Uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM Dodoma: Rais Samia achaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Taifa kwa kupata kura zote 1862 zilizopigwa

Sasa mlitegemea Nini? Sioni la breaking news hapa. No new news hapa
 
Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan, amempendekeza mabadiliko ndani ya Chama Cha Mapinduzi ya SEKRETARIETI CCM na kuridhiwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM katika kikao Maalumu kilichoketi Leo Mara baada ya Mkutano Mkuu wa Chama.

1. Mwenyekiti SAMIA Suluhu Hassan amependekezo yaliyotolewa na Mwenyekiti katika Sekretarieti Kuu CCM kuwa mhe.Daniel Chongolo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kuwa Katibu Mkuu wa CCM.
1619784247730.png

2. Mhe.Shaka Hamdu Shaka, kuwa Katibu wa NEC ya CCM Itikadi na Uenezi, akichukua nafasi ya mhe.Humphrey Polepole.

1619782165063.png

3. Mheshimiwa Maudline Cyrus Castico, amechukuwa nafasi ya Pereira Ame Silima, ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

1619782870035.png
 
Sisimu hawawezi kuweka mtu mstaarabu kwa kuwa wanataka mtu wa kuropoka ropoka na kutukana kuwakata maini upinzani style za kina nape na makonda, kibajaji angekuwa na elimu nzuri wangempa lazima, mzee wa kashfa.
Bora abaki tu polepole
 
Kwa mwenendo iliyokuwa inaenda nayo CHADEMA tulikionya kuwa kinajichimbia kaburi lake yenyewe!

TSON akaenda mbali kusema 2013 ndo mwisho wa CHADEMA (chenyewe kikajitahidi mpaka 2020)

Ikiwa ni kweli (tunarudia) ikiwa ni kweli, Naona kabisa chama dume kikianza kukusanya Majembe, sururu, Makoleo .... (maandalizi ya kuchimba kaburi)
Sema dictator Jpm ndo alitaka kukimaliza chadema kwa ubabe tu na siyo ushawishi. Uchaguzi ungekuwa huru na wa haki ccm wangerudi wachache bungeni. Mfano kawe, Kilimanjaro yote, tarime vijijini na mjini, mikumi n.k chadema ilishinda ila dictator akaamlisha wakurugenzi watangaze ushindi kwa ccm Mana alijua watanzania ni wavivu wa kudai haki kwa maandamano.

Ki ujumla upinzani upo strong ila kosa lilikuwa kuwa na dictator ndani ya nchi yetu aliyeamini kumwaga ndamu tu eti ndo maendeleo
 
Kijiti cha uenyekiti kukabidhiwa rasmi leo.

Chama cha Mapinduzi(CCM) kinafanya Mkutano Mkuu Maalumwa kumchagua Mwenyekiti wake wa taifa jijini Dodoma katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Makao Makuu ya Chama.

Wajumbe wengi wapo ukumbini

Updates:

Rais Samia apata kura zote 1862, 100%

Rais Samia Suluhu Hassan ameibuka kuwa Mwenyekiti wa chama hicho kwa asilimia 100, Kura zilizopigwa ni 1862 na kura zote ni za ndio hakuna kura ya hapana.

‘Asanteni sana wana CCM wenzangu kwa kunichagua mimi kuwa mwenyekiti wa chama chetu najua jukumu mlilonipa ni kubwa lakini naamini nitaweza, naamini nitaweza kwanza chama chetu kinaongozwa na katiba na kanuni, kazi hii si yangu pekee yangu bali ni yetu sote’

Idadi ya wajumbe yapungua kutoka 1,909 hadi 1,876
Naibu katibu mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo amesema wajumbe wanaotakiwa kuhudhuria mkutano mkuu wa chama hicho ni 1,909 lakini waliowasili katika ukumbi wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma ni 1,862.

Amesema idadi wa wajumbe imepungua kutoka 1,909 hadi 1,876 na kwamba watu 33 hawajafika kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo vifo na kwamba waliohudhuria ndio watakaopiga kura.

Amesema CCM imekuja na kauli mbiu ya ‘chama imara, Serikali madhubuti, kazi inaendelea’

e4fca260-2b42-4c09-ba9e-bc7c413366f1.jpg

800df0d5-9c49-4a6a-9db5-99d69f059467.jpg

9a3eb121-dc7c-4342-89c4-55b25d32d2ea.jpg

702b7da2-5cdf-49d7-843b-a5cb10bd7eca.jpg

ff0697c0-22ed-4d17-b031-83faf2938afe.jpg

be96a98c-f3be-46d7-b26f-263038760306.jpg

302f351b-4041-4f9f-988a-2c71e4a77e3c.jpg

d489adaa-9648-4158-926c-849216ed5ba4.jpg

5a82cd1f-61cf-490a-9c42-f4892a0cad86.jpg
 
Kijiti cha uenyekiti kukabidhiwa rasmi leo.

Chama cha Mapinduzi(CCM) kinafanya Mkutano Mkuu Maalumwa kumchagua Mwenyekiti wake wa taifa jijini Dodoma katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Makao Makuu ya Chama.

Wajumbe wengi wapo ukumbini

Updates:

Rais Samia apata kura zote 1862, 100%

Rais Samia Suluhu Hassan ameibuka kuwa Mwenyekiti wa chama hicho kwa asilimia 100, Kura zilizopigwa ni 1862 na kura zote ni za ndio hakuna kura ya hapana.

‘Asanteni sana wana CCM wenzangu kwa kunichagua mimi kuwa mwenyekiti wa chama chetu najua jukumu mlilonipa ni kubwa lakini naamini nitaweza, naamini nitaweza kwanza chama chetu kinaongozwa na katiba na kanuni, kazi hii si yangu pekee yangu bali ni yetu sote’

Idadi ya wajumbe yapungua kutoka 1,909 hadi 1,876
Naibu katibu mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo amesema wajumbe wanaotakiwa kuhudhuria mkutano mkuu wa chama hicho ni 1,909 lakini waliowasili katika ukumbi wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma ni 1,862.

Amesema idadi wa wajumbe imepungua kutoka 1,909 hadi 1,876 na kwamba watu 33 hawajafika kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo vifo na kwamba waliohudhuria ndio watakaopiga kura.

Amesema CCM imekuja na kauli mbiu ya ‘chama imara, Serikali madhubuti, kazi inaendelea’

1308a27d-345a-447e-8348-1a93494ce0a5.jpg

9ae04948-34a9-403b-966b-db9c1bb1da83.jpg

b455dc63-d376-4fb7-8411-4fe2fed309b3.jpg

63834c9c-b37f-43c6-a925-2ab5f41eeb9b.jpg

9f822df9-123c-4aa5-b770-ac872a9e0c9e.jpg

06fe40c7-e3d6-4e2a-866b-a86f0dbca955.jpg

72c32b22-1b76-4c09-99d0-9c31cbf7216c.jpg
 
Pamoja na 100% ya kura lakini wapo CCM ambao wameumia sana kwenye hiyo hiyo asilimia 100% mama kuwa Mwenyekiti
 
Tumeshuhudia CCM ikiwahadaa wanachama kwa kupoteza mda kuandaa uchaguzi wa nafasi ya mwenyekiti huku wakijua Mgombea ni mmoja. Hii inamaana gani? Je kama katiba ya chama inasema hivi,tutegemee walioshindwa kutunga katiba bora ya chama kuja kuleta katiba nzuri ya Tanzania? Yaani wanaendelea na uleule upumbavu wa Kuchagua kati ya Kivuli na Picha ya Nyerere enzi za TANU. Hivi hawawezi kuweka hata mgombea mmoja japo ashindwe lakini kuonesha Rais hakuwa Mgombea peke yake? Vizazi vijavyo vitashangaa huu upumbavu wa CCM ndani ya Chama chao.

EWE MTANZANIA MZALENDO SHIRIKI KATIKA KUWEKA SHINIKIZO KWA WATAWALA ILI KUPATA KATIBA MPYA ILIYOBORA KWA MANUFAA YA VIZAZI VIJAVYO.
 
Mimi nitafurahia tu siku ccm ikifa kifo cha mende. Kuhusu hayo maigizo yao, binafsi hayanihusu kabisa.
 
Kijiti cha uenyekiti kukabidhiwa rasmi leo.

Chama cha Mapinduzi(CCM) kinafanya Mkutano Mkuu Maalumwa kumchagua Mwenyekiti wake wa taifa jijini Dodoma katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Makao Makuu ya Chama.

Wajumbe wengi wapo ukumbini

Updates:

Rais Samia apata kura zote 1862 (100%)

Rais Samia Suluhu amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kura zote 1862 za ndio za Mkutano Mkuu Maalum sawa na asilimia 100

Rais Samia: Asanteni sana wana CCM wenzangu kwa kunichagua mimi kuwa mwenyekiti wa chama chetu najua jukumu mlilonipa ni kubwa lakini naamini nitaweza, naamini nitaweza kwanza chama chetu kinaongozwa na katiba na kanuni, kazi hii si yangu pekee yangu bali ni yetu sote.

Rais Samia: Nafahamu kuwa nachukua jukumu la kukiongoza Chama hiki (CCM) kikiwa kina baadhi ya changamoto ikiwemo uhaba wa vitendea kazi, kuna baadhi ya Mikoa na Wilaya Viongozi hawana usafiri, changamoto nyingine ni maslahi duni kwa Watumishi wa Chama.

Rais Samia: Nafahamu kuwa kuna malimbikizo ya madai ya stahiki zikiwemo za uhamisho na kustaafu, nawaahidi nitashirikiana na nyinyi kuzitatua changamoto zilizopo kwenye CCM nilizozitaja na ambazo sijazitaja.

Idadi ya wajumbe yapungua kutoka 1,909 hadi 1,876
Naibu katibu mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo amesema wajumbe wanaotakiwa kuhudhuria mkutano mkuu wa chama hicho ni 1,909 lakini waliowasili katika ukumbi wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma ni 1,862.

Amesema idadi wa wajumbe imepungua kutoka 1,909 hadi 1,876 na kwamba watu 33 hawajafika kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo vifo na kwamba waliohudhuria ndio watakaopiga kura.

Amesema CCM imekuja na kauli mbiu ya ‘chama imara, Serikali madhubuti, kazi inaendelea’

Lazaro Nyalandu arejea Chama cha Mapinduzi (CCM)
Lazaro Nyalandu ametangaza rasmi kurejea CCM mbele ya Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Samia Suluhu kupitia Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Dodoma leo akitokea CHADEMA, Nyalandu alitangaza kujiondoa CCM mwaka 2017.

Nyalandu: Kupitia Mkutano huu Maalum wa CCM naomba kukushukuru Mwenyekiti (Rais Samia) kwa kukubali Kunipokea, kunisamehe na kuniruhusu kurejea nyumbani (CCM), hakuna furaha inayozidi furaha ya Mtoto arejeapo nyumbani

Nyalandu: Katika Nchi ya ugenini wimbo hauimbiki, Mzee Lowasa, Mzee Sumaye, Mzee Slaa hawa ni Mashuhuda wachache kati ya wengi wa kwanini wimbo wa Bwana hauimbiki katika Nchi ya ugenini

Nyalandu: Watanzania wameiona nyota yako Rais Samia, wameguswa kwa kuinuliwa kwako kwakuwa Mungu alikuandaa kuwa Kiongozi wa Taifa hili, Mungu akuongoze katika safari, uwepo wangu kwenye Mkutano huu ni kielelezo tosha cha wewe kuungwa mkono na Watanzania wote

Nyalandu: Kazi iendelee, Rais wetu (Samia Suluhu), Mama yetu, Mwenyekiti wa Chama chetu (CCM), Mama tuma neno lako likaponye wote walioumia, ukaitwe heri na shujaa wa mioyo ya Watanzania, ukaongeze Tabasamu katika nyuso za Watanzania wote

Uteuzi wa viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM);
1. Katibu Mkuu- Daniel Chongolo
2. Naibu Katibu Mkuu (Bara)- Christina Mndeme
3. Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi- Shaka Hamdu Shaka

72c32b22-1b76-4c09-99d0-9c31cbf7216c.jpg

06fe40c7-e3d6-4e2a-866b-a86f0dbca955.jpg

9f822df9-123c-4aa5-b770-ac872a9e0c9e.jpg

63834c9c-b37f-43c6-a925-2ab5f41eeb9b.jpg

b455dc63-d376-4fb7-8411-4fe2fed309b3.jpg

9ae04948-34a9-403b-966b-db9c1bb1da83.jpg

1308a27d-345a-447e-8348-1a93494ce0a5.jpg
 
Tumeshuhudia CCM ikiwahadaa wanachama kwa kupoteza mda kuandaa uchaguzi wa nafasi ya mwenyekiti huku wakijua Mgombea ni mmoja. Hii inamaana gani? Je kama katiba ya chama inasema hivi,tutegemee walioshindwa kutunga katiba bora ya chama kuja kuleta katiba nzuri ya Tanzania? Yaani wanaendelea na uleule upumbavu wa Kuchagua kati ya Kivuli na Picha ya Nyerere enzi za TANU. Hivi hawawezi kuweka hata mgombea mmoja japo ashindwe lakini kuonesha Rais hakuwa Mgombea peke yake? Vizazi vijavyo vitashangaa huu upumbavu wa CCM ndani ya Chama chao.

EWE MTANZANIA MZALENDO SHIRIKI KATIKA KUWEKA SHINIKIZO KWA WATAWALA ILI KUPATA KATIBA MPYA ILIYOBORA KWA MANUFAA YA VIZAZI VIJAVYO.
Tuna kazi kubwa ya kuvunja mfumo ccm, ni hatari sana kwa maendeleo yetu.
 
Poa
Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan, amempendekeza mabadiliko ndani ya Chama Cha Mapinduzi ya SEKRETARIETI CCM na kuridhiwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM katika kikao Maalumu kilichoketi Leo Mara baada ya Mkutano Mkuu wa Chama.

1. Mwenyekiti SAMIA Suluhu Hassan amependekezo yaliyotolewa na Mwenyekiti katika Sekretarieti Kuu CCM kuwa mhe.Daniel Chongolo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kuwa Katibu Mkuu wa CCM.View attachment 1769123

2. Mhe.Shaka Hamdu Shaka, kuwa Katibu wa NEC ya CCM Itikadi na Uenezi, akichukua nafasi ya mhe.Humphrey Polepole.

View attachment 1769049

3. Mheshimiwa Maudline Cyrus Castico, amechukuwa nafasi ya Pereira Ame Silima, ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

View attachment 1769056

Poa,ahsante kwa taarifa.
 
Back
Top Bottom