Uchaguzi 2020 Uchaguzi utakuwa wa haki na uwazi – NEC

Uchaguzi 2020 Uchaguzi utakuwa wa haki na uwazi – NEC

desmond JJ

Member
Joined
Jul 6, 2012
Posts
55
Reaction score
27
mbarouk s mbarouk.jpg
Tume ya Taifa ya uchaguzi imesisitiza kuwa Uchaguzi utakaofanyika Tarehe 28 Oktoba, 2020 utakuwa huru, wa haki na wenye kuzingatia uwazi kwa mujibu wa sheria.

Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mstaafu Mhe. Mbarouk S. Mbarouk alipokuwa akihutubia Mkutano wa Wadau na Asasi mbalimbali za Uchaguzi Mkoani Iringa.

SOURCE: Daily News Tanzania
 
Tunatamani kuona vitendo zaidi kuliko maneno kwa mustakabali mwema wa taifa letu. Maneno yanayotolewa na bosi wake hayapendezi yeyote mwenye mapenzi mema na taifa hili.

Tunatamani ushindi (wa CCM au CHADEMA) usiwe wa malalamiko na masuto ya dhamiri. Ushindi wa wizi ni jinamizi lisiloondoka kichwani na kila wakati humsababishia mporaji kuwa na kisirani ili kuhalalisha ushindi.

Tume ikisimama imara tutavuka na watakaoshindwa kwa haki hawatakuwa na moral authority ya kulalamika. Wote tutawaona ni wendawazimu.
 
Huu ni ungese sasa. Vyombo vya habari vinatoa habari za wagombea wa chama tawala tu, NEC ya Muungano inamjibia hoja mgombea wa CCM, mass disqualification ya wagombea wa vyama vya upinzani... Hawa jamaa wameweka kichwa kwenye mchanga halafu wanajifanya kuwa hawaonekani.
 
CCM si wa kuamini hata kidogo, ni lazima wananchi tujipange kisawasawa!! wakileta ujinga - ni kumwaga mboga ili wote tuanze tulumangia!!
 
..NEC imekuwa kama mnara wa babeli.

..kila mtendaji anazungumza analojisikia.

..Katibu wa Nec anahimiza wapinzani wapigwe MABOMU.

..Makamu Mwenyekiti anadai uchaguzi utakuwa huru na wa haki.

..Only in Tanzania.
 
Huu ni UONGO wa mchana kweupe....

Uchaguzi haina maana ya siku ya kupiga kura tu hiyo tarehe 28/10/2020

Uchaguzi ni mchakato mrefu wenye stages mbalimbali hadi ile ya mwisho ya kutangaza mshindi....

Tulianza mchakato wa uchaguzi na hatua (stage) ya uchukuaji fomu za uteuzi wa wagombea, urejeshaji fomu hizo, uteuzi wa wagombea na sasa tupo kwenye hatua ya kampeni....

UHURU na UWAZI wa uchaguzi huu wa 2020 uliingia kwenye mashaka kuanzia ktk hatua ya uteuzi wa wagombea wa ngazi zote....

Mamia ya wagombea wa vyama vya upinzani hawajateuliwa kwa sababu za kijinga kabisa huku wa CCM eti kwa 100% wakiwa hawana kasoro hata moja....!

Kituko kingine kinachofanywa na NEC kuonesha UONGO wao na kuwa hakuna UHURU wala UWAZI ktk uchaguzi huu, wamekalia rufaa za wagombea kwa takribani mwezi na ushee mpaka sasa bila kutoa uamuzi bila sababu zozote za msingi....

Katika hatua ya sasa ya KAMPENI zinazoendelea, KAULI na MATENDO mengi ya NEC yanaonesha kuwa hakutakuwa na UHURU wala UWAZI katika hatua zinazofuata hadi kutangaza washindi....!!!

Wasitudanganye hata kidogo....
 
' Kuanzia sasa hivi mtaanza kuona watu wanapigwa mabomu' Aliyasema huyo mbwiga Mahera na kweli msafara wa Tundu na Mwalimu ukashambuliwa. Uhuru na haki hio 'kwio'.
 
Hilo haliwezi kutokea kama walikuwa wanawaeungua wagombea wa upinzani kwa mabavu iweje kuwe na uchaguzi huru na wa haki?
 
CCM si wa kuamini hata kidogo, ni lazima wananchi tujipange kisawasawa!! wakileta ujinga - ni kumwaga mboga ili wote tuanze tulumangia!!
Hakutakua na ugali mkuu fuso! Si wao wanamwaga mbogamboga, Sisi tumanwaga ugali? Au tunamwaga mbogamboga, tunaondoka na ugali!??
 
Uchaguzi ni process na hiyo process hainzii tarehe 28 October. Wagombea wa upinzani wameenguliwa kishenzi, sasa mwenye akili timamu hawezi sema uchaguzi utakuwa wa haki
 
Tume ya Taifa ya uchaguzi imesisitiza kuwa Uchaguzi utakaofanyika Tarehe 28 Oktoba, 2020 utakuwa huru, wa haki na wenye kuzingatia uwazi kwa mujibu wa sheria.

Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mstaafu Mhe. Mbarouk S. Mbarouk alipokuwa akihutubia Mkutano wa Wadau na Asasi mbalimbali za Uchaguzi Mkoani Iringa.

SOURCE: Daily News Tanzania

Hizo ni porojo tu. Tangu lini wakasema hautakuwa huru na haki?
Kama wanamaanisha, basi wamwite mgombea wa ccm wenye tume ya maadili kujibu shutuma za kutoa rushwa (kuagiaza utekelezaji wa miradi wakati yupo kwenye kampeni) na waziri wake mkuu kufanya kampeni ambazo hazipo kwenye ratiba ya tume.
 
Back
Top Bottom