Wana JF
Lazima tukumbuke kuwa katiba yetu ni ile tuliyopewa na mkoloni, na kikatiba/kisheria polisi wanapewa haki na kulindwa kisheria kutokana na vitendo vyao vya kupiga watu. Polisi wetu wana uwezo mkubwa wa kutumia nguvu kuliko kutumia akili, kama ilivyokuwa polisi wa kikoloni, kwa hiyo hapa tukiwalaumu sana polisi, ambao wanatumwa tunaweza kuwa tunawaonea. Tunaweza kuwalaumu kwa kutotumia busara zao kuangalia lipi wanatakiwa kufanya wanapotumwa kufanya kazi zao.
Kupiga ni unyama na ni ushenzi, lakini lazima tuwe tunaelekeza mapambano kwa wanaowatuma polisi hao.
Nakumbuka kuna kipindi mkuu mmoja wa polisi alikuwa anatuma polisi kufanya kazi kwenye maeneo kama hayo kwaa masharti kuwa, hakuna kuua wala kuumiza mtanzania, bila sababu ya msingi. Kama waandishi wa habari wakipata nafasi ni vizuri kuwauliza wakuu wa polisi ni kwanini wamefanya hivyo. Na tupiganie utaratibu wa watanzania kuwa na ulinzi kutokana na unyama na ukandamizaji kutoka kwa vyombo vyetu vya dola!