monde arabe
JF-Expert Member
- Oct 22, 2017
- 8,781
- 13,444
Noma sana!Uchaguzi huu umeshaingia influence za chama cha majizi ya kura inanipa wasiwasi sana kama utakamilika ukiwa huru na wa haki
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Noma sana!Uchaguzi huu umeshaingia influence za chama cha majizi ya kura inanipa wasiwasi sana kama utakamilika ukiwa huru na wa haki
Huko unguja TAL ana kura kweli😂Ijulikane mwanzoni kabisa kuwa Mkutano Mkuu wa CHADEMA ndiyo, kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho, chombo mahsusi cha kumchagua Mwenyekiti na Makamu wake wawili-wa Tanzania Bara na yule wa Zanzibar.
Mkutano huu mkuu wa CHADEMA hufanyika mara moja katika miaka mitano. Lakini, mikutano mikuu ya dharura au maalum yaweza kuitishwa kwa mujibu wa Kanuni.
Hadi hapo, ni wazi kuwa wajumbe wa Mkutano Mkuu ndiyo watakaomaliza utata siku ya uchaguzi. Akina nani hasa ni wajumbe wa Mkutano Mkuu? Kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA, Mkutano Mkuu unaundwa na:
(a) Wajumbe wote wa Kamati Kuu
(b)Wajumbe wote wa Baraza Kuu
(c) Wenyeviti wa Wilaya/Majimbo
(d) Makatibu wote wa Majimbo/Wilaya
(e)Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wanaotokana na Chama
(f) Wajumbe ishirini watakaochaguliwa na Mikutano Mikuu ya kila Baraza la chama kuingia kwenye Mkutano Mkuu Taifa kwa kama ifuatavyo:-
(i) Wajumbe kumi na tano kutoka Tanzania Bara
(ii) Wajumbe watano kutoka Tanzania Zanzibar kwa kila baraza
(g)Mjumbe Mwakilishi wa kila Wilaya
Ni vyema na haki kuwajua wajumbe wa Kamati Kuu na Baraza Kuu ili kupata mwanga wa nani hasa atahudhuria kwenye Mkutano Mkuu. Kamati Kuu ya CHADEMA inaundwa na:
(a) Mwenyekiti wa Taifa
(b) Makamu Mwenyekiti Bara.
(c) Makamu Mwenyekiti Zanzibar
(d) Katibu Mkuu
(e) Naibu Katibu Mkuu Bara
(f) Naibu Katibu Mkuu Zanzibar
(g) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayetokana na Chama
(h) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayetokana na Chama
(i) Rais wa Zanzibar anayetokana na Chama
(j) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar anayetokana na Chama
(k) Spika wa Bunge na Spika wa Baraza la Wawakilishi watokanao na Chama.
(l) Wawakilishi watano wa Wabunge wa Bunge la Muungano.
(m) Wajumbe watatu toka Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
(n) Wajumbe nane waliochaguliwa na Baraza Kuu kuingia Kamati Kuu kwa uwiano wa nusu kwa nusu wanaume na wanawake na mjumbe mmoja kutoka kila kundi atoke Zanzibar.
(o) Wawakilishi watano wa madiwani wa Chama, wawili wakiwa madiwani wa kawaida na watatu wawe Wenyeviti/Mameya wa Halmashauri zinazoongozwa na Chama. Wajumbe hawa watachaguliwa na umoja wa madiwani wa Chama.
(p) Wenyeviti wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee ngazi ya Taifa.
(q) Wajumbe wateule wasiozidi sita watakao teuliwa na Mwenyekiti Taifa kwa kushauriana na Katibu Mkuu na kuthibitishwa na Baraza Kuu angalau wawili wawe wanawake.
(r) Wenyeviti Wastaafu wa Chama ngazi ya Taifa .
(s) Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni au Waziri Mkuu atokanaye na Chama.
(t) Kiongozi wa Kambi ya Upinzani au Makamu wa Pili wa Rais kwenye Baraza la Wawakilishi atokanaye na Chama.
(u) Wenyeviti wa Kanda
(v) Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini atakuwa mjumbe asiye na kura.
(w) Wakurugenzi wa Kurugenzi za Chama watakuwa wajumbe wasio na kura.
(x) Makatibu wa Mabaraza ya Chama ngazi ya Taifa watakuwa wajumbe wasio na kura.
Baraza Kuu la CHADEMA linaundwa na:
(a) Wajumbe wote wa Kamati Kuu
(b) Makamu Mwenyekiti wa Kanda
(c) Makatibu wa Kanda
(d) Watunza Hazina wa Kanda
(e) Wenyeviti wa Baraza la Uongozi, Mkoa.
(f) Makatibu wa Mkoa
(g) Wajumbe wateule wasiozidi sita watakaoteuliwa na Mwenyekiti wa Taifa kwa kushauriana na Katibu Mkuu na kuidhinishwa na Baraza Kuu. Wajumbe wateule hawa watateuliwa kwa uwiano wa wajumbe wanne; wanaume na wanawake wawili.
(h) Wajumbe watano watakaochaguliwa na Mkutano Mkuu wa kila Baraza la Chama, kwa uwiano wa wajumbe wanne toka Bara na mmoja toka Zanzibar kwa kila Baraza.
(i) Wenyeviti wa Wilaya za Chama
(j) Makatibu wa Wilaya za Chama
Hao ndiyo wazee wa vichinjio katika siku, mahali na muda wa uchaguzi mkuu wa CHADEMA!
Na ccm safari hii lazima kuna kitu watajifunza kutoka Chadema.Unashangaa? Hapo ndio ujue kuwa huku Chadema sio CCM wanakosubiri uwe Rais basi wawakusanye wajumbe wa mkutano mkuu kisha wavunge uchaguzi kisha wanakutangaza mwenyekiti wa chama kwa kura 💯 %.
Maigizo matupu!
hapa unazingua kwa kuleta utani, bora ungesema atapata kura chacheLisu atapata kura 2 tu
Wamejifunza kuwa ,wanabaka demokrasia,kwa kudalalia nafasi za juu za chama,badala ya wanachama kugombea na kupigiwa kuraNa ccm safari hii lazima kuna kitu watajifunza kutoka Chadema.
Endelea kuamini ujinga wako kuna siku utaelewa kulingana na wakati.Kwa Katiba ya JMT 1977 na Katiba ya CCM ya 1977 Rais na Amiri Jeshi mkuu Lazima atoke CCM 😂😂
Kivipi mkuu?Huu uchaguzi unaweza kuleta maajabu ambayo haujawahi kutokea
Matokeo ya uchaguzi ni niniHuu uchaguzi unaweza kuwa na nguvu kubwa kuliko uchaguzi Mkuu wa October 2025 😀😀
Maajabu ni kwa mropokaji kukimbilia mahakamaniHuu uchaguzi unaweza kuleta maajabu ambayo haujawahi kutokea
Yeah ila ndio wapiga kura wengi inapokuja chaguzi za urais, ubunge & udiwani.wanaopiga kelele mitandaoni wengi hawapigi kura
kama akipata uraisi kwa tiketi ya chademaRais wa JMT ni mjumbe