Uchaguzi wa Kiteto: Taarifa mbalimbali

Uchaguzi wa Kiteto: Taarifa mbalimbali

Status
Not open for further replies.
Inatia hudhuni sana, Tanzania ya leo haina haki kabisa. Hawa wananchi wana haki ya kuchagua wampendao na sio CCM impendae. I feel deep sad for my country.
 
Kinacho nisikitisha ni viongozi wetu kutokusoma alama za nyakati kwani yanayotokea kenya pia yanawezatokea hapa kwetu kinachopelekea watu kuwa wakali na hali ngumu ya maisha na kila mtu anafahamu hali ngumu inayotukabili watanzania.

Hivi karibuni mambo mengi yametokea ikiwa ni pamoja na viongozi kuzomewa,vituo ya polisi kuvamiwa na wananchi wenye hasira na viongozi kuulizwa maswali magumu hata na watoto wadogo,Jamani inatosha viongozi wetu badilikeni mtaanza kunyang`anywa mali zenu kwa nguvu na wanachi wakionewa kupita kiasi, nchi hii si masikini kama watu wanavyozani kama rasilimali zikitumika vizuri tutasonga mbele haraka sana.
 
Kama hali ni kama hiyo huko Kiteto,Serikali ya CCM inapaswa kufunga domo lake kuhusu yaliyotokea na yanayoendelea huko Kenya kwani hayana tofauti na Kiteto.
Huwezi kumwambia mwenzio uko uchi wakati wewe mwenyewe hujavaa hata chupi. Ninamashaka sana kama CCM wanatumia nguvu hizi kwa kiti kimoja cha ubunge, jee itakuwaje 2010 wakati Watanzania watakapoamua kuiondoa serikali nzima madarakani?
Nadhani hali inaweza kuwa mbaya zaidi ya tunayoiona Kenya.
Kwangu mie naona hawa askari wetu wanaotumwa na wakubwa wao kuwashambulia NDUGU zao ili kulinda maslahi ya mafisadi ndio WAJINGA WA KUTUPWA. Wao wenyewe hali zao ni duni sana kwa sababu ya ufisadi huohuo lakini hawalioni hilo.
Dawa ni kuendeleza harakati hizi kwa nguvu zaidi mpaka kieleweke.
 
Hii ni ya Mhe Karume kule Ujerumani, boya hapa

http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2008/02/18/108605.html

Duh, si mchezo kumbe kwenye siasa kuna bahati mbaya, si utani kuna kaazi kubwa kweli kweli hata hapa kwetu Kiteto....

Ee Molla wetu, ibariki Tanzania na utuepushe na mzuka wa fujo, lakini utusaidie kuutokomeza ufisadi na kuushinda daima!!! Uwasaidie viongozi wetu kuona dalili na mabadiliko ya majira, pia kuwapa nguvu ya kujua mazuri kutoka mabaya!!
 
jamani tumechukua hadithi za upande mmoja na kuziamini moja kwa moja na kuanza kukandamiza kisawa sawa.

mtindo huu ndio unaopelekea watu kuliona jamvi letu ni la kishabiki sana,ni busara kuangalia pande zote za shilingi.

wakuu kuna watu wao zikiletwa habari za upande fulani hawafikiri mara mbili huziamini na kuanza kushusha pumba.

hivi demokrasia maana yake upinzani uwe na uhuru ya kufanya walitakalo hata wakivunja sheria ya nchi?

demokrasia ili itendeke lazima wapinzani washinde?

rafu kwa upinzani ok ila kwa chama tawala no.

upinzani walitudanganya kuwa mgombea wao kapewa sumu, uongo wa mchana kweupee hakuna alie na sauti ya kukemea wakati iko wazi, bali haya kusikia tumeyavalia njuga.

taireni wakuu.
Mtu wa Pwani,

Binafsi sina ushabiki upande wowote na kwakuwa Zitto alikuwa na namba yangu kama mwanachama wa JF basi akaniuliza kama niko mtandaoni na naweza kuwafahamisha kinachojiri. Nikafanya kuwafahamisha kadiri alivyokuwa anani-update.

Kwa sasa nimepata ujumbe toka kwake ambapo anawashukuru wana JF kwa ushirikiano. Ujumbe unasema hivi:

"Tupo kituo cha polisi Kiteto, RPC amesafiri toka Babati kuja kufuatilia suala hili. Wamekamatwa makomandoo wawili ambao wamekiri ni toka CCM na wametokea Dar trained JKT Militias. Majina yao ni Hamis Kilindo na Keneth Mbilinyi. Keneth anayejiita mlinzi wa Pius Msekwa alikabidhiwa machine gun na mkuu wa kituo". Mwisho wa kumnukuu.

Mjumbe hauwawi sio?
 
Tunahitaji taarifa za kina na zilizothibitishwa. Hawa polisi kama hawasomi alama za nykati wasubiri kivumbi. Patakucha hapa
 
Tunahitaji taarifa za kina na zilizothibitishwa. Hawa polisi kama hawasomi alama za nykati wasubiri kivumbi. Patakucha hapa
Ningekuwa mwandishi wa habari ningempigia OCD wa Kiteto na kuwarushia maongezi yangu na yeye. Namba yake ninayo lakini mimi si mwandishi wa habari. Anapatikana kupitia namba +255-784-368-759
 
... OCD .... Anapatikana kupitia namba +255-784-368-759
Nimeipata namba ya RPC anayeshughulikia suala hili sasa hivi. Ni +255-773-606-560 au +255-713-606-560. Kwa Mwanakijiji nadhani nimekurahishia mkubwa. Try out
 
Pamoja na kuchelewa kwa taarifa, nadhani waaandishi wetu "walizidiwa na Bush" lakini naamini kuanzia kesho mambo yataku hadharani.
 
Pia tukio lenyewe limetokea jana usiku, wakati ambapo magazeti mengi yalikuwa mitamboni tayari. Tukio kama hilo linahitaji upate uthibitisho wa taarifa kutoka sehemu zote zinazohusika, polisi, hospitali na kwa viongozi wa vyama vinavyohusika ili kutoa taarifa ambayo haiko biased ili kuepuka uandishi wa kukurupuka.
 
jee umeuliza sababu za ugomvi huo? tokeo sawa limetokea lkn sababu ni nn?

hebu tupatie chanzo cha hayo kutokea

Mtu wa Pwani wakati MKJJ anafanya mahojiano kila mmoja alikuwa anamsikia .Polisi walikataa kusema lolote mbali na kusema vitendo vipo hivyo na akashangaa kama mkuu wa kituo anaweza kuwapiga raia.Kimesela pia sote tumemsikia na akasema walikuwa ndani ya ofisi ya Chama chao wanafanay mazoezi ya nyimbo za kuhamasisha wakavamiwa .


Leo kw amujibu wa OCD yule wanatagemea kusema zaidi maana jana hakumpa mwanakijiji majibu zaidi .Ila tuna ambiwa baada ya simu ya MKJJ walianza kutoa ushirikiano .
 
barakadau67diwv5.jpg






Huyo ni kiongozi wa Chadema Bw. Baraka Daudi baada ya kupewa mkong'oto kwenye Kituo cha Polisi huko Kiteto.


viongo987ziwengineer9.jpg





Hawa ni viongozi wengine wa Chadema wakiwa kituo cha Polisi baada ya kupigwa wakiwa mikononi mwa Polisi.

Ni nani anayeleta mambo kama ya Kenya? Najaribu kumtafuta RPC na OCD wake, this is unacceptable!!!
 
uuuuuuwwwwwwwwwwwwwwwwwwwwwiiiiiiiiiiii,

Jamani jamani jamani jamani,

yaani yamekuwa haya tena?!?!!?
 
Binafsi nashangaa hata chombo kimoja cha habari kilicho andika habari hizi hakuna!! Jamani wandishi wa habari, hapa hakuna?

Wataandika hizi wakati kila mtu anajaribu kuwa karibu na Kichaka na ujumbe wake. Si unajua tena mambo ya kujikomba kwa wageni huku ukiacha wenyeji wakila makombo na kufa kwa njaa!
 
Najua watu wa vyombo vya habari nyumbani bado havijamaliza kuchapa magazeti ya kesho.. tafadhali kombeni hizo picha zitoke Kesho kuonesha jinsi gani serikali yetu inajali haki za binadamu na utawala wa sheria!
 
Mambo ya Kenya haya!! sasa Kofi Annan atajigawaje iwapo Kiteto itakuwa Nairobi ama Naivasha?

Joji Kichaka yuko bongo na kama kweli ana nia ya kuendeleza demokrasia bongo na sio kujenga kambi ya kijeshi kama wengi hapa tunavyojua basi itabidi hapa ndio aonyeshe nia yake....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom