Uchaguzi wa Kiteto: Taarifa mbalimbali

Uchaguzi wa Kiteto: Taarifa mbalimbali

Status
Not open for further replies.
sawa tusubiri uchunguzi ila inaonekana tumefika pahala sasa mtu asiumwe tutatafuta mchawi

basi hizi dini tuzifuteni na tuamini kila aumwae kuna njama ziwe za kisiasa au kishirikina


watanzania tunaelekea wapi?
 
sawa tusubiri uchunguzi ila inaonekana tumefika pahala sasa mtu asiumwe tutatafuta mchawi

basi hizi dini tuzifuteni na tuamini kila aumwae kuna njama ziwe za kisiasa au kishirikina


watanzania tunaelekea wapi?

Sema wewe kiazi.... nikisema mimi mhogo mchungu...
 
si unajua tena tanzania hakuna anayeumwa isipokuwa amelogwa na hakuna anayekufa isipokuwa kwa ulozi wa aina fulani.
 
Rwanda, Burundi, DRC,Kenya, Uganda, Msumbiji, Malawi, Zambia na Tanzania wote ni jamii moja.

Kinachotokea kwa jirani vile vile kinaweza tokea kwetu. Sana sana hapo ni trigger mechanism.

Kama waliokabidhiwa dhamana ya kuongoza si makini, lolote laweza kutokea Tz pia, japo hatuombei iwe hivyo
 
Hii habari ikithibitishwa kwamba ni sumu itakuwa mbaya sana kwa nchi yetu.

Lengo hapa ni kuua na tukianza kuuana kwasababu ya mambo ya politics basi tunaelekea kubaya mno.

Wacha tusubiri na kusikia madaktari watasema nini ila inaelekea Tanzania tunaelekea huko waliko Kenya sasa. Hata wao walianza na ujinga mdogo mdogo na sasa wamefika pabaya mno.

Kaka hakuna wakumwekua sumu huyo jamaa yenu kwa kuwa si kweli kwamba nitishio kiwango hicho.ata hivyo nashukuru madokta waliogundua kuwa ni maambukizi ya njia ya mkojo ambayo huwa ina magonjwa mengisana kuanzia yanayosababishwa na uchafu mpaka magonjwa ya zinaa.anyway poleni sana
 
Mgombea kambi ya upinzani apata nafuu baada ya kula sumu
Na Salim Said, MUM

HALI ya mgombea ubunge wa jimbo la Kiteto kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Victor Kimesera aliyelazwa katika Hospitali ya Aga Khan jijini, Dar es Salaam baada ya kuugua ghafla mwishoni mwa wiki iliyopita akidhaniwa kula chakula kilichokuwa na sumu inaendelea vizuri.


Hayo yalisemwa jana na Dk Isaya Tosiri ambaye anashughulika na matibabu ya Kimesera alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake jana.


Alisema hali ya Kimesera inaendelea ukilinganisha na hali aliokuja nayo juzi akitokea katika hospitali ya wilaya ya Kiteto mkoani Manyara.


Alisema baada ya kupigwa picha ya Xray na uchunguzi zaidi madaktari wamebaini kuwa hakuna dalili yoyote ya mgonjwa huyo kula chakula ambacho kilikuwa na sumu na kuongeza kuwa tatizo lililoonekana ni njia ya mkojo na kwa sasa wanatumia mpira kuutoa mkojo huo.


�Hakuna dalili yoyote ya sumu iliyooneshwa na vipimo vyetu isipokuwa tatizo ni njia ya mkojo ambayo ilikua haifanyi kazi vizuri na sasa tumemfunga mpira kuutoa mkojo huo na anakula anaongea vizuri, alisema Tosiri.


Alisema mwanzo walidhania kuwa kungekua na haja ya kumfanyia upasuaji lakini baada ya kumfanyia uchunguzi waliona hakuna haja ya kumfanyia upasuaji wa aina yoyote.


Aliongeza kulingana na uchunguzi wao inaonekana kuwa chanzo cha ugonjwa wa mteja wake ni tatizo la kihistoria kwani Kimesera alishawahi kupata ugonjwa huo mnamo mwaka 1999.


Akizungumzia hali yake hospitalini hapo jana, alisema anaendelea vizuri na aliwatoa wasiwasi wafuasi wake na kuongeza kuwa amesikia huenda leo akapata ruhusa ambapo alisema atapumzika Dar es Salaam siku moja na Alhamisi atarejea Kiteto kuendelea na mapambano.


Alisema siasa ni mapambano, yanahitaji hadhari ya hali ya juu kwani inawezekana kuna watu ambao wapo tayari hata kutoa uhai wa mtu, ili waingie madarakani na kuongeza kuwa hana uhakika na chanzo cha ugonjwa wake kuwa ni sumu au la.


Dk Ben Kapwani wa Uhuru Dispensari ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Iringa ambaye alisafiri Kimesera alisema yeye ndye aliyempatia huduma ya kwanza kwa kumpa dawa ya kutapika na kuongeza kuwa kwa uzoefu wake inawezekana alikula chakula chenye sumu.
 
haaaa haaaa

unaona mambo haya hata maradhi watu huyachukulia advantage ya kujenga utashi wa kisiasa.

maelezo ya madaktari yako wazi bado wanataka kuspin.

mungu amejaalia kuwa yu hai angekufa pangekuwa hapatoshi.

mungu akupe uzima na nguvu ukaendeleze kampeni ila haya mambo ya uongo usiyavae mungu atakusuta na utashindwa
 
Kituko kingine hiki cha wahandisi wetu wa habari heading inasomeka hivi;


Mgombea kambi ya upinzani apata nafuu baada ya kula sumu
Na Salim Said, MUM

Halafu ukisoma kwenye main body unakuta vitu tofauti kabisa!

Alisema baada ya kupigwa picha ya Xray na uchunguzi zaidi madaktari wamebaini kuwa hakuna dalili yoyote ya mgonjwa huyo kula chakula ambacho kilikuwa na sumu na kuongeza kuwa tatizo lililoonekana ni njia ya mkojo na kwa sasa wanatumia mpira kuutoa mkojo huo.

Hawa nao wanahitaji semina elekezi ya Ngurdoto....
 
Labda kuna mtu alimroga hadi kibofu cha mkojo kisifanye kazi maana teknolojia ya wabongo si utani..
 
Hata ww MKJJ unaamini hayo? pls usidhihaki wananchi.profile yako kubwa bro...
Tukubali kuwa pale HAKI inapochanua na Batili/Uongo tujitenge nayo
 
Anataka kura za "sympathy", haya mambo ya kukurupuka sijui kuna mkono wa CCM yanawashuhsia hadhi wapinzani, haya sasa mambo hadharani.................
 
Mtu wa Pwani usishangae hilo bcs kuna siku Fisadi mtoto aliwahi kumwambia Mwafrika wa KIKE kua anamawazo ya KIJIMA bcs ktk Primitive society kila kitu tunahusisha na mkono wa mtu.

Sasa hapa kuna vitu viwili wanataka tuamini kua sisi CCM tumemfanyia ktu mbaya jamaa ili wapate KURA ZA HURUMA na kuidanganya jamii abt hujuma kama kawaida ya wapinzani wa nchii hii.

Ukitazama watu wenye mawazo mgando hutafuta majibu Rahisi na ya haraka.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
 
CCM watafanya kila liwezekanalo ili "washinde" Kiteto. Si kwamba wana wabunge wachache, bali ni kutokana uchu wao na nia yao ya KUHODHI madaraka. Wana uchu wa madaraka wa kupindukia, na ikibidi wataiba kura ili "washinde". Wameshafanya hivyo mara nyingi sana. Sote tunajua hivyo, so I don't want anyone coming here with this "show me the evidence" nonsense.

Kwa bahati mbaya, Usalama wa Taifa umejikita CCM. Wanadhani kulinda maslahi ya nchi ni pamoja na kuisaidia CCM katika mbinu zake za wizi wa kura. Their loyalty should have been to the nation rather than to CCM.

Wapinzani waangalie sana mbinu zitakazoweza kutumika na CCM kuiba kura wakati huu. Waangalie vile vile kama CCM itaiba tena fedha za taifa na kuzitumia kuhonga wapiga kura kama ilivyofanya kwenye chaguzi zilizopita.

We have a problem in Tanzania, and it is called CCM. Haiwezekani kuleta utawala bora wa kisheria na kukomesha rushwa hadi CCM ikae upinzani kwanza, kwa miaka mitano hadi kumi. Ni kweli, lakini kwa vile wako madarakani sasa na wanahodhi madaraka yote, ni kazi sana kuwazuia kuiba kura ili waendelee KUHODHI MADARAKA.

Tegemeo la Taifa ni Dr. Slaa. Tunadhani ataweza kuwathibiti.
 
Hakuna kura za maoni tukajua kunaendeleaje huko? Au CCM haijaona umuhimu wa kuitumia REDET wakati huu?
 
Kuanguka kwa baraza la mawaziri kutawanufaisha wapinzani kushinda kiteto ama CCM itakuwa imejisafisha na kuanza kupata ajenda ya kujitetea kuwa wanaisafisha serikali na chama?
 
Pia kwa taarifa tuu ni kuwa nimepata habari za uhakika kuwa kimesera kesho anategemewa kwenda Kiteto kuendelea na kampeni zake na kuwashawishi wananchi wake.

Nitaendelea kuwapa updates kwani hapa inaonekana kama tumesahau huu uchaguzi ambao ni muhimu sana pia kwenye historia ya taifa hili.

Mteule wa CCM ni chaguo la aliyekuwa waziri mkuu je?kuanguka kwa waziri mkuu kutaadhiri vipi uchaguzi huo?
 
Pia kwa taarifa tuu ni kuwa nimepata habari za uhakika kuwa kimesera kesho anategemewa kwenda Kiteto kuendelea na kampeni zake na kuwashawishi wananchi wake.

Nitaendelea kuwapa updates kwani hapa inaonekana kama tumesahau huu uchaguzi ambao ni muhimu sana pia kwenye historia ya taifa hili.

Mteule wa CCM ni chaguo la aliyekuwa waziri mkuu je?kuanguka kwa waziri mkuu kutaadhiri vipi uchaguzi huo?

Mpaka Kieleweke,

Bado upo na Kiteto tu? wenzio wapo busy na mambo yana vinjari huko Idodomya!

Talk abt twisting priorities up side down!
 
" maambukizi ya njia ya mkojo ambayo huwa ina magonjwa mengisana kuanzia yanayosababishwa na uchafu mpaka magonjwa ya zinaa."
Kama kweli Doctor huyo alitoa Diagnosis ya mgonjwa huyo kama hivyo basi he has breached CONFIDENTIALITY AND MUST PAY A LOT
 
Mpaka Kieleweke,

Bado upo na Kiteto tu? wenzio wapo busy na mambo yana vinjari huko Idodomya!

Talk abt twisting priorities up side down!


Nipo huko kwani hili nalo ni tukio ambalo hatupaswi kulisahau pia humu kwani mchakato unaendelea.

watu wananikwaza huko Dodoma kwani unakuta wengine mara wanaandika kuwa waziri mkuu ni Salim ,hata hawajui kuwa masharti ya katiba ni hadi mtu awe mbunge tena wa kuchaguliwa jimboni na sio kuteuliwa?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom