Uchaguzi wa Kiteto: Taarifa mbalimbali

Uchaguzi wa Kiteto: Taarifa mbalimbali

Status
Not open for further replies.
Dah, kumbe hata mkuu wa kituo alikuwa chakari pia. Aliwapa kichapo watu na kuondoka ndani ya gari ya CCM. Hivi Tanzania ipo Dar tu?
 
Natafuta namba ya Zitto anayo weza kupatikana ama anayo patikana kwa sasa .Naomba aliye nayo anipe please
 
This is free press for Opposition as long as our reporters and political opperatives will be quick to act.

Perfect opportunity to put Kikwete on spotlight, if he is to have another press conference with George Bush.

Someone ought to ask Kikwete what is his stand on Tanzanian Police acting as stooges or an armed force of the ruling party to suppress opposition ? can he explain if Tanzanian government is partner for change and he is AU chairman, how can anyone trust his leadership if Police which is a government institution entrusted to protect and serve the nation is biased and act as agents for rulling party, by beating up opposition party members or delay to act on injustice practice done by CCM?

How can he Kikwete expect to mend the conflict in Kenya if he is silent about Police and CCM tacticts in his own country?
 
Ya mwisho ambayo imenisikitisha ni hii taarifa ya mwisho ya Zitto:

"Tumefika hospitali na kukuta daktari kalewa ile mbaya, wagonjwa wetu hawajapewa matibabu labda kesho" what a statement! Inasikitisha sana.

Wengine itabidi kusubiri kabla ya kutoa comments zetu juu ya hili la wana CHADEMA kupigwa, maana ile ya kupewa sumu, tuliingia kichwa kichwa kumbe hakuna cha sumu.

Kuhusu hizo hospitali za wilayani, ni ukweli unaojulikana, mimi niliwahi hata kuandika hapa JF, hospitali za wilaya huwa hazina huduma hasa kwa weekend. Kwanini? Naona ni uzembe wa viongozi wa wilaya.

Mimi sikuamini nilipofika hospitali ili kumpeleka mgonjwa wangu nikaambiwa mpaka Jumatatu. Nilijaribu kutumia influence yote niliyokuwa nayo hapo wilayani lakini haikusaidia.

Matatizo kama haya yanaweza kutatuliwa bila hata kuwahusisha viongozi wa taifa. Wabunge walio wengi wamelala na wanashinda kwenye kamati kiasi kwamba hata matatizo madogo kama hayo hawayaoni, hawayajui na wanashindwa kuyatatua.

Kama jimboni kwa Zitto kuna huduma wakati wa usiku na hasa weekend basi wamefanikiwa sana. Sitashangaa nikisikia hata huko mambo ni hivyo hivyo tu. Mara nyingi waheshimiwa huwa hata hawajui (out of touch).

Matatizo ya Tanzania ni makubwa mno na hata tukiondoa ufisadi kwa asilimia 100 bado matatizo zaidi ya asilimia 80 yatabaki tu. Capacity ya viongozi kule wilayani iko chini mno!
 
This is free press for Opposition as long as our reporters and political opperatives will be quick to act.

Perfect opportunity to put Kikwete on spotlight, if he is to have another press conference with George Bush.

Someone ought to ask Kikwete what is his stand on Tanzanian Police acting as stooges or an armed force of the ruling party to suppress opposition ? can he explain if Tanzanian government is partner for change and he is AU chairman, how can anyone trust his leadership if Police which is a government institution entrusted to protect and serve the nation is biased and act as agents for rulling party, by beating up opposition party members or delay to act on injustice practice done by CCM?

How can he Kikwete expect to mend the conflict in Kenya if he is silent about Police and CCM tacticts in his own country?

Yeah, hakuna wakati mzuri kama huu wakati Tanzania ikiwa kwenye focus ya World media. Na hapo Kikwete hapendi kabisa kuchafuliwa sifa zake anazozizolea.

Wapinzani waitumie vizuri nafasi hii kuondoa manyanyaso wanayoyapata ya mara kwa mara kutokana na polisi na vyombo vingine vya kitaifa vinavyotumiwa na CCM kama mali yao.

Kama jambo hili ni kweli, basi tunayo matatizo makubwa na hii CCM yetu; ni lazima wakomeshwe uonevu huu.
 
