nini? Kwa mawazo yako au uelewa wako Tundu Lisu kuwadi wa mashoga kweli anaweza kuwaletea maendeleo Watanzania? Tundu Lisu kuwadi mkuu, kibaraka kweli anaweka rehani nchi yetu kwa sababu tu anataka kushika kuwa rais? Watanzania wote wawe watumwa kwenye nchi yao?Ndio maana namshangaa mtu kama Wacha1...nashindwa kuelewa kwa nini anafurahia uchaguzi uliowezeshwa kuangushwa kwa Trump na hapo hapo akisifia uchafuzi tulioushuhudia nyumbani kwetu Tanzania. Watu kama Wacha1 nashindwa kabisa kujua kiwango cha uelewa wao kinasukumwa na nini...unafiki, ujinga, uoga au hila.
You are such a baby and an idiot! You don't even have any idea of what you are talking about, goodbye!Sasa utaelewa vipi? Wewe unasukumwa na nini? Kwa mawazo yako au uelewa wako Tundu Lisu kuwadi wa mashoga kweli anaweza kuwaletea maendeleo Watanzania? Tundu Lisu kuwadi mkuu, kibaraka kweli anaweka rehani nchi yetu kwa sababu tu anataka kushika kuwa rais? Watanzania wote wawe watumwa kwenye nchi yao?
Mlevi wa Konyagi kila mwezi alikuwa anakomba pesa za ruzuku at least more than 330million ambayo ipo kisheria , vile vile kuwachangisha wabunge wa Chadema. Je, alifanya nini kikubwa kuwezesha Chadema kupata ofisi, kuwa na wanachama nchi nzima, kuwa na ofisi nchi nzima na kutetea maendeleo yao? Je, alifanya nini Bungeni yeye binafsi na wabunge wengine wa Chadema? Je, hiyo Demokrasia mnayo dai ipo nje ya Chadema tu na sio ndani ya Chadema? Mimi niwe mwoga? Uoga wa kipi? Upo hapa kwa sababu ya watu wachache ambao walikuwa front line kuwezesha huu utumbo ambao unaandika. Therefore do not even go there. Mmeshindwa uchaguzi kwa vitu ambavyo Watanzania wote wanaviona kwa macho sio kuambiwa. Mimi sio Bendera fuata upepo.
View attachment Rais mpya wa Marekani huyooo.mp4Wacha1
Sina uhakika kama tupo katika 'same page'' kuhusu hoja ya Mag3
Tunaongelea uchaguzi wa Marekani na jinsi ambavyo taasisi za nchi hiyo zilivyosimama imara katika kulinda masilahi mapana ya Demokrasia ya nchi yao.
Mfano, Trump kwa kutumia mamlaka yake alimteua mtu alichangisha pesa zake kuua shirika la Posta.
Kila state ina utaratibu wake wa uchaguzi na hivyo taratibu nyingine mbadala zilifuatwa.
Pamoja na hayo Mahakama kama Taasisi nyeti ililazimisha shirika la Post lihakikishe masanduku yanafika kwa wakati
Wakati huo huo postmaster general aliitwa na kamati ya Bunge chini ya kiapo na kuahidi kufanikisha uchaguzi
Rais Trump alitaka uchaguzi wa 'vote by mail'' ufutwe kabisa. Taasisi zikamwambia hiyo si kazi ya Rais
Juzi Jumatano , Rais Trump alikuwa na maongezi na Gavana wa Arizona na Georgia kuwashawishi. Walikataa
Hiyo ni mifano tu lakini uharibifu ni mkubwa sana hasa katika taasisi kama DOJ. Hata hvyo uimara wa Taasisi hizo bado upo licha ya uharibifu. Majuzi wakati Trump anashangilia Bus la Biden kuzingirwa na wahuni wake, FBI wamefungua uchunguzi bila kujali ukubwa wa Rais.
Miaka 4 iliyopita kulikuwa na maandamano ya kumpinga Trump.
Wote walioandamana waliambiwa hawana haki ya kumuondoa Trump, wasubiri miaka 4.
Miaka 4 baadaye wale wale walionyimwa haki sasa wanapewa haki ndiyo shamra shamra tunazoziona
Rais Trump alisema kulikuwa na 'fraud' katika kura za 2016 ndiyo maana Hillary alishinda kwa popular vote
Trump aliunda tume ambayo baada ya kuchunguza ilibaini hakuna tatizo na hivyo alishindwa kufanya lolote
Marekani kuna kamisheni ya uchaguzi, hata hivyo shughuli za uchaguzi zinaratibiwa katika ngazi za vitongoji ,miji, majiji n.k. kwa kufuata sheria za state husika.
Mfano, kuna state zina vote kwa mail tu hakuna kituo cha uchaguzi.
Kuna state zinaanza kuhesabu kura za posta kwanza, halafu za watu waliopiga na zingine ni kinyume
Ukifuatilia kwa ukaribu uchaguzi wa Marekani una matokeo makubwa matatu
Urais ni Biden
Senate itabaki kwa GOP
House itabaki kwa Dems
Chaguzi zote zimefanyika na kura kuhesabiwa kwa haki na uwazi ndiyo maana kuna tofauti hiyo.
Haya yanawezekana kwasababu uchaguzi wa Marekani si mali ya mtu au watu au kundi la watu.
Si mali ya GOP au Dems, ni mali ya wananchi. Hakuna mamlaka juu ya kura za watu.
Hatukuona mabomu, virungu au FBI wakibeba maboksi.
Hatukuona wagombea wakitiwa ndani ili kupisha hujuma zinazoratibiwa na vyombo vile vile vinavyopaswa kutoa haki na kusimamia haki.
Hoja hapa si personality, ni mifumo na kwamba wenzetu mifumo yao inaruhusu kujitawala kwa maana kwamba wananchi ndio wenye mamlaka.
Hii ni tofauti na nchi zinazoendelea ambako uchaguzi ni njia ya kujenga uhalali si mchakato wa kupata uhalali.
Hapa ni kuwa kwa nchi za kiafrika '' the end justifies the means''.
Kwa tulichokiona Marekani ni ''legitimacy derived from institutional procedure''
Ni kwa msingi huo Mag3 anasema kuna uchaguzi kama tulioona , halafu kuna vitu vingine vinavyofanana na uchaguzi yeye akiita uchafuzi