Pre GE2025 Uchaguzi wa CHADEMA umedhihirisha Lissu ni Mwanaharakati Mbowe ni Mwanasiasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wajumbe Wana wasiwasi kuhusu uwezo wa Tundu Lissu kuongoza Chadema kama mwenyekiti, na kuna sababu kadhaa zinazoweza kuungwa mkono na mtazamo huu:
1. Historia ya Kiongozi
- Uzoefu wa Kisiasa: Ingawa Lissu ana uzoefu kama mwanasheria na mbunge, kukosekana kwa uzoefu wa moja kwa moja katika uongozi wa chama kikubwa kunaweza kumfanya asionekane kuwa na uwezo wa kutosha kuongoza chama katika mazingira magumu ya kisiasa.

2. Mgawanyiko na Mizozo
- Mgawanyiko wa Chama: Lissu anaweza kuwa na maono tofauti na wanachama wengine. Hali hii inaweza kuleta mgawanyiko na kuathiri umoja wa chama, jambo muhimu katika kuongoza chama kikubwa.

3. Uwezo wa Kujenga Ushirikiano
- Mahusiano na Wafuasi: Uwezo wa Lissu kujenga na kudumisha mahusiano mazuri na wanachama ni muhimu. Ikiwa hatashirikiana vizuri na wanachama, kuna hatari ya kupoteza uaminifu na ushirikiano wa ndani.

4. Athari za Kisheria
- Mizozo ya Kisheria: Tundu Lissu amekuwa katika mizozo ya kisheria na serikali, ambayo inaweza kuathiri hadhi ya chama na uwezo wake wa kuongoza. Hali hii inaweza kuleta changamoto zaidi katika uongozi.

5. Mtazamo wa Kisiasa
- Msimamo Mkali: Lissu anaweza kuwa na mitazamo ambayo ni makali au yanayopingana na sera za chama. Hii inaweza kumfanya asikubalike na wanachama wengine, na hivyo kuathiri uwezo wake wa kuongoza.

Hitimisho
Kwa mantiki hii, kuna sababu za msingi za kutokubaliana na wazo la kumchagua Lissu kuwa mwenyekiti wa Chadema.

Ni muhimu kwa wajumbe wa chama kuzingatia uwezo wa kiongozi kuleta umoja, kujenga ushirikiano, na kukabiliana na changamoto za kisiasa.
Uamuzi wa kuchagua mwenyekiti unahitaji uelewa mzuri wa uwezo wa kiongozi kuongoza chama katika mazingira magumu.
 
Mbowe: Siondoki kwasabb nimetumia fedha zangu nyingi sana ktk chama hiki

Mbowe: Mimi Sina njaa, nina vitega uchumi mpk nje huko, lkn wengine ni wabangaizaji tu.

Kauli hizi za Mbowe, ndiyo unamsifia kuwa anajenga taasisi???
Mamluki yke yanajikeshesh hku kumpamba..yn akifany kosa la kujikuta chama ni yeye tu anafaa kuw chea asibinue domo kutak katiba wkt udikteta ameuvaa
 
Reactions: G4N
Huenda siku za cdm kuendelea kuwa top ktk siasa za Tz zimeisha. Tusubiri tuone
 
Lissu labda ashinde Njaaa
 
Usikose kuja kuyanena hayo kwenye mdahalo japokuwa hadi sasa bado hujazibitisha kushiriki

Kifupi MBOWE miaka 21 imemtosha kwa kuwa muda wake haupo naye busara asubuli hilo sanduku la kura litakavyomuumbua

Atashindwa kwa kura ambazo hata ukiiba hawezi kushinda

Mark maneno haya 80% ndio ushindi wa LISSU trh 21
 
Mbowe: Siondoki kwasabb nimetumia fedha zangu nyingi sana ktk chama hiki

Mbowe: Mimi Sina njaa, nina vitega uchumi mpk nje huko, lkn wengine ni wabangaizaji tu.

Kauli hizi za Mbowe, ndiyo unamsifia kuwa anajenga taasisi???
Kuna uongo Gani hapo?
 
Badilisheni mada! Sikilizeni hii maneno sasa
 

Attachments

  • VID-20241228-WA0044.mp4
    23.2 MB
Hahaha Team Lisu kama Team Wema, kelele kila kona.

Mbowe yeye katulia anapiga kampeni kimya kimya tu, Kura itaamua mshindi.

Team Lisu hamuoni aibu kupiga kelele hovyo hovo kiasi hiki?
 
Kwa uchache maandishi.
Lisu bado si mwanasiasa ila mwanaharakati.

LIsu bado hana uwezo wa kuongoza chama cha siasa kama mwenyekiti

Lisu ni mzuri akiwa chini ya uangalizi na akiwa anapangiwa nini cha kufanya na kipi si cha kufanya hasa yale mambo makubwa.

Mbowe ni mzuri sana kwenye uongozi na kiongozi.
 
 
Tulipo hatuitaji Mwanasiasa Bali Kiongozi asiyefata script na kuleta Sanaa na hadaa za kishamba.
Matokeo ya kuleta siasa na kukwepa uwajibikaji ndio chanzo Cha hapa tulipo.
 
Chadema inahitaji uongozi wenye HYBRID yaani mwansiasa mwenye sura zote mbili kulingana na mazingira ya kisiasa ya sasa na muktadha wa mapambano mapya yaliyopo. mwana siasa aliye na uanaharakati sehemu kadhaa na mwanadiplomasia mazingira kadhaa. hapo rangi mbili hazina budi kutumika. CCM imebadili maxingira ya siasa zake. inahitaji vyote viwili kuiendea.
 
Lissu anaweza kuongoza iwapo tu atakuwa karibu sana na Mbowe kumshauri na kumshirikisha kwenye mambo mengi kama Mzee wa Chadema kwa muktadha ya siasa za nchi hii. Na pia asimame na siasa za ndani kuwaleta pamoja wanachama na kutowatumikia sauti ya watanzania ambao wanaweza kuigeuka chadema na kuitelekeza au kuendesha uanaharakati kwa mgongo wake. Hapo ndipo penye Paradox
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…