Interested Observer
JF-Expert Member
- Mar 27, 2006
- 3,384
- 4,428
Mtu wa Pwani,
Binafsi sina ushabiki upande wowote na kwakuwa Zitto alikuwa na namba yangu kama mwanachama wa JF basi akaniuliza kama niko mtandaoni na naweza kuwafahamisha kinachojiri. Nikafanya kuwafahamisha kadiri alivyokuwa anani-update.
Kwa sasa nimepata ujumbe toka kwake ambapo anawashukuru wana JF kwa ushirikiano. Ujumbe unasema hivi:
"Tupo kituo cha polisi Kiteto, RPC amesafiri toka Babati kuja kufuatilia suala hili. Wamekamatwa makomandoo wawili ambao wamekiri ni toka CCM na wametokea Dar trained JKT Militias. Majina yao ni Hamis Kilindo na Keneth Mbilinyi. Keneth anayejiita mlinzi wa Pius Msekwa alikabidhiwa machine gun na mkuu wa kituo". Mwisho wa kumnukuu.
Mjumbe hauwawi sio?
UnbelievablE!!!!