Torra Siabba
JF-Expert Member
- Jul 24, 2016
- 289
- 415
Chama cha soka Mkoa wa Mbeya kesho aprili 6, kinatarajia kufanya uchaguz wa kuwapata viongozi wake lakini cha ajabu kuna madudu ambayo yanaweza kusababisha maafa jambo ambalo ni muhimu kwa serikali, na wadau wengine kuingilia kati ili Haki ipatikane na mkoa uweze kuongozeka.
Iko hivi, awali mchakato wa uchaguzi ulikua unasimamiwa na Kamati ya uchaguzi ya mkoa wa Mbeya, baadae ikaonekana kwamba hawafai, Ikabidi TFF ndio walete kamati yao ya uchaguzi ndio isimamie huu uchaguzi, ile kamati ya mwanzo ilikuwa imefikia hatua ya Usaili, hata walipokuja kamati ya uchaguzi ya TFF wakaanzia hatua hiyo badala ya kuanza moja.
Baada ya hilo wakakatwa waliokatwa zoezi likaendelea, kama inavyojulikana kwa siku za karibuni Katiba za vyama.vyotr vya soka nchini zilifanyiwa maboresho ambapo ili uchaguzi wa chama cha soka mkoa uweze kufanyika lazima Vyama vya wilaya vimalize uchaguzi wao ndipo wa mkoa ufuate kwakua wale wanaopiga kura kwenye uchaguzi wa mkoa wanatokana na wale waliochaguliwa kwenye wilaya.
KICHEKESHO ni kwamba Kuna maelekezo ya kumtaka Elias Mwanjala ambaye aliwahi kufungiwa na Baraza la michezo nchini BMT na kuzuiwa kugombea tena mkoani Mbeya kwa kosa la kusigina Katiba kwamba ndiye achaguliwe kuwa mwenyekiti wa chama cha soka hapa Mbeya.
Kibaya zaidi ni kwamba badala ya viongozi waliochaguliwa kwenye wilaya ndio watumike kwenye uchaguzi kwa sasa wamepanga njama ya kutumia wapiga kura ambao walishajiuzuru nafasi zao na kuwaacha viongozi wapya waliochaguliwa Kwa mujibu wa katiba mpya wilayani.
Kwa mantiki hiyo kwakua kuna dalili za kuubaka mpira wa Mbeya tunaomba wenye mamlaka kuliangalia hili. kwanini itumike nguvu kubwa kumpitisha Mwanjala na mbaya zaidi kila anapogombea Kuna kuwa na ukiukwaji wa katiba?
TFF kupitia kwa Mwenyekiti Kiomoni Kibamba fuateni utaratibu ili tupate viongozi waliobora kulikoni kubumba viongozi.
Kwanza inakuwaje viongozi wa wilaya ambao hawako madarakani waalikwe kupiga kura wakati viongozi halali wapo? Na barua za kufuta chaguzi zote za wilaya zilizofanyika iko wapi?
Na lini kamati tendaji ya Mrefa ilikaa na kupitisha maamuzi hayo ya kufuta Chaguzi za wilaya?
Tunajua TFF Haina mamlaka ya kufuta Chaguzi za wilaya sababu FA wilaya siyo wanachama wa TFF.
Katibu wa chama Cha mpira wa miguu Mbeya acha kutumika vibaya,sababu wewe ndiyo ulikuwa unaongozana na hiyo kamati mliyoiondoa Kwenye Chaguzi za wilaya.