Uchaguzi wa Marekani umemalizika, tumeona umuhimu wa kujenga taasisi imara sio watu imara

Marekani ndio waje wajifunze kwetu maana ni aibu kubwa kwa Taifa kama lile kufanya uchaguzi kwa kelele.
Ni wazi viongozi wa Marekani wamekosa Political torelance.
No democracy in U. S wao ndio waje wajifunze kwetu.
 
Taasisi zetu ni imara lakini zilijengwa kwa ajili ya kukilinda na kukiimarisha chama tawala kiendelee kukaa madarakani. Hi ni tofauti na nchi za magharibi kama Marekani ambazo taasisi na katiba zao ni kuongeza udhaifu wa serikali (limit government power) kwa kutumia checks and balances. Hata Nyerere alivyopendekeza mfumo wa vyama vingi nia yake ilikuwa ni kuimarisha CCM maana alionea wanaenda vibaya. Siyo kwamba alitegemea kuna siku upinzani utashinda na kutawala nchi.
 
Kwani kwenye hizo vurugu za Marekani hakuna waliokufa ? Usipindishe ukweli. Tabia ya kupinga kila kitu bila ushahidi hapa TZ ndio kilichoathiri upinzani hapa kwetu. USA wamethibitisha kwamba Demokrasia mnayoimba usiku na mchana siyo rahisi kivile ni ushabiki maandazi tu.
 
Huna hoja wewe. Unawajua waliouawa wewe ? Popote duniani ukileta ujuaji wa kupinga pinga unakula shaba tu.
 
Nani kapindua matokeo hapa kwetu ? Toka kampeini zilipoanza hapa kwetu mgombea uraisi wa upinzani ni kutoa matusi tu bila hoja za msingi. Unategemea angeshinda uraisi huyo ? Pinga pinga popote duniani mwisho wao ni huwa ni shaba tu kama ilivyotokea kwa hao wanaojiita wanademokrasia ( USA ).
 
Ingetokea sawa tu yaliyotokea USA. Ni kula shaba kwa kwenda mbele. Kwa nini ubembelezwe na wewe unaleta fujo ?
 
Kwa sababu nni Kiongozi halali.
 
Wamepigwa sana tu.
 
Kama zilivyo na nguvu Taasisi zetu. Kuwatia adabu pinga pinga wote wa bila sababu.
Sio kwamba hawajui kuwa taasisi za huko zina nguvu, bali wanajaribu kupotosha ili tusione nguvu ya hizo taasisi.
 
Imetumika kwa nidhamu wakati kuna watu wamelamba shaba, we vipi ?
 
Marekani wameiga kwetu ukipinga bila sababu na kuleta vurugu ni shaba tu
 
Kwani wazungu siyo wahamiaji huko USA ? Yaani hata historia hujui ! Pole sana
 
Kwani Tanzania kuna upinzani?
 
Naona umejaribu kutafuta "angle" nzuri ya kupenyeza ajenda yako katika hili.

Inawezekana ni kweli hizo taasisi unazozisema zikawa na nguvu na kutekeleza majukumu yao kulingana na matakwa ya wananchi.

Lakini Marekani wana taasisi nyingi sana zenye majukumu mbalimbali hivyo tukio hili pia limetufunza kwamba katika masuala ya kiusalama ilitakiwa Donald trump apitie vinu vikali kabla ya jina lake kupendekezwa mgombea wa uraisi mwaka 2015.

Hilo ni kosa namba moja, kumwachia mtu kama Donald Trump ambae mpaka sasa anaonekana ana mapungufu kiakili, kushika ofisi kubwa duniani ya uraisi na kukalia vitufe vya makombora ya nyuklia.

Pili, kuhusu ghasia za Capitol ni kwamba hakukuwepo polisi wa kutosha kwenye first barrier of security hivyo kulipotokea breach ikawa ngumu kwa polisi wachache walokuwepo kukabiliana na uwingi wa wafanya vurugu.

Hivyo hakukuwepo mpangilio maalum au planning kwamba Capitol pana mjadala wa kumpitisha Biden hivyo security lazima ingekuwa "beefed up".

Na mwisho ni kushindwa kwa integensia kutambua kuwepo na mpango wa vurugu hizo ambazo zimesababisha vifo vya watu watano akiwepo askari polisi.

Yaani vyombo vya kijasusi vya Marekani NSA, FBI na vingine kushindwa kubaini mipango ya vurugu, hapo pia tuna la kujifunza kwa upande wetu kama kainchi ka Afrika.

Ila vyombo vya usalama vya Tanzania pamoja na kauwezo vilivyo navyo vilijiandaa mapema kabla, wakati na baada ya uchaguzi na moja ya maeneo ya kuyaangalia kwa ukaribu ilikuwa ni mitandao ya kijamii na kuhakikisha Tweeter haitumiwi vibaya kusambaza taharuki.
 
Wewe ni ntu makini na tena mwenye busara sana
 
Taasisi zote muhimu Nchini JWTZ, polisiccm, tume ya uchaguzi, Bunge, mahakama, maadili ya viongozi, TAKUKURU, media huyo anayejiita mwendawazimu kaziweka mfukoni. Hakuna wa KUFURUKUTA.
Huwezi kukabili hisia zako mpk utukane we mbwiga?Utafikiwa ulipo bwege wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…