Uchaguzi wa Papa ni wa kiimani, siyo uchaguzi kama tulivyozoea

Uchaguzi wa Papa ni wa kiimani, siyo uchaguzi kama tulivyozoea

Kama ndivyo then why kuwe na rumours kuhusu yule jamaa wa ghana?
Wapo ambao wanatazamwa na wengi, mfano yule Cardinal wa Philipines. Hao ndiyo hupigiwa kura kwa sababu ubora wao mara nyingi huonekana na hutambulika ila mpaka wafikishe 2/3 ya kura zote.
 
Kama Papa anateuliwa na mungu wenu kama ulivyomalizia hapo chini basi mungu wenu ni mbaguzi wa rangi
 
Mbona sijaona chochote cha ajabu cha kuutofautisha huu uchaguzi na chaguzi zingine? Mwisho wa siku papa anapatikana kwa kupigiwa KURA kati ya makadinali wanaofahamika "wagombea".

Mi nilidhani labda jina linashushwa kutoka mbinguni..

Ndugu yangu, kama umejengeka katika imani, utakuwa unafahamu kuwa Mungu hutenda kazi zake kuputia mikono ya wanadamu. Siyo kwa hiyo namna unaifikiria.

Waliokolewa na mafuriko, ilikuwa kwa mkono wa Nubu.

Wayahudi waliokolewa kutoka utumwani Misri kwa mkono wa Musa.

NA miujiza yote Yesu masiha aliitenda akiwa ameubeba mwili wa kibinadamu.

Miujiza mingi ilifanyika kwa mikono ya mitume.

Mwanadamu huumbwa na Mungu kuoitia mume na mke.

Goliath aliuawa na Mungu kwa kulitia mkono wa Daud.

NB. Ukisikia kitu hiki kimedondoshwa na Mungu moja kwa moja, weka alama ya kuuliza. Maana huo siyo utendaji kazi wa Mungu.
 
Wengi wakisikia uchaguzi wa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki, wanadhani ni uchaguzi kama hizi chaguzi tunaazozifanya kuwachagua viongozi wa kijamii.

Mchakato wa Uchaguzi wa kumpata Papa, ni mrefu na mgumu kwa sababu umejengwa kwa msingi wa kiimani kuliko werevu wa kibinadamu. Mambo muhimu yanayoonesha utofauti mkubwa wa uchaguzi wa Papa na Chaguzi nyingine za kawaida:

1. Hairuhusiwi kupiga kampeni yoyote ile.

2. Hakuna majina ya wagombea, iwe ni wao wenyewe kwa kutaka au kupendekezwa.

3. Uchaguzi kura hupigwa mara 2 kwa siku, asubuhi na mchana, kwa kutumia maboksi mawili tofauti.

4. Kila kadinali anatakiwa kuandika jina la mtu anayemfikiria anafaa kuwa kiongozi mkuu wa kanisa, bila ya yeye kujadiliana na mtu mwingine yeyote. Mtu huyo anayestahili kuwa Papa anaweza kuwa miongoni mwa makadinali au hata asiye kadinali alimradi ana daraja la uaskofu.

4. Kila zoezi linapokamilika, kura huhesabiwa, na anayekuwa amependekezwa na makadinali wengi, lazima iwe kuanzia theluthi 2 kwenda juu , ndiye anayetangazwa kuwa Papa.

5. Kama hatapatikana aliyepata theluthi 2 kwenda juu, zoezi hurudiwa kwa siku 3 mfululizo.

6. Kama hata baada ya siku 3, hakuna aliyepata kura kuanzia kura theluthi 2 kwenda juu, waumini wanatengaziwa kuwa papa hajapatikana, bila hata ya kusomewa matokeo, kujua nani wamepigiwa kura na wamepata kura ngapi kila mmoja.

7. Kama Papa hakupatikana baada ya siku 3 mfululizo za kupiga kura, uchaguzi husimamishwa, na makadinali huingia katika maombi maalum. Kisha zoezi hurudiwa.

A. Wakati wote, makadinali wanapoingia kwenye maombi na wakati upigaji kura unaendelea, wakristo wengi huwa nje, nao wakifunga na kuomba ili Mungu amteue kiongozi wake mkuu wa Kanisa la hapa Duniani, kupitia kura zinazopigwa na makadinali.

NB: Historia inaonesha kuwa kuna wakati baada ya kupita miezi 6 bila ya kupatikana papa, waumini waliokuwa nje wakiomba na kufunga, huku kipindi cha baridi kikiwa kimeingia, walikasirika na kwenda kuvunja paa la jengo ambalo makadinali walikuwa wamejifungia. Waumini hao walidai kuwa makadinali walikosa imani ndiyo maana papa ameshindwa kupatikana. Makadinali wakapigwa na baridi kali, baada ya siku chache, Papa alipatikana.

Mpaka sasa, rekodi inayoonesha papa alipatikana kwa taabu sana, baada ya miaka mitatu, ni wa mwaka 1268, kufuatia kifo cha Papa Clement wa 4. Sababu zinazotajwa ni kwamba kulikuwepo makadinali waliotaka kutumia mbinu za kisiasa kuipata nafasi hiyo.

Kati ya mapapa wanaotajwa kupatikama kwa urahisi kabisa, ni Papa John Paulo wa pili, ambaye mzunguko wa kwanza tu, tayari kura zilitimia, na mchakato ukawa umekamilika.

Waumini wakatoliki na wasio wakatoliki, tumwombe Mungu amteue mtumishi afaaye kwa nafasi hiyo ya juu kabisa ya taasