Uchaguzi wa Marekani umemalizika, tumeona umuhimu wa kujenga taasisi imara sio watu imara

Uchaguzi wa Marekani umemalizika, tumeona umuhimu wa kujenga taasisi imara sio watu imara

Wewe muongo angalia polisi wa Marekani walivyokuwa wanatoa kipigo cha Mbwa koko you tube -

Chaos in Washington as Trump supporters storm Capitol and force lockdown of Congress​

Nani kasema hawakutoa kipigo na sio kipigo tu hata kuua wameua lkn hoja yangu kuu sio hiyo.
 
Jaribu kufikiri kama hilo lingetokea Dodoma watu wamevamia pale Bungeni kuzuia wakina Mdee wasiapishwe, wanavamia wanaingia hadi kwenye ofisi ya Ndungai, jaribu kupata picha nini kingetokea! nadhani mitaro yote hapo jirani ingejaa maji mekundu nasema hivyo si kwa sababu za kisiasa ila ueredi wa kukabiriana na hali kama hiyo hatuna kabisa,hasa ikijulikana wanaoandamana ni wa upande furani aaa hapo ndio kabisaaa, ungeshuhudia mambo yakusikitisha na kukusononesha maisha yako yote mpaka utakapoingia kaburini.
Uzuri ni kwamba Tanzania hakuna waandamanaji wenye weledi pia! Hawawezi andamana.
 
Wanafanya sana na polisi ndio watatoa ulinzi. Usidhani hatuelewi, hapa kwetu rais ndio Mungu, na taasisi zote taka zisitake lazima zitii atakacho. Mfano uchaguzi wa juzi taasisi zote zimesimamia wizi wa kura na mauji, maana rais alitaka yeye na chama chake watangazwe washindi.
Una ushahidi wa haya madai yako au ni mwendelezo tu wa porojo?
 
Pamoja na "MATAGA" wa marekani kuandamana wakitaka bwana "TRUMP" asalie madarakani pamoja na kushindwa, ila hujasikia IGP wakule akisema watapigwa kipigo cha mbwa koko, makamo wa raisi Mike Pence yani mama Samia Suluhu Wakule kasema "MATAGA" hao wanaiaibisha MAREKANI.
Ccm na vibaraka wenu mna la kujifunza.
Wao ndio wanachakujifunza kutoka Kwetu Haiwezekani wahuni waandamane waongie kwe ye ofisi za Bunge, sisi Tumefanikiwa kuwatoa vibaraka waliotakwa kuuza nchi yetu, na taasisi zetu Imara zilihakikisha hakuna vurugu za kudumu muda mlefu
 
Ndio, ni sahihi polisi kudhibiti ghasia.

Ulitakaje labda?

Lakini unaweza kuona namna taasisi ya polisi inavyotumika kwa nidhamu.

Ingekuwa Tanganyika, polisi wanapata wapi ujasiri wa kuwadhibiti wafuasi wa rais aliyeko madarakani? Ulikisia wapi?

Ni sawa na polisi wawapige wanachama wa CCM! Thubutu! Huyo mkuu wa kituo atashughulikiwa mpaka maji aite mma.

Na mapolisi waliohusika wangefukuzwa kazi summarily na kuwa disarmed immediately!

Huko kwenye hako kanchi kenu cha kufikirika, polisi ni mali ya chama.

Kwenye nchi zenye nidhamu ya kisiasa, polisi ni taasisi huru inayofanya kazi professionally, sio kufuata matakwa ya mwenyekiti wa UENEZI sijui.

Mimi huwa nasikia tu, mara sijui mwenyekiti wa UENEZI ameamrisha polisi!

Kuna siku Magufuli alipokea wanaccm waliohamia kwenye kamisheni ya jeshi huko Arusha mchana wa saa 7, huku CDF akitabasamu kwa huo uzalendo, wakati jeshi limetengwa kikatiba na siasa. Pale ndio nilishuhudia ulevi wa madaraka wa kiwango cha juu.
 
Una ushahidi wa haya madai yako au ni mwendelezo tu wa porojo?
Ushahidi ninao wa kutosha, je huo ushahidi naupeleka wapi wakati taasisi zinazopaswa kusimamia sheria na zenyewe ni sehemu ya hizo taasisi dhaifu? Taasisi za hapa ziko kukandamiza yoyote aliye kinyume na watawala, na huu ni udhaifu uliopo ndani ya katiba unaomfanya rais asishitakiwe akiwa madarakani au akiwa ametoka. Ila iko siku mambo haya yatafikia mwisho.
 
Wao ndio wanachakujifunza kutoka Kwetu Haiwezekani wahuni waandamane waongie kwe ye ofisi za Bunge, sisi Tumefanikiwa kuwatoa vibaraka waliotakwa kuuza nchi yetu, na taasisi zetu Imara zilihakikisha hakuna vurugu za kudumu muda mlefu
Kwa nini mnawang'ang'ania covid 19,mlishafeli na mtaendelea kufeli.
 
Rais wa marekani, the most POWERFUL MAN on the planet, lakini anabwata tu TWITA na hana cha kufanya.

Taasisi ziko imara ZINAMDHIBITI ipasavyo na ulevi wake.

Mahakama zinamdhibiti, Bunge linamdhibiti. Amebaki kubwata tu kama kifaranga yatima.

That is a perfect display of how CHECKS AND BALANCES work.

Taasisi imara kweli kweli. Hazibabaishwi na wajinga wajinga.

Huko Tanganyika, kwenye kanchi fukara kalichojichokea kwa umasikini, unakutana na vimungu mtu vingi ajabu.

Vimungu mtu viko juu ya taasisi. Havigusiki.

Hata katoto cha uvccm kana uwezo wa KUMUAMURU JAJI na kumtisha kwa vimemo!

Ati oohh unanijua mimi ni nani!! EBOO!!!!!!!
Aisome Crimea mezani kwake.
 
Ndio, ni sahihi polisi kudhibiti ghasia.

Ulitakaje labda?

Lakini unaweza kuona namna taasisi ya polisi inavyotumika kwa nidhamu.

Ingekuwa Tanganyika, polisi wanapata wapi ujasiri wa kuwadhibiti wafuasi wa rais aliyeko madarakani? Ulikisia wapi?

Ni sawa na polisi wawapige wanachama wa CCM! Thubutu! Huyo mkuu wa kituo atashughulikiwa mpaka maji aite mma.

Na mapolisi waliohusika wangefukuzwa kazi summarily na kuwa disarmed immediately!

Huko kwenye hako kanchi kenu cha kufikirika, polisi ni mali ya chama.

Kwenye nchi zenye nidhamu ya kisiasa, polisi ni taasisi huru inayofanya kazi professionally, sio kufuata matakwa ya mwenyekiti wa UENEZI sijui.

Mimi huwa nasikia tu, mara sijui mwenyekiti wa UENEZI ameamrisha polisi!
Hapa ndipo wangwafi alikua hajaelewa. Polisi kumdhibiti au kudhibiti supporters wa rais aliye madarakani... Afrika!???
 
Uchaguzi wa Marekani umemalizika rasmi leo usiku kwa Rais mteule Joe Biden kuthibitishwa na mabunge yote mawili kuwa rais wa nchi hiyo baada ya rais Trump kwa kipindi cha miezi miwili kuhangaika kupinga matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika Novemba mwaka jana.

Tulichojifunza zaidi ni jinsi uchaguzi huu ulivyofanyika na mapungufu yake yalivyofanyiwa kazi na vyombo husika chini ya mihimili mitatu ya nchi hiyo na jinsi utawala wa sheria ulivyoheshimiwa na demokrasia kuachwa ichukue mkondo wake.

Baada ya matokeo kutangazwa Trump alipeleka malalamiko yake Mahakamani akipinga matokeo ya baadhi ya majimbo, mahakama ikasema malalamiko yake hayakuwa na msingi wowote kwa vile hayana ushahidi.

A district court in Nevada shot down the Trump’s claims, finding “that there is no credible or reliable evidence that the 2020 General Election was affected by fraud.”

Jumamosi 2/1/2021 simu ya Trump ilidukuliwa akimpigia Afisa Tume ya uchaguzi wa Georgia Brad Raffensperger akitaka atafute kura 11,780 za ushindi akakataliwa.

“I just want to find 11,780 votes, which is one more than we have. Because we won the state," said Trump on call.

“President Trump, we’ve had several lawsuits, and we’ve had to respond in court to the lawsuits and the contentions," Raffensperger told Trump on the call. "We don’t agree that you have won."

Siku chache kabla ya Bunge la Congress kukutana kuthibitisha ushindi wa Biden, Makamu wa rais Mike Pence alikataa shinikizo la boss wake Trump la kumtaka kuingilia kati matokeo ya kura Electral College Votes na kuzuia kuthibitishwa kwa Rais mteule Jo Biden, Pence alimwambia hana uwezo huo.

"Our Founders were deeply skeptical of concentrations of power and created a Republic based on separation of powers and checks and balances under the Constitution.”

"The Presidency belongs to the American people, and to them alone," Pence told Trump.

Huu ni uthibitisho kuwa viongozi wengi walisimamia haki, utawala wa sheria, imagine makamu wa rais wa Tanzania au nchi yeyote ya Afrika angekataa maelekezo ya rais aliye madarakani.

Baada ya Trump kuona ugumu wa kuitumia mihimili ya Mahakama, Ofisi ya rais White House na Bunge, suluhisho la mwisho lilikuwa ni kuwatumia wafuasi wake na baadhi ya wabunge wa chama chake kuvamia bunge na kujaribu kuzuia mjadala wa kumthibitisha Biden kwa nguvu jaribio ambalo nalo halikufanikiwa.

Mitchell McConnell wa chama cha REPUBLICAN chama anachotoka TRUMP ndani ya Congress alisema;

"I will vote to respect the American people’s decision & defend our system of government. My full remarks".

Kwa Tanzania ni mbunge gani wa chama tawala anaweza kumwambia hivyo rais aliye madarakani.

Pamoja na wafuasi wa Trump kuvamia na kuingia hadi kwenye ukumbi wa bunge na ofisi ya Spika hatukuona polisi kutumia nguvu kupita kiasi kuwatawanya, najiuliza ingekuwa Dodoma watu wamevamia bunge kiasi hicho wakati huu tungekuwa na vifo vingapi na gereza la Isanga lisingetosha.

Pamoja na hayo yote leo Trump amekubali kukabidhi madaraka ifikapo 20/1/2021. Bila taasisi imara leo Trump asingekubali kutoka madarakani.

Tujifunze kuheshimu taasisi zetu, katiba na sheria tulizojitungia na tuache uhuru wa wananchi kufikisha hisia zao kwa vyombo vinavyohusika. Tutumie uchaguzi wa Marekani kuwa kama somo kwetu hasa kwa watawala wa nchi zetu za ki Afrika wanaojiona wao kama miungu watu, kuwa hakuna aliye juu ya sheria hata kama ni rais.
Pole sana ndugu yangu, lakini muda mwingine inapendeza ukichukua kitabu cha hadithi na kuingia msituni na kuanza kukisoma kwa sauti kubwa sababu huwezi juwa pengine wengine wakakusikiliza na kukifurahia. Kama hawakumuelewa Lissu na akina Lema, Msigwa sijui kama leo watakuelewa wewe. Watanzania walipiga kura kwa kishindo wakishirikiana na wakurugenzi ili kuchagua maendeleo ya Chato Ova.
 
Uchaguzi wa Marekani umemalizika rasmi leo usiku kwa Rais mteule Joe Biden kuthibitishwa na mabunge yote mawili kuwa rais wa nchi hiyo baada ya rais Trump kwa kipindi cha miezi miwili kuhangaika kupinga matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika Novemba mwaka jana.

Tulichojifunza zaidi ni jinsi uchaguzi huu ulivyofanyika na mapungufu yake yalivyofanyiwa kazi na vyombo husika chini ya mihimili mitatu ya nchi hiyo na jinsi utawala wa sheria ulivyoheshimiwa na demokrasia kuachwa ichukue mkondo wake.

Baada ya matokeo kutangazwa Trump alipeleka malalamiko yake Mahakamani akipinga matokeo ya baadhi ya majimbo, mahakama ikasema malalamiko yake hayakuwa na msingi wowote kwa vile hayana ushahidi.

A district court in Nevada shot down the Trump’s claims, finding “that there is no credible or reliable evidence that the 2020 General Election was affected by fraud.”

Jumamosi 2/1/2021 simu ya Trump ilidukuliwa akimpigia Afisa Tume ya uchaguzi wa Georgia Brad Raffensperger akitaka atafute kura 11,780 za ushindi akakataliwa.

“I just want to find 11,780 votes, which is one more than we have. Because we won the state," said Trump on call.

“President Trump, we’ve had several lawsuits, and we’ve had to respond in court to the lawsuits and the contentions," Raffensperger told Trump on the call. "We don’t agree that you have won."

Siku chache kabla ya Bunge la Congress kukutana kuthibitisha ushindi wa Biden, Makamu wa rais Mike Pence alikataa shinikizo la boss wake Trump la kumtaka kuingilia kati matokeo ya kura Electral College Votes na kuzuia kuthibitishwa kwa Rais mteule Jo Biden, Pence alimwambia hana uwezo huo.

"Our Founders were deeply skeptical of concentrations of power and created a Republic based on separation of powers and checks and balances under the Constitution.”

"The Presidency belongs to the American people, and to them alone," Pence told Trump.

Huu ni uthibitisho kuwa viongozi wengi walisimamia haki, utawala wa sheria, imagine makamu wa rais wa Tanzania au nchi yeyote ya Afrika angekataa maelekezo ya rais aliye madarakani.

Baada ya Trump kuona ugumu wa kuitumia mihimili ya Mahakama, Ofisi ya rais White House na Bunge, suluhisho la mwisho lilikuwa ni kuwatumia wafuasi wake na baadhi ya wabunge wa chama chake kuvamia bunge na kujaribu kuzuia mjadala wa kumthibitisha Biden kwa nguvu jaribio ambalo nalo halikufanikiwa.

Mitchell McConnell wa chama cha REPUBLICAN chama anachotoka TRUMP ndani ya Congress alisema;

"I will vote to respect the American people’s decision & defend our system of government. My full remarks".

Kwa Tanzania ni mbunge gani wa chama tawala anaweza kumwambia hivyo rais aliye madarakani.

Pamoja na wafuasi wa Trump kuvamia na kuingia hadi kwenye ukumbi wa bunge na ofisi ya Spika hatukuona polisi kutumia nguvu kupita kiasi kuwatawanya, najiuliza ingekuwa Dodoma watu wamevamia bunge kiasi hicho wakati huu tungekuwa na vifo vingapi na gereza la Isanga lisingetosha.

Pamoja na hayo yote leo Trump amekubali kukabidhi madaraka ifikapo 20/1/2021. Bila taasisi imara leo Trump asingekubali kutoka madarakani.

Tujifunze kuheshimu taasisi zetu, katiba na sheria tulizojitungia na tuache uhuru wa wananchi kufikisha hisia zao kwa vyombo vinavyohusika. Tutumie uchaguzi wa Marekani kuwa kama somo kwetu hasa kwa watawala wa nchi zetu za ki Afrika wanaojiona wao kama miungu watu, kuwa hakuna aliye juu ya sheria hata kama ni rais.
Ni kweli kabisa watanzani (Tanzania) na vyombo vyake vyote vya dola ikiwemo mahaka na nchi zote za Africa watoe mfano na kuiga utawala wa sheria, democrasia na katiba kama ndugu zetu wa USA (Marekani).
Na vyombo vyetu hivi vya dola kama mahakama, tume ya uchaguzi, jeshi(polisi) visiingiliwe na wanasiasa wala wasijihusishe na wanasiasa (siasa) bila ya kujali ni mwanasiasa wa chama gani anaongoza nchi, vyombo vyote vya dola viwe huru na kufuata sheria.
Kama katiba yetu hairuhusu hayo, basi katiba yetu ibadilishwe mapema mno kwaajili ya maslahi sawa kwa wote na haki sawa kwa wote. Ikiwezekana katiba yetu na za nchi nyingine za Africa iwe kama ya USA(Marekani) kabisa. (Mazuri tuyaige na kuyachukua, mabaya tuwaachie na tuyaache)
Hii itasaidia sana kukomaza democrasia na kupunguza mabavu ya watawala wanaong'ang'ania madaraka na kufanya mambo kama watakavyo katika nchi zetu hizi za Africa. Mfano mzuri tumekwisha jionea USA(Marekani).
 
Achana na ujinga wa hao wamarekani, uchaguzi umeonyesha madhaifu ya hiyo wanayoita demokrasia. Uchaguzi toka mwaka jana mtu ameshindwa anapigia tu kelele. Ndio maana sisi tuna taasisi imara kama jeshi la polisi, ukishindwa umeshindwa unakaa kimya.

Kwa uimara wa jeshi letu hakuna hata mjinga mmoja aliyesogeza pua yake nje eti kuandamana kupinga matokeo, hao wamarekani mpaka watu wanaingia kwnye jengo la bunge ni upuuzi tu, ni muhimu huku kwetu polisi waimarishwe zaidi na kupewa meno, ili wajinga wachache na vibaraka wa mabeberu watakaotaka kuiga hayo ya wamarekani waadabishwe wapugwe mpaka wachakaee.
You are more than Idiot!
 
Mleta maada unajua maana ya Democracy. Unafiriki Democracy ni upinzani kuangusha chama tawala. Acha kuwadanganya watanzania. Ivi unamlaumu Trumpo au unalaamu sera Republican zinazolinda matajiri na viongozi . Subiri kilio cha kufungwa kwa biashara na kodi kubwa, madawa ya kulevya ,bangi, ushoga, huko kipindia cha Democractic ya Biden
 
Watanzania wote kwa pamoja tuzikatae sera za chama Biden demo, zinazohawalisha Bangi na Ushoga, freemason,. Mungu mbariki Trumpo, kwa kupamba mashoga,vibaka, madawa, Kusababisha amani ya dunia hasa mashariki ya kati.
 
Kilichooneka marekani sio democrasia, Kwa sababu hizi. 01. Trumpo anadai ameibiwa kura. 2. Black american 90% vote Biden 3.Most asian vote for biden 4.wahamiaji ,vibaka, waharifu vote biden. 5. Biden amewadanyanya wasio na elimu kuwa Trumpo amesababisha watu kufa kwa Covid-19. Ndio maana Trumpo anasema ushindi wa biden ni wa udanyanyifu, kwa sababu amepata kula kwa kudanyanya watu juu covid-19, ubaguzi wamarekani weusi
 
Huku hakuna taasisi imara ni maagizo kutoka juu mara moja yanatekelezwa kama ingekuwa kwetu kitendo cha rais Trump kupinga matokeo jeshi la polisi lingemsapoti,mahakama ingemsapoti,chama chake kingemsapoti,makamu wa rais angemsapoti,usalama wa taifa wangemsapoti na Biden mpaka wa leo angalikuwa korokoroni upo.
Nimecheka kwa sauti kubwa😂😂😂
 
Watanzania wote kwa pamoja tuzikatae sera za chama Biden demo
Ona huyu mlevi sijui katoka wapi?

Sasa wewe ndugu yangu unaishi namtumbo huko maporini unawaambia watu wamkatae Biden?

Unaota au umekunywa makonyagi?
 
Back
Top Bottom