Uchaguzi wa Marekani umemalizika, tumeona umuhimu wa kujenga taasisi imara sio watu imara

Wewe muongo angalia polisi wa Marekani walivyokuwa wanatoa kipigo cha Mbwa koko you tube -

Chaos in Washington as Trump supporters storm Capitol and force lockdown of Congress​

Nani kasema hawakutoa kipigo na sio kipigo tu hata kuua wameua lkn hoja yangu kuu sio hiyo.
 
Uzuri ni kwamba Tanzania hakuna waandamanaji wenye weledi pia! Hawawezi andamana.
 
Una ushahidi wa haya madai yako au ni mwendelezo tu wa porojo?
 
Wao ndio wanachakujifunza kutoka Kwetu Haiwezekani wahuni waandamane waongie kwe ye ofisi za Bunge, sisi Tumefanikiwa kuwatoa vibaraka waliotakwa kuuza nchi yetu, na taasisi zetu Imara zilihakikisha hakuna vurugu za kudumu muda mlefu
 

Kuna siku Magufuli alipokea wanaccm waliohamia kwenye kamisheni ya jeshi huko Arusha mchana wa saa 7, huku CDF akitabasamu kwa huo uzalendo, wakati jeshi limetengwa kikatiba na siasa. Pale ndio nilishuhudia ulevi wa madaraka wa kiwango cha juu.
 
Una ushahidi wa haya madai yako au ni mwendelezo tu wa porojo?
Ushahidi ninao wa kutosha, je huo ushahidi naupeleka wapi wakati taasisi zinazopaswa kusimamia sheria na zenyewe ni sehemu ya hizo taasisi dhaifu? Taasisi za hapa ziko kukandamiza yoyote aliye kinyume na watawala, na huu ni udhaifu uliopo ndani ya katiba unaomfanya rais asishitakiwe akiwa madarakani au akiwa ametoka. Ila iko siku mambo haya yatafikia mwisho.
 
Wao ndio wanachakujifunza kutoka Kwetu Haiwezekani wahuni waandamane waongie kwe ye ofisi za Bunge, sisi Tumefanikiwa kuwatoa vibaraka waliotakwa kuuza nchi yetu, na taasisi zetu Imara zilihakikisha hakuna vurugu za kudumu muda mlefu
Kwa nini mnawang'ang'ania covid 19,mlishafeli na mtaendelea kufeli.
 
Aisome Crimea mezani kwake.
 
Hapa ndipo wangwafi alikua hajaelewa. Polisi kumdhibiti au kudhibiti supporters wa rais aliye madarakani... Afrika!???
 
Pole sana ndugu yangu, lakini muda mwingine inapendeza ukichukua kitabu cha hadithi na kuingia msituni na kuanza kukisoma kwa sauti kubwa sababu huwezi juwa pengine wengine wakakusikiliza na kukifurahia. Kama hawakumuelewa Lissu na akina Lema, Msigwa sijui kama leo watakuelewa wewe. Watanzania walipiga kura kwa kishindo wakishirikiana na wakurugenzi ili kuchagua maendeleo ya Chato Ova.
 
Ni kweli kabisa watanzani (Tanzania) na vyombo vyake vyote vya dola ikiwemo mahaka na nchi zote za Africa watoe mfano na kuiga utawala wa sheria, democrasia na katiba kama ndugu zetu wa USA (Marekani).
Na vyombo vyetu hivi vya dola kama mahakama, tume ya uchaguzi, jeshi(polisi) visiingiliwe na wanasiasa wala wasijihusishe na wanasiasa (siasa) bila ya kujali ni mwanasiasa wa chama gani anaongoza nchi, vyombo vyote vya dola viwe huru na kufuata sheria.
Kama katiba yetu hairuhusu hayo, basi katiba yetu ibadilishwe mapema mno kwaajili ya maslahi sawa kwa wote na haki sawa kwa wote. Ikiwezekana katiba yetu na za nchi nyingine za Africa iwe kama ya USA(Marekani) kabisa. (Mazuri tuyaige na kuyachukua, mabaya tuwaachie na tuyaache)
Hii itasaidia sana kukomaza democrasia na kupunguza mabavu ya watawala wanaong'ang'ania madaraka na kufanya mambo kama watakavyo katika nchi zetu hizi za Africa. Mfano mzuri tumekwisha jionea USA(Marekani).
 
You are more than Idiot!
 
Mleta maada unajua maana ya Democracy. Unafiriki Democracy ni upinzani kuangusha chama tawala. Acha kuwadanganya watanzania. Ivi unamlaumu Trumpo au unalaamu sera Republican zinazolinda matajiri na viongozi . Subiri kilio cha kufungwa kwa biashara na kodi kubwa, madawa ya kulevya ,bangi, ushoga, huko kipindia cha Democractic ya Biden
 
Watanzania wote kwa pamoja tuzikatae sera za chama Biden demo, zinazohawalisha Bangi na Ushoga, freemason,. Mungu mbariki Trumpo, kwa kupamba mashoga,vibaka, madawa, Kusababisha amani ya dunia hasa mashariki ya kati.
 
Tulio gizani, porini tunaangalia walio kwenye mwanga wanavyoishi.
 
Kilichooneka marekani sio democrasia, Kwa sababu hizi. 01. Trumpo anadai ameibiwa kura. 2. Black american 90% vote Biden 3.Most asian vote for biden 4.wahamiaji ,vibaka, waharifu vote biden. 5. Biden amewadanyanya wasio na elimu kuwa Trumpo amesababisha watu kufa kwa Covid-19. Ndio maana Trumpo anasema ushindi wa biden ni wa udanyanyifu, kwa sababu amepata kula kwa kudanyanya watu juu covid-19, ubaguzi wamarekani weusi
 
Nimecheka kwa sauti kubwa😂😂😂
 
Watanzania wote kwa pamoja tuzikatae sera za chama Biden demo
Ona huyu mlevi sijui katoka wapi?

Sasa wewe ndugu yangu unaishi namtumbo huko maporini unawaambia watu wamkatae Biden?

Unaota au umekunywa makonyagi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…