Nyongeza tu: Danda Juju Martin ni Afisa Mwandamizi(Idara ya Sera na Utafiti) katika Kurugenzi ya Bunge na Halmashauri.
JJ
Viongozi sita Chadema wajeruhiwa vurugu za uchaguzi
Na Mussa Juma,Kiteto
VIONGOZI sita waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutoka makao makuu ya chama hicho, wamejeruhiwa vibaya mmoja akiwa mahututi baada ya kupigwa na kuchomwa visu na kundi la vijana wanaodhaniwa kuwa ni wa CCM na Polisi katika vurugu za uchaguzi Jimbo la Kiteto ambalo lipo wazi baada ya aliyekuwa mbunge wake, Benedict Lusulutya (CCM) kufariki dunia hivi karibuni.
Licha ya kupigwa viongozi hao pia walimwagiwa kemikali machoni ambayo bado haijafahamika na kusababisha kutoona kwa zaidi ya nusu saa na mmoja wao hadi jana macho yalikuwa yake hayaoni.
Vurugu hizo zilitokea katika kata ya Kijungu wilayani hapa juzi majira ya saa 12 jioni , baada ya kundi la vijana hao maarufu kama Green Guard kutoka jijini Dar es Salaam, kuvamia viongozi hao wa Chadema wakiwa katika ofisi yao ya kata ya Kijungu kwa tuhuma za kuwapigia kelele wakiwa katika eneo lao la mkutano.
Waliopigwa ambao hadi jana asubuhi hali zao zilikuwa mbaya na wengine kulazwa katika hospitali ya wilaya hiyo ni Hamadi Mussa Yusuph Naibu katibu mkuu wa Chadema Zanzibar, Juju Danda, Afisa mwandamizi kurugenzi ya bunge na halmashauri kuu Taifa.
Wengine ni Joseph Freme(43) Mwenyekiti wa Ruvuma Chadema na mjumbe wa kamati kuu,Msafiri Mtemelwa, Kaimu Mkurugenzi wa kampeni na Uchaguzi,Selemani Mohamed mjumbe wa uchaguzi Kiteto.
Katika sakata hilo, dereva wa gari la makao makuu Daudi Baraka ndiye alijeruhiwa vibaya kwa kuchomwa visu na kupigwa vibaya ambaye hadi jana hali yake ilikuwa mahututi akiwa anaongezewa maji na kushonwa nyuzi kadhaa.
Freme alisema licha ya kupigwa viongozi hao, pia walikamatwa na kupigwa na polisi wa kituo kidogo cha Kijungu ambao awali walikuwa pamoja na viongozi wa CCM, Katibu Mkuu Yusuph Makamba na Makamu Mwenyekiti Pius Mswkwa.
"Sisi hatukupigwa sana na green guard pale ofisini lakini tulipofikishwa kituo kidogo cha polisi kijungu ndipo tulipigwa sana japo kuwa tayari mwenzetu alikuwa amechomwa kisu ubavuni," alisema Freme ambaye alikuwa hajaweza kutembea hadi jana.
Hata hivyo alisema mara baada ya kuona wakipigwa ovyo, alipiga simu kwa IGP na baadaye aliambiwa awasiliane na mkuu wa polisi mkoa wa Manyara ambaye baadaye ndiye alituma polisi kuja katika kituo hicho kutoka makao makuu ya wilaya hiyo umbali wa takriban kilometa 70.
Viongozi hao, waliashiwa na polisi majira ya saa tano usiku baada ya juhudi kubwa zilizofanywa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa,Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe na Mbunge wa viti maalum Grace Kiwelu.
Viongozi hao mara baada ya kuandikisha maelezo yao kwa� mkuu wa polisi wa wilaya ya Kiteto,Archi Killo waliachiwa kwa dhamana na kupewa hati ya matibabu PF 3 na walitakiwa jana asubuhi kuripoti polisi.
Akizungumzia mgogoro huo, Msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Kijungu, Ibrahim Mdugo alisema vurugu hizo zilianza majira ya saa 12 jioni baada ya kundi la vijana hao wa CCM kuanza kulalamikia kelele kutoka kwa viongozi hao wa Chadema waliokuwa wakisimamia kwaya yao iliyokuwa inafanya mazoezi.
Mdugo alisema awali viongozi hao wa Chadema walikuwa na gari lao wakitangaza watu kujitokeza kupiga kura Februari 24 bila ya woga wakitumia vipaza sauti ambavyo CCM waliokuwa katika mkutano ulikuwa unahutubiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa,Pius Msekwa walikuwa wanalalamikia.