Wengine itabidi kusubiri kabla ya kutoa comments zetu juu ya hili la wana CHADEMA kupigwa, maana ile ya kupewa sumu, tuliingia kichwa kichwa kumbe hakuna cha sumu.

Kuhusu hizo hospitali za wilayani, ni ukweli unaojulikana, mimi niliwahi hata kuandika hapa JF, hospitali za wilaya huwa hazina huduma hasa kwa weekend. Kwanini? Naona ni uzembe wa viongozi wa wilaya.

Mimi sikuamini nilipofika hospitali ili kumpeleka mgonjwa wangu nikaambiwa mpaka Jumatatu. Nilijaribu kutumia influence yote niliyokuwa nayo hapo wilayani lakini haikusaidia.

Matatizo kama haya yanaweza kutatuliwa bila hata kuwahusisha viongozi wa taifa. Wabunge walio wengi wamelala na wanashinda kwenye kamati kiasi kwamba hata matatizo madogo kama hayo hawayaoni, hawayajui na wanashindwa kuyatatua.

Kama jimboni kwa Zitto kuna huduma wakati wa usiku na hasa weekend basi wamefanikiwa sana. Sitashangaa nikisikia hata huko mambo ni hivyo hivyo tu. Mara nyingi waheshimiwa huwa hata hawajui (out of touch).

Matatizo ya Tanzania ni makubwa mno na hata tukiondoa ufisadi kwa asilimia 100 bado matatizo zaidi ya asilimia 80 yatabaki tu. Capacity ya viongozi kule wilayani iko chini mno!

Eeeeeh, Mtanzania, kama tumefikia hapo pa kuambiwa njoo Jumatatu, tena hospitali ya Wilaya?
Ninachoweza kusema hapa ni kwamba hatuwezi kwenda chini zaidi ya hapo. Kwa hiyo labda sasa tujipe moyo tu kwamba 'graph' yetu itaanza kupanda.

Kwa mara ya mwisho nilipokuwa kijijini, pale Zahanati wananchi walikuwa na nafasi ya kwenda hadi usiku kumwamsha mganga amhudumie mgonjwa wa dharura. Hiyo ilikuwa ni miaka ileee, sijui sasa hali ilivyo.
Lakini hilo la hospitali ya wilaya? Hapo panatisha!
 
Napenda kuwapa taarifa wote kwamba baada ya simu yako Mwanakijiji kwa OCD ameamka na ameanza ku cooperate .He got shocked kwamba habari zimefika Ulaya na USA na kwa kweli naamnbiwa polisi wameanza kuamka na kujua it is getting real .Habari za uhakila ni kwamba CCM wameamua kuvurga uchaguzi baada ya Chadema kufanya mambo kama yale ya Tarime .Ulinzi Mkali eneno ambao Msekwa kaweka kambi .

Naambiwa CCM imeleta vijana 30 wanawaita makomandoo na wanafanya kazi ya ku terrorise watu .Napata habari kwamba sasa Chadema uongozi umefikia makubaliano na polisi kwamba waonane kesho .

More news to come .
 
Mkuu,

Ni kweli tupu, weekend sana sana unaweza kumkuta nurse tu na daktari wa wilaya na wasaidizi wake wameenda kutia maji.

Maisha ya maskini Tanzania yako mikononi mwa mungu. Mimi nilijiuliza sana, ukipata ajali mbaya muda huo, jua utakufa tu.

Bahati mbaya hata mambo madogo kama hayo, tunataka mpaka rais au PM aingilie kati. Viongozi wa wilaya wanafanya nini?
 
Ukweli wa mambo ni kwamba hali ya demokrasia Tanzania ni mbaya sana kuliko tunavyofikiria. Hatujaiona kwa sababu upinzani haukuwahi kuwa tishio. Sasa hivi ambapo upinzani unazidi kuimarika tutashuhudia madhira mengi sana ya CCM. Hawa ni watu hatari ambao hawaamini kama kuna mtu mwingine anastahili kushinda uchaguzi zaidi yao hata kama wananchi wawakatae vipi. Upinzani unavyozidi kupata ngumu tutashuhdia unyama wa CCM kuliko tuliowahi kuuona Zanzibar. Na tutajua kwamba vyombo vyetu vya usalama vipi kwa ajili ya kuilinda CCM ibaki madarakani first and foremost.
 
Nakubaliana na Kitila, unyama na uharamia wa CCM unaanza kujionesha wazi hivi sasa. Wameshaona jinsi upinzani unavyokuwa serious and that will make them act in the same way as they have been acting in Zanzibar. Na muda huu ambapo George Kichaka yupo bongo ndio wakati muafaka wa kumtoa nishai huyu Kikwete kuhusu mbinu za chama chake za ku-supress upinzani.
 
Bado hatujasahau yalyotokea Kenya, yanaibuka hapa hapa kwetu mbele ya macho yetu.
 
Napenda kuwapa taarifa wote kwamba baada ya simu yako Mwanakijiji kwa OCD ameamka na ameanza ku cooperate .He got shocked kwamba habari zimefika Ulaya na USA na kwa kweli naamnbiwa polisi wameanza kuamka na kujua it is getting real .Habari za uhakila ni kwamba CCM wameamua kuvurga uchaguzi baada ya Chadema kufanya mambo kama yale ya Tarime .Ulinzi Mkali eneno ambao Msekwa kaweka kambi .

Naambiwa CCM imeleta vijana 30 wanawaita makomandoo na wanafanya kazi ya ku terrorise watu .Napata habari kwamba sasa Chadema uongozi umefikia makubaliano na polisi kwamba waonane kesho .

More news to come .

Mimi ndio maana siwaamini tena hawa Chama Cha Majambazi/Mafisadi wameweka mbele maslahi ya chama chao zaidi kuliko ya nchi na wanaweza kufanya chochote kile ili kuendelea kubaki madarakani. CCM kama tulivyoifahamu mwaka 1985 si hii ya leo iliyojaa mafisadi, mafioso na majambazi wanaojali maslahi yao binafsi.
 
jamani tumechukua hadithi za upande mmoja na kuziamini moja kwa moja na kuanza kukandamiza kisawa sawa.

mtindo huu ndio unaopelekea watu kuliona jamvi letu ni la kishabiki sana,ni busara kuangalia pande zote za shilingi.

wakuu kuna watu wao zikiletwa habari za upande fulani hawafikiri mara mbili huziamini na kuanza kushusha pumba.

hivi demokrasia maana yake upinzani uwe na uhuru ya kufanya walitakalo hata wakivunja sheria ya nchi?

demokrasia ili itendeke lazima wapinzani washinde?

rafu kwa upinzani ok ila kwa chama tawala no.

upinzani walitudanganya kuwa mgombea wao kapewa sumu, uongo wa mchana kweupee hakuna alie na sauti ya kukemea wakati iko wazi, bali haya kusikia tumeyavalia njuga.

taireni wakuu.
 
Ni kweli ndio maana sisi wengine tunaenda kwa wenye habari wenyewe na siyo watu wa pembeni. NImezungumza na Kimesera na nimezungumza na OCD na wote wamethibitisha kutokea kwa matukio hayo.
 
Kiteto ni tik tik tik.....

Someone have to think real fast hapo manake walisema:
"You can fool some people sometimes, you cant fool all the people all the times"

Olpayan Kimesera, una support ya watu wote nyuma yako, kaza buti manake hata wakileta mamluki kura tutazihesabu hata mara mia... Tunajua historia, tunajua yaliyotokea na tunaagalia kwa ukaribu yanayo na yatakayotokea Kiteto... Tonyua Papalai
 
yeroo morani 75..taphala doii!! kaanyooo!
 
Ni kweli ndio maana sisi wengine tunaenda kwa wenye habari wenyewe na siyo watu wa pembeni. NImezungumza na Kimesera na nimezungumza na OCD na wote wamethibitisha kutokea kwa matukio hayo.

jee umeuliza sababu za ugomvi huo? tokeo sawa limetokea lkn sababu ni nn?

hebu tupatie chanzo cha hayo kutokea
 
Mzee Philemon, kwa kweli inatia hasira sana hii mambo eti..... Yaani mwaka huu tunajua wapi ni wapi na hivi nguvu yao ya kule mangaribi imechukuliwa na umeme itabidi sijui waende wapi.........
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom