Uchaguzi wa Kiteto: Taarifa mbalimbali

Uchaguzi wa Kiteto: Taarifa mbalimbali

Status
Not open for further replies.
Aliyekamatwa akinunua shahda anaitwa; Mohamed Bakari.

Ambaye ni mwenyekiti wa kitongoji cha matui ,pia balozi wa CCM .

Alikutwa na shahada za wapiga kura na waliokuwa na hizo shahada walipoulizwa walisema kuwa aliwaendea na kuwaambia kuwa kama hawatampa basi wangefukuzwa hapo kijijini na hilo ni agizo la serikali.

Kesi hivi sasa ipo kituo kidogo cha polisi Matui.

La ajabu ni kuwa polisi wanataka kusuluhisha jambo hilo na hawataki kufungua jalada kama inavyotakiwa kwani wao wanataka kusuluhisha .....

Ntaendelea kuwapa news kuhusu kiteto na haswa baada ya bunge kuahirishwa najua wote sasa tutajielekeza huko uwanja wa mapambano.

Tingatinga halijafika ,ila kuna taarifa kuwa litafika w.end hii huku yupo makamba na timu yake pia TOT wapo huku na badala ya kufanya hamasa wamekuwa wakipiga nyimbo usiku na kudai viingilio wananchi kuhudhuria.
 
Mwanakijiji ,soma PM zako tayari nimekutumia namba za simu za polisi wa huko kiteto.
 
Aliyekamatwa akinunua shahda anaitwa; Mohamed Bakari.

Ambaye ni mwenyekiti wa kitongoji cha matui ,pia balozi wa CCM .

Alikutwa na shahada za wapiga kura na waliokuwa na hizo shahada walipoulizwa walisema kuwa aliwaendea na kuwaambia kuwa kama hawatampa basi wangefukuzwa hapo kijijini na hilo ni agizo la serikali.

Kesi hivi sasa ipo kituo kidogo cha polisi Matui.

La ajabu ni kuwa polisi wanataka kusuluhisha jambo hilo na hawataki kufungua jalada kama inavyotakiwa kwani wao wanataka kusuluhisha .....

Ntaendelea kuwapa news kuhusu kiteto na haswa baada ya bunge kuahirishwa najua wote sasa tutajielekeza huko uwanja wa mapambano.

Tingatinga halijafika ,ila kuna taarifa kuwa litafika w.end hii huku yupo makamba na timu yake pia TOT wapo huku na badala ya kufanya hamasa wamekuwa wakipiga nyimbo usiku na kudai viingilio wananchi kuhudhuria.

Ndio kwanza kumekucha Kiteto, Kiteto, Kiteto...
 
Sumaye na Mary Nagu wao wamepangiwa kata moja ya Engusero ...kunani hapo?

Kura za hapo ni 7000+ sasa hapo nasi tutamwekea Sumaye kiboko yake naamini mnanielewa nikisema kiboko yake .......
 
Sumaye na Mary Nagu wao wamepangiwa kata moja ya Engusero ...kunani hapo?

Kura za hapo ni 7000+ sasa hapo nasi tutamwekea Sumaye kiboko yake naamini mnanielewa nikisema kiboko yake .......

Mhh hii combination sipati picha.....
 
Hapa mwaweza kuona jinsi ambavyo hawa jamaa wanatumia nguvu kubwa kwenye kushinda uchaguzi,je?nguvu ya pesa ikoje kama hii ni ya watu tuu???????/
 
Hapa mwaweza kuona jinsi ambavyo hawa jamaa wanatumia nguvu kubwa kwenye kushinda uchaguzi,je?nguvu ya pesa ikoje kama hii ni ya watu tuu???????/

Ni dhahiri nguvu unayo isema hapo ni ya pesa!! si nguvu ya hoja, mzee!! hao ndivyo walivyo!!
 
Hapa mwaweza kuona jinsi ambavyo hawa jamaa wanatumia nguvu kubwa kwenye kushinda uchaguzi,je?nguvu ya pesa ikoje kama hii ni ya watu tuu???????/

Kieleweke:
Na haya ndio matatizo tunayotakiwa kuyapigia kelele sana, kwani yanatuharibia kuwa na demokrasia ya kweli. Nadhani kuna umhimu mkubwa wa kuwa na mjadala mkubwa wa kitaifa kuhusu mambo haya; ikiwa ni pamoja na kuchambua sehemu za katiba yetu zinazotunyima haki ya kuwa na uhuru wa kweli kwa kila mwananchi. Tatizo lililopo nadhani ni kukosa waanzilishi na wasimamizi mahiri wa kuwashawishi wananchi na kusimamia vizuri kazi kama hiyo.

Civil Societies zetu ndizo zingekuwa na nguvu hii, lakini sielewi ni kwa nini hawashughulikii haya.

Vitendo hivyo wanavyovifanya CCM ni kuwanyima haki ya msingi wananchi kujiamlia mambo yao. Mwisho wake tunajua ni yale yale yanayotokea huko Kenya.

Watu wakisema wanaambiwa katiba yetu ni nzuri haihitaji mabadiliko! Ni nzuri kwa manufaa ya nani? Hata kama ni nzuri, kuna ubaya gani wa kuipitia kipengele kwa kipengele kitaifa ili pale tunapoona hapafai tupabadilishe?
 
Kesho kuanzia kama saa nane za mchana KLH News itakuletea matangazo ya hatua za kampeni kutoka Kiteto. Licha ya kuona nini kinaendelea tutapata nafasi ya kuzungumza na viongozi wa serikali na siasa.

Muda ni ule ule kupitia idhaa yenu ile ile ya bongoradio!!!

Nina lineup ya viongozi wengi, lakini tunahitaji msaada..

- Prof. Shivji
- Mhe. Eng. Stella Manyanya
- Mhe. Dr. Mwakyembe

na wengine wengi!!

na wengine wengi, tunaomba support ya kila aina maana hapa ndipo kufilisika kunapokaribia!!!

Dola 15 inaleta mahojiano ya karibu saa nzima!! So please support KLH News http://www.klhnews.com
 
Taarifa niliyopata kwa mwanachama mwenzetu Zitto ambaye yupo Kiteto ni kuwa Polisi wamewavamia wanachama wa CHADEMA wakiwa kwenye mazoezi ya nyimbo na Dereva wao (Baraka) amepigwa kisu, Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa Joseph Fuime, Mkurugenzi wa kampeni Ndg Msafiri Mtemelwa na Afisa Mwandamizi Sera ndg Juju Danda wamepigwa vibaya sanana Polisi.

Najaribu kuwasiliana naye zaidi na OCD wa Kiteto kujua nini zaidi. I will keep you notified on the progress
 
Nimeongea na Zitto sasa hivi na kwa kadiri ya maelezo yake ni kuwa Dereva huyo kachomwa kisu cha mbavu mbele za polisi na akaondoka bila hata kuguswa. Kinachosikitisha ni kuwa eneo walilofanyiwa uonevu huu ni eneo ambalo halikuwa na masuala ya kampeni na wanachama hao walikuwa wanafanya mazoezi ya kwaya (nyimbo za kichama).

My take:

Njia ya kuwamaliza wapinzani kisiasa isiwe kimabavu; hoja ikijibiwa na hoja inapendeza zaidi kuliko kuiga njia hizi za kidikteta. Tunahitajika kulipigia kelele suala la matumizi makubwa ya nguvu, bado ni tatizo Tanzania.
 
Tumefikia hapo ? OCD anasemaje baada ya Zitto ?Uchaguzi wa Kiteto kwani lazima watu wafe ? Je hali ya dereva ikoje ?
 
Haya nyie mapolisi na usalama wa taifa mnaopitia humu, fanyeni kazi sio mnakodolea tu, haraka tunaka haki itendeke.
 
Haya nyie mapolisi na usalama wa taifa mnaopitia humu, fanyeni kazi sio mnakodolea tu, haraka tunaka haki itendeke.

Nakubaliana nawe kabisa ndugu Zomba this is evil na kama JK atakaa kimya will be so damaging
 
Tumefikia hapo ? OCD anasemaje baada ya Zitto ?Uchaguzi wa Kiteto kwani lazima watu wafe ? Je hali ya dereva ikoje ?
Nimepata ujumbe toka kwa Zitto sasa hivi, anasema eneo lilolotokea vurugu ni Kijungu ambapo Pius Msekwa kaweka kambi yake.

Kata ya Kijungu iko mpakani mwa wilaya ya Handeni na dhamira ya kuweka kambi pale inaelekea ni ili watu wapelekwe Kiteto kupiga kura. CHADEMA wanadai wameweka ulinzi mkali ndo maana CCM wamepata hasira na kutumia nguvu za ziada kuharibu mambo.

Zitto, Dr. Slaa, Grace Kihwelu na Lucy Owenya wanaelekea Polisi sasa kuonana na OCD. Majeruhi wamepelekwa hospitali
 
Polisi hawawezi kusaidia chcochote badala watatoa ahadi ya kuwasaka na kuwatia hatiani wahusika, lakini amini usiamini vitendo hivyo vitaendelea ili kuwatisha watu na baada ya uchaguzi watasema uchaguzi ulikuwa free and fair. hakukuwa na intimidation yoyote. Endelea kutuletea habari sisi tulio huku Iguguno.
 
Mugo"The Great";143979 said:
Endelea kutuletea habari sisi tulio huku Iguguno.
Ya mwisho ambayo imenisikitisha ni hii taarifa ya mwisho ya Zitto:

"Tumefika hospitali na kukuta daktari kalewa ile mbaya, wagonjwa wetu hawajapewa matibabu labda kesho" what a statement! Inasikitisha sana.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom