Uchaguzi wa Kiteto: Taarifa mbalimbali

Uchaguzi wa Kiteto: Taarifa mbalimbali

Status
Not open for further replies.
Kiteto Kiteto Kiteto... itabidi tuanze kutengeneza ukumbi wa "Vijembe". Si unajua watu hawapigani shuleni hadi baada ya kengele?
 
Na: Kitila Mkumbo


KUNA imani kwamba Watanzania ni wepesi wa kusahau mambo makubwa ya kitaifa. Kuna imani pia kwamba Watanzania ni wepesi wa kukubali yaishe pale wanapoona jambo fulani walilokuwa wanalidai limekataliwa na serikali, hata kama wanajua kuwa msimamo wa serikali si sahihi.
Hata hivyo, inaonekana tumeanza kubadilika, tena kwa kasi ambayo hata watawala itabidi waanze kujiuliza kunani.

Dalili za Watanzania kubadilika zinaonyeshwa na jinsi ambavyo tumeweza kulibebea bango tatizo la ubadhirifu katika Benki Kuu. Ubadhirifu wa kutisha katika Benki Kuu umeendelea na inaonekana utaendelea kubaki katika akili na midomo ya Watanzania kwa muda mrefu ujao.

Tutakumbuka kwamba sakata la ubadhirifu liliwekwa hadharani na wabunge wa upinzani kwa mara ya kwanza katika bunge la bajeti la mwaka jana. Kwa hiyo, ni takribani zaidi ya nusu mwaka sasa bado tunaendelea kulijadili.

Hii ni tofauti na matukio mengine mengi ya kitaifa yaliyowahi kutokea, yakiwemo yale ya mikataba ya aibu inayohusu kampuni za kusambaza umeme za IPTL na Richmond pamoja na ile ya madini. Vilevile sakata la Benki Kuu limeweka historia mpya katika nchi yetu kwani ni kwa mara ya kwanza wananchi waliweza kukubaliana na maelezo ya upinzani na kukataa yale yaliyotolewa na Serikali ya CCM ya kujaribu kuukana au kuutetea ubadharifu huo.

Pamoja na hatua nzuri ya kutokusahau mapema mambo mazito ya kitaifa inayoanza kujitokeza miongoni mwa Watanzania, inaonekana bado tuna tatizo la kutambua chanzo halisi cha matatizo ya ubadhirifu katika nchi yetu. Inaonekana wengi wetu tunaendelea kuamini kwamba matatizo ya ubadhirifu katika serikali yetu yanasababishwa na watu wachache waliopo katika mamlaka na hayatokani na mfumo. Kwa hiyo inaonekana tunaelekea kuamini kwamba tunaweza kumaliza tatizo la ubadhirifu kwa kuwatoa katika serikali wabadhirifu ambao pengine ni wachache tu.

Mimi siamini kwamba tatizo la ubadhirifu katika nchi yetu ni la watu wachache wanaotumia madaraka yao vibaya. Ninaamini kabisa kwamba hili ni tatizo la kimfumo ambalo halikutokea kwa bahati mbaya bali limetengenezwa mahsusi kama njia ya kulinda huo mfumo uendelee kubaki hapo ulipo.

Ninachojaribu kueleza hapa ni kwamba, tatizo la samaki wenye sumu kwenye bwawa haliwezi kwisha kwa kumtoa samaki mmoja mmoja. Samaki hawawezi kuwemo kwenye bwawa pasipo kuwemo maji. Kwa hiyo sasa dawa ya kuwatoa samaki wenye sumu kwenye bwawa si kuwavizia samaki wanaojitokeza nje na kuwaua bali ni kukausha maji yote kwenye bwawa na kuanza upya. Maji yakishakauka bwawani samaki wote watakufa na hivyo utapata nafasi ya kuweka maji mengine na kupandikiza samaki wapya.

Kosa ambalo tunaelekea kulifanya katika mapambano ya ufisadi ni kuwavizia mawakala wa ufisadi na kujaribu kuwatoa hawa tukifikiri huko ndiko kupambana na ufisadi. Kwa hiyo kuna watu wanaamini kwamba kama Dk. Daudi Ballali akifikishwa mahakamani, basi tutapata jibu la wale waliotuibia pesa pale Benki Kuu.

Kuna watu wengine wameenda mbali hata kutaka Dk. Ballali apewe kinga ili awataje wenzake walioshiriki katika kutafuna hayo mapesa. Na kuna wengine wanasema kuwa Dk. Ballali alitumiwa tu na anajiandaa kuwaanika walaji hasa wa yale mapesa. Bila shaka ni kweli kabisa kwamba hata kama kweli Dk. Ballali alishiriki katika ubadhirifu wa mabilioni ya shilingi pale Benki Kuu isingewezekana akawa ameiba pesa zote zile peke yake.

Inabidi tujikumbushe pia hapa kwamba Dk. Ballali hakutoroka nchini. aliondoka kihalali, tena kwa kuaga. Kitu ambacho hatuna uhakika nacho ni sababu zilizomuondosha nchini, hasa baada ya ugonjwa na mahala anapotibiwa kufichwa na watawala kwa sababu wanazozijua wao.

Kwa hakika kuna kila sababu ya kuamini kwamba serikali imemficha Dk. Ballali, na kwa kumficha huko kuna makubwa zaidi wanayoyaficha. Bahati mbaya waliyo nayo wenzetu serikalini ni kwamba hawana uwezo wa kuficha ukweli kwa muda wote katika ulimwengu wa leo. Wakati utafika ukweli wote utakuwa wazi na itabidi wabuni uongo mwingine.

Kwa hiyo, ninachokataa mimi ni hii imani inayoanza kujengeka kwamba kuwajua walioshirikiana na Dk. Ballali katika wizi huu kutasaidia kutatua tatizo la ubadhirifu katika nchi yetu. Nakataa hili kwa sababu mbili. Ya kwanza ambayo nimeshaileza ni hiyo kwamba tatizo la ubadhirifu katika nchi yetu halisababishwi na watu wabaya au wabadhirifu katika serikali, bali mfumo wa ubadhirifu ambao ni sehemu muhimu ya utawala katika Serikali ya CCM.

Sababu ya pili ni ukweli kwamba hakuna jina hata moja atakalolitaja Dk. Ballali ambalo hatujalisikia mpaka sasa. Majina ya watu wote walioshiriki katika ubadhirifu wa Benki Kuu tayari yanajulikana sana kote nchini, mijini na vijijini na hata nje ya nchi. Kwa hiyo kama tungekuwa na mfumo ambao si wa kibadhirifu, tayari ungeshawachukulia hatua watuhumiwa wa ubadhirifu huo.

Kwa hiyo, utaona kwamba tunachotaka kukifanya hapa ni kujaribu kuwavizia samaki wenye sumu wanaojitokeza ili tuwatoe katika maji badala ya kutoa maji yenyewe. Mtazamo wangu hapa ni kwamba, bwawa letu (Tanzania) tumeliwekea maji (CCM) yenye sumu ambayo yanasababisha samaki wote (viongozi wa serikali) waliomo humo wapate sumu. Kwa hiyo dawa yake hapa ni kuyatoa haya maji (CCM) katika bwawa letu na kuweka maji mengine (chama kingine) ili tutakapopandikiza samaki wengine wasipate hiyo sumu.

Kimsingi Chama Cha Mapinduzi kimekuwa kikitumia ubadhirifu kama mradi wa kutengeneza fedha za kukiwezesha kubaki madarakani. Tutakumbuka, kwa mfano, baada kuchaguliwa kwa kipindi cha pili serikali ya Rais Mkapa ilibuni mradi wa kununua ndege ya rais kwa bei kubwa huku baadhi ya wananchi wakikabiliwa na njaa. Tukalalamika sana, lakini tukakemewe na serikali ya Mkapa kupitia kwa Waziri Mramba kwa sentensi moja rahisi, lakini iliyojaa kiburi na dharau; kwamba ndege ya rais lazima inunuliwe hata kama hao wenye njaa itabidi wale nyasi.

Tukumbuke kwamba Rais Mkapa alikuwa ananunua ndege hii karibu kabisa na mwisho wa utawala wake. Kwa hiyo kama ingekuwa ni shida ya ndege kweli angekuwa hana ulazima wa kuharakisha na kuhakikisha kwamba inanunuliwa katika kipindi cha urais wake angeweza kuanzisha mchakato tu ambao rais anayemfuata angeweza kuukamilisha.

Kwa hiyo si vigumu kutambua kwamba huu ulikuwa ni mradi wa kujitengenezea hela kwa kisingizio cha kununua ndege ya rais. Hili lilikuja kuthibitishwa na wauzaji wenyewe kupitia Bunge la Uingereza kwamba bei tuliyonunulia ile ndege ilikuwa si halali bali tulijibambikizia. Sasa kama kweli mfumo wetu wa utawala si sehemu ya ubadhirifu huu iweje hadi leo hata baada ya kujua ukweli wote huu umeshindwa kuwachukulia hatua wale walioshiriki kuibambikia nchi yetu bei ya juu hiyo ndege ya rais?

Kuna watu pia wanaotaka tuamini kwamba Rais Kikwete na serikali yake wapo tofauti na hao waliopita. Mimi nitaendelea kuwauliza swali, kama kweli Rais Kikwete yupo tofauti, ilikuwaje amuweke katika baraza lake la mawaziri mtu ambaye aliwatukana Watanzania wenye njaa kwa kiwango cha kuwaambia wale nyasi, na ambaye alishiriki katika kutubambikia bei ya juu ya hiyo inayoitwa ndege ya rais?

Katika ulimwengu wa leo, ni Tanzania pekee ambako waziri wa serikali ya wananchi anaweza akadiriki kuwakejeli na kuwadharau wananchi waliomchagua kwa kiwango hiki na akaendelea kubaki madarakani. Kwingineko duniani kejeli kama hizi zilisikika mara ya mwisho kutoka kwa miongoni mwa mawaziri wa aliyekuwa Rais wa Zaire, Mobutu Sese Seko. Hata hivyo pamoja na udikteta na ujeuri wake, naye ilifika mahala akawafukuza mawaziri wa namna hii!

Kuna jambo lingine linalothibitisha kwamba ubadhirifu ni sehemu muhimu ya utawala wa CCM, na kwamba viongozi wetu wanatumia matatizo yanayoikabili nchi kubuni miradi ya kuchota pesa za walipa kodi kwa matumizi haramu. Hili ni pamoja na kutumia matatizo ya umeme katika kujitengenezea miradi ya kuchota fedha kutoka hazina kwa matumizi haramu. Sote tunakumbuka jinsi ambavyo serikali ya Rais Mkapa ilibuni miradi haramu ya IPTL na Net Group Solution.

Rais Mkapa akipingana na upembuzi wote wa kitaalamu, alizitetea kampuni hizi za kitapeli hadi akahakikisha zinapata nafasi katika kuiendesha TANESCO. Lakini sote tunajua jinsi ambavyo mashirika haya yalivyotumika kufyonza hazina yetu na watumiaji wa umeme kwa ujumla.

Kama vile ya IPTL na Netgroup hayakutosha, naye Rais Kikwete alipochaguliwa tu aliibuka na mradi mpya wa Richmond kama njia ya kutatua matatizo ya umeme yaliyokuwa yanaikabili nchi mwanzoni mwa utawala wake. Richmond wakalipwa mamilioni ya shilingi, lakini tukaendelea kukaa kwenye giza hadi pale mwenyezi Mungu alipotupatia mvua ya kuzalisha umeme. Richmond walilipwa na umeme hawakuleta! Sasa ni wapi kwingineko hapa duniani umewahi kusikia haya yakitendeka zaidi ya Tanzania?

Mlolongo wa matukio yote haya ya kibadhirifu ni uthibitisho kwamba huu ufisadi unaoendelea si wa bahati mbaya au kwamba unafanywa na watu wachache tu, bali ni mfumo na mtandao uliojengwa na kujijenga kwa makusudi na malengo maalumu. Narudia tena kwamba tatizo la ubadhirifu katika nchi yetu limetengenezwa na mfumo wa utawala uliopo kama njia ya kuiwezesha CCM kukabiliana na siasa za ushindani katika mfumo wa vyama vingi kwa upande mmoja, na kwa upande mwingine, kukineemesha kikundi cha watu wachache ndani ya utawala wa serikali ya CCM.

Hakuna shaka yeyote kwamba Watanzania tumeonyesha kukerwa na ubadhirifu unaoendelea katika serikali ya CCM. Lakini wasiwasi wangu ni kwamba tunayaelekeza mashambulizi yetu kusiko. Tunapoitaka serikali ya CCM iwachukulie hatua akina Dk. Ballali ni sawa na kumwambia mwizi ajikamate mwenyewe jambo ambalo haliwezekani. Ndiyo kusema madamu serikali ya CCM inaendelea kubaki madarakani, ufisadi hauwezi kwisha bali utashamiri kwa kubadili maumbo: IPTL, Richmond, Benki Kuu, na kadhalika.

Kuna haja basi ya kubadili mbinu za mapambano yetu dhidi ya ufisadi kwa kuelekeza mashambulizi dhidi ya mfumo unaozalisha mafisadi badala ya kulenga fisadi mmoja mmoja. Katika mapambano haya inabidi tujue kwa dhati kabisa mambo matatu. Mosi, lazima tumjue adui yetu, pili, tujue silaha yetu, na tatu, tujue fursa za kumshinda huyu adui.

Ni wazi kabisa sasa kuwa adui yetu hapa ni mfumo unaolea ufisadi, ambao umejengwa na CCM. Silaha tuliyonayo katika mapambano haya ni kura zetu, na fursa pekee tuliyonayo ni chaguzi zinazojitokeza sasa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Tuzitumie chaguzi zinazojitokeza sasa kama fursa ya kuimarisha mapambano yetu dhidi ya ufisadi wakati tukijiandaa kufanya mabadiliko makubwa ya kisiasa ifikapo uchaguzi wa mwaka 2010.

Tuna bahati mbili kubwa ambazo Mungu ametupa katika vita yetu dhidi ya ufisadi na uporaji wa rasilimali za nchi yetu. Kwanza, tunao majemedari ambao Mungu amewapa ujasiri wa ajabu wa kusimama kidete dhidi ya nguvu kubwa za ufisadi. Hawa ni wabunge wa upinzani. Pamoja na uchache wao, wametuonyesha kwamba majimbo yao ni wananchi na nchi wakati wenzao wa CCM, kwa matendo yao bungeni ya kutetea na kuhalalisha ufisadi, wamejionyesha wazi kabisa kuwa majimbo yao ni chama chao.

Bahati ya pili ambayo pia Mungu ametupa ni ukweli kwamba, katika wiki chache zijazo kutafanyika uchaguzi mdogo katika Jimbo la Kiteto. Hii ni fursa muhimu waliyoipata wenzetu wa Kiteto ya kutuanzishia safari yetu ya mabadiliko katika uongozi wa kisiasa ambayo, kama tulivyokwishaona hapa, ndio njia ya uhakika na endelevu ya kuvunja nguvu za mtandao wa ufisadi nchini.

Kwa hiyo, nitumie fursa hii niwaombe wana-Kiteto watuanzishie safari yetu ya mabadiliko kwa kutuchagulia mbunge kutoka kambi ya upinzani katika jimbo hili. Kusema kweli wana-Kiteto wana hiari ya kuchagua kati ya kuimarisha mapambano dhidi ya ufisadi kwa kumchagua mbunge wa upinzani au kudhoofisha nguvu ya upinzani bungeni na hivyo kufifisha mapambano dhidi ya ufisadi kwa kumchagua tena mbunge wa CCM. Ni matumaini yangu kuwa wana-Kiteto hawatawaangusha Watanzania wenzao kwa kuhakikisha kuwa wanamchagua mbunge wa upinzani ili kuimarisha jeshi la kupambana na ufisadi katika Bunge letu la Jamhuri ya Muungano. Sote tunawaombea Mungu awape ujasiri na hekima ili siku ya uchaguzi watuongezee askari katika jeshi la kupambana na ufisadi kupitia bunge letu.

Kwa maoni na mchango niandikie: kitilam@yahoo.com
au nitumie ujumbe: +44 7904 237 414.

http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/1/30/makala1.php
 
Kiteto Kiteto Kiteto... itabidi tuanze kutengeneza ukumbi wa "Vijembe". Si unajua watu hawapigani shuleni hadi baada ya kengele?


Mkuu mwenzangu, maneno ya Kiteto hayo, wewe tafuta popcorn subiri cinema ya bure hapa, kwi! kwi! kwi! Kumkoma nyani giladi tunaanzia JF mpaka tunaingia Kiteto huko! Maana watu wazima wakililia wembe hupewa.....! Siasa kuna waliozaliwa nazo na kuna kujifunzia ukubwani!
 

Na pia kuna mwingine walimpa break wiki iliyopita hapa, wanajua kwamba amebadili jina tayari, amekuwa akiropoka sumu hapa kwa muda mrefu na mara ya mwisho ilikuwa last two weeeks, lakini sasa wanamsubiri ili wamfunue hapa kwanza, halafu wamfahamishe mkewe tabia zake za ku-cheat na mwanamama mmoja pale wa ubalozi wa Botswana, maana mkewe anafahamika kwa kumtwanga vibao kila wakati,

[/U]

Hii kali, duh, hawa watu wa namna hii natamani kweli kuwajua, basi tu.
 
Mimi niko radhi kabisa ES umwage nyeti zote hapa kama kweli ni Mimi Lunyungu maana siwezi kusema mafisadi na mimi nakuwa Fisadi at the other hand . Nina kuruhusu sema uyajuayo na hizo connections zako wa mke wa Balozi wote you have said ili kukata mzizi majungu hapana .Naomba taja kabisa ili tuwekane sawa kuanzia hapa tuendelee na mada badala ya mada kugeuzwa uongo kuua maana ya mada .Mbinu za ki CCM hizi . Weka ukweli wote hapa nina kuruhusu .
 
Jamani wandugu ,habarini za leo kilichojiri hapa kwetu kijiweni yaani Kiteto ni kuwa mgombea wa upinzani kawekewa pingamizi na mgombea wa CCM.

sababu ya pingamizi ni kuwa eti Kimesera aliwahi kufungwa siku moja mwaka 1996 kwa kosa la trafick baada ya kuvuka taa nyekundu pale ubungo na alikaa ndani kwa muda wa siku moja tuu na kesho yake hukumu ikafutwa na hata yeye alikuwa tayari amesahau juu ya jambo hilo.

Kumbukeni kuwa alikuwa mgombea 2000 na 2005 ila hilo pingamizi halikuwahi kuwekwa ila ndio limewekwa leo ila kwa vile ushirikiano wa vyama walikuwa na vyanzo vya habari kutoka ndani ya CCM walikuwa wameshapata habari hizo na ndio maana waskatuma timu ya wanasheria kwenda huko ili kuweka mambo sawa na timu hiyo inaongozwa na wakili na mbunge Halima mdee.

Nitaendelea kuwahabarisha ilka jueni tuu kwamba pingamizi lao ni base less kwani sheria ya uchaguzi iko wazi juu ya mamabo kama hayo .
 
Hapana nataka ES aseme shutuma zake kwa uwazi kabla hatuja endelea na mambo ya Kiteto. Es please nakupa ruhusa sema kwa uwazi .
 
kwa taarifa tuu ni kuwa vyama vilivyorudisha fomu ni vitatu, CHADEMA (ushirikianO),CCM na PPT Maendeleo.

Kwa hivyo mpsambano huo ndivyo utakavyokuwa hapa kwenye uwanja wa mampambano.

Pingamizi bado wanasheria wapo ndani wakilitatua jambo hilo,ila cha ajabu ni kuwa hao CCM hawana hata mwanasheria wa kuwawakilisha ila mgombea anajiwakilisha kwenye pingamizi mwenyewe.
 
Mkuu Mtanzania,

Usiwe na hofu mkuu, unajua habari za kuokota vijiweni bila ya kuwa na ukweli, ni vyema kuuliza ukaelezwa ukweli kuliko kujifanya kujua wakati hujui, maana sasa watu wanatafuta za kweli na kuzimwaga kama zilivyo kwa wanaohusika hapa JF,

Na pia kuna mwingine walimpa break wiki iliyopita hapa, wanajua kwamba amebadili jina tayari, amekuwa akiropoka sumu hapa kwa muda mrefu na mara ya mwisho ilikuwa last two weeeks, lakini sasa wanamsubiri ili wamfunue hapa kwanza, halafu wamfahamishe mkewe tabia zake za ku-cheat na mwanamama mmoja pale wa ubalozi wa Botswana, maana mkewe anafahamika kwa kumtwanga vibao kila wakati,

Kwa hiyo mkuu wala usiwe na hofu na habari za vijiweni mkuu maana kwenye siasa watu wamesikia mengi sana, isipokuwa huwa wanachagua ya kujibu, tena on the right time, mengine huwa wanaachia tu, ila sasa kazi maana watu wazima hawatishiani nyau hufanya kweli!

Mkuu Mtanzania, everything is under control na kumkoma nyani mbele tena mpaka giladi!

FMES,

Mmmhhhh!!!! mkuu wacha ninyamaze maana huenda waarabu wa Pemba hujuana kwa viremba.

JF kwa data, mtu unaweza kudhani umejificha kumbe kuna Wambeya wanachungulia.

Haya tuendelee na Kiteto (Kuteta) na tutasikia mengi mwaka huu. Huenda hii ni maandalizi ya mwaka 2010.
 
FMES
bado nasema nakutaka kwa uhakika na uwazi useme lolote in connection na mimi Lunyungu.This is not nickname like yours but is my real name . Sasa make no mistake .Nasema mimi Lunyungu nakuruhusu sema uyajuayo then tuendelee. Thibitisha madai yako hapa hapa na si sirini .Utakuwa umejenga heshima kwamba kweli usemayo unayajua na si uzushi ama mbinu za kudhoofisha mijadala hapa.Nangoja na feel free to clear the air .
 
Hapana nataka ES aseme shutuma zake kwa uwazi kabla hatuja endelea na mambo ya Kiteto. Es please nakupa ruhusa sema kwa uwazi .

Mikwara mbuzi hakuna chochote Cyber-bullying ishapitwa na wakati one minute wanakuwa watetezi wa personal attacks na ku reveal identity za watu the next minute hao hao wanatishia watu.

Tumechoka kama ana data aweke hapa mtu mzima atishiwi nyau hapa ni kumkoma Nyani Giladi kwa kwenda mbele tu...
 
nI WAKATI HUU AMBAPO WANAHITAJI KUWA MAKINI SANA. VIONGOZI WA UPINZANI WOTE WAUNGANE NA CHADEMA,KWANI NDIYO CHAMA AMBACHO KIPO JUU SANA KWA SASA. KUMBUKUMBU NILIZONAZO KWENYE ILE ZOMEAZOMEA TOUR YA MAWAZIRI,KULE KITETO PIA WALIZOMEWA. KWAHIYO WAPINZANI WAUNGANE KIKWELIKWELI
 
Masatu nakubaliana nawe kabisa . Mimi nimesema ukweli baada ya yeye kusema dume la mbegu . Malecela ni kweli dume la Mbegu maana ana watoto kibao wa nje wengine tunao humu humu. Hili si jungu na niko tayari kuwataja majina nani mtoto wa nje ya ndoa ya Malecela. Yeye anageuza issue na mimi nasema taja na nanghoja hili ili watu waamini kwamba una data za personal life za watu . Kindly go ahead taja mambo ya Botswana mimi nikeurahisishia moja . Kwa jina kamili mimi naitwa Lunyungu na wala situmii nicknames kama wewe FMES ambaye majina yako si haya .Mimi si mnafiki na siogopi . Sasa nakutaka utaje ili uaminiwe na forum kwamba kweli unajua mambo . Kwenye hili ndipo watakujua kama you are real am hoax and pretender. Nangoja
 
Hili si jungu na niko tayari kuwataja majina nani mtoto wa nje ya ndoa ya Malecela. Yeye anageuza issue na mimi nasema taja na nanghoja hili ili watu waamini kwamba una data za personal life za watu

Wakubwa zangu tusipoteze uelekeo hapa kama ni personal issues zitakazo saidia ushindi wa jimbo la Kiteto tuweekeni hapa lakini ni kama kuiabishana tuache nawasihi......isije kuwa ganzi za mafisadi zinaanza kushambulia wana JF...
 
Ushirombo
Mimi natumia jina langu halisi hapa . Kwanza sijaoa na wala sina mke .Kuelezwa habari hizi na kupewa connection na mke wa mtu Botswana na mimi sitakubali . Nampa muda aseme ukweli hapa .Na kama alitaka kuvuruga mada kwa makusudi basi aje aombe msamaha kwa wanajambo na mimi mwenyewe kwamba alitaka kujipatia ujiko . Vinginevyo sikubali maana hili ni jina langu halisi tofauti na wewe unayetumia Ushirombo . Aje clean tuendelee na hoja .Siwezi kupinga ufisadi na huku nikawa naendekeza ufisadi .Kuwa na mke wa mtu ni hatari na ni Ufisadi ambao CCM pekee ndiyo vinara kuanzia kwa pesa hadi wake wa wenzao .Mimi hapana he need to clear my name kwa kuomba msamaha .Nasema aongee hapa kwa uwazi siogopi kuaibika .Tunataka kukomesha majungu hapa .
 
USHAURI WA BURE
Wakati CCM wanajipanga kupata ushindi kule Kiteto nyie Chadema na wengineo mnapiga porojo tu hapa, so far hakuna habari / taarifa yeyote inayoelezea walau mwelekeo wa uchaguzi na huenda nani ataibuka mshindi na kwa vigezo gani.
Nilitaraji kuwa walau hata wale wenye taaluma ya uandika habari wange tuletea kujua hali ya maisha ya Kiteto yakoje, ni nini matarajio ya wananchi wa jimbo hilo nk.
Hii ingesaidia kwa wanaJF wengi kupata picha ya hali halisi ya Kiteto kabla ya uchaguzi.
Wasiwasi wangu kuwa wengi wa wachangiaji wanaona kuwa tayari jimbo la Kiteto limekwisha chukuliwa na upinzani, kumbukeni kuwa:
CCM ni chama bora na imara katika medani za siasa hapa Tanzania
Pili, Wananchi wa Kiteto si mambumbumbu kwamba hawajui wanachokitaka.
Fanyeni kazi ya ziada tupate habari za uhakika otherwise siku ya siku msije na stori nyingine kuwa kura ziliibiwa kumbe hazukutosha.
 
USHAURI WA BURE
Wakati CCM wanajipanga kupata ushindi kule Kiteto nyie Chadema na wengineo mnapiga porojo tu hapa, so far hakuna habari / taarifa yeyote inayoelezea walau mwelekeo wa uchaguzi na huenda nani ataibuka mshindi na kwa vigezo gani.
Nilitaraji kuwa walau hata wale wenye taaluma ya uandika habari wange tuletea kujua hali ya maisha ya Kiteto yakoje, ni nini matarajio ya wananchi wa jimbo hilo nk.
Hii ingesaidia kwa wanaJF wengi kupata picha ya hali halisi ya Kiteto kabla ya uchaguzi.
Wasiwasi wangu kuwa wengi wa wachangiaji wanaona kuwa tayari jimbo la Kiteto limekwisha chukuliwa na upinzani, kumbukeni kuwa:
CCM ni chama bora na imara katika medani za siasa hapa Tanzania
Pili, Wananchi wa Kiteto si mambumbumbu kwamba hawajui wanachokitaka.
Fanyeni kazi ya ziada tupate habari za uhakika otherwise siku ya siku msije na stori nyingine kuwa kura ziliibiwa kumbe hazukutosha.


Umesema CCM ni Chama bora na Imara ? Ubora kivipi na Uimara wake uko wapi ? Labda hao waandishi unao wataka wako nje wanatafuta habari na labda wao si wana JF so tutapataje habari za huko? Nani kakueleza kwamba wapinzani wanaona wamesha pata jimbo wakati umesoma hapo juu kwamba wana hangaikia Mgombea kuwekewa pingamizi ?Au hizi si habari mpaka waandike kile wewe wataka kukisikia ?
 
Nimewapa taarifa kuwa Kimesera kawekewa pingamizi na mgombea wa CCM ambalo halina kichwa wala miguu ndio linatatuliwa muda huu jaribu kurudi page 13 utaona nilichowapa nashangaa watu wanajadili issue zao binafsi hapa , ama hamkuelewa maana ya kuwekewa pingamizi?
 
Nimewapa taarifa kuwa Kimesera kawekewa pingamizi na mgombea wa CCM ambalo halina kichwa wala miguu ndio linatatuliwa muda huu jaribu kurudi page 13 utaona nilichowapa nashangaa watu wanajadili issue zao binafsi hapa , ama hamkuelewa maana ya kuwekewa pingamizi?

Mkuu,

Tumeona hilo na tunasubiri kujua hilo pingamizi limeishia wapi. Nafikiri sheria ya pingamizi ni katika sheria mbovu. Inatakiwa baada ya pingamizi kuwe na muda wa kutosha kwa chama kuwakilisha jina lingine kama inaonekana aliyepingwa hana sifa.

Nagu anatuambia katiba yetu ni imara, in fact ni bomu hasa.

Tunashukuru kwa taarifa kutoka Kiteto.
 
Jamani wandugu ,habarini za leo kilichojiri hapa kwetu kijiweni yaani Kiteto ni kuwa mgombea wa upinzani kawekewa pingamizi na mgombea wa CCM.

sababu ya pingamizi ni kuwa eti Kimesera aliwahi kufungwa siku moja mwaka 1996 kwa kosa la trafick baada ya kuvuka taa nyekundu pale ubungo na alikaa ndani kwa muda wa siku moja tuu na kesho yake hukumu ikafutwa na hata yeye alikuwa tayari amesahau juu ya jambo hilo.

Kumbukeni kuwa alikuwa mgombea 2000 na 2005 ila hilo pingamizi halikuwahi kuwekwa ila ndio limewekwa leo ila kwa vile ushirikiano wa vyama walikuwa na vyanzo vya habari kutoka ndani ya CCM walikuwa wameshapata habari hizo na ndio maana waskatuma timu ya wanasheria kwenda huko ili kuweka mambo sawa na timu hiyo inaongozwa na wakili na mbunge Halima mdee.

Nitaendelea kuwahabarisha ilka jueni tuu kwamba pingamizi lao ni base less kwani sheria ya uchaguzi iko wazi juu ya mamabo kama hayo .

Jamani.. CCM wanaanza kutetemeka sasa.. mbona safari ndiyo imeanza tu...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom