Nilivyoelewa mada yako hii, ni kama umeweka mambo mawili tofauti kwa pamoja.Nawapongeza kwa kurasimisha concept ya bunge la wananchi ila sijapenda suala la Suzan Lyimo kuwa kiongozi Tena!!
Mtu ameshakua mbunge since 2010 akastaafu 2020 akakaribishwa Baraza la wazee how on earth anapewa active post??
Hili bunge ni kwa ajili ya active politics na liko kimkakati kwa wagombea wa Chadema 2025 waanze kuonekana mapema. So ni jambo jema watu kama Lumola na Shija kuibuliwa Leo ila sura zile zile kupewa Uspika sioni kama ni strategic kabisa na hapo tumefeli.
Na hii tabia haipo Chadema tu hata CCM, unakuta mtu ni waziri Bado anagombea ujumbe NEC wakati huo huo ni mbunge as if hakuna sura mpya!!
Iwekwe kanuni kwamba mtu mmoja kofia Moja haiwezekani Msigwa akawa mwenyekiti wa Kanda hapo hapo alikua mbunge hapo hapo ukute mjumbe wa kamati kuu!! Hapana waamue Moja na kingine waachie wengine nao wapate fursa ya kuonyesha uwezo wao.
Cc Erythrocyte Kalamu
Kwa mtu aliyewahi kuwa kiongozi, halafu akastaafu; baadae akaitwa tena kushika nafasi ya uongozi. Hili moja.
La pili, nilivyoelewa mimi, ni kwamba mtu bado ni kiongozi ambaye anashikilia cheo maalum ndani ya chama, halafu wakati huo huo, anasaka au anateuliwa kushika nyadhifa nyingine ambazo zitahitaji ufanisi wa kuzisimamia.
Hili la pili ninakubaliana nawe moja kwa moja.
Hilo la mwanzo, kama kiongozi alistaafu na rekodi nzuri ya utendaji, na bado anazonguvu za kukisaidia chama kufikia malengo yake, sioni tatizo kabisa juu ya hilo.
Na hasa ukichukulia, kwa mfano hilo la kuwa Spika wa Bunge, kazi ambayo nadhani inahitaji mtu ambaye, hata kama hakushika nafasi hiyo kabla ya kung'atuka kwake, lakini alifanya kazi zake kwenye taratibu zinazohusiana na cheo hicho, nadhani mtu huyo anafaa sana kurudishwa ili uzoefu wake usaidie shughuli za chama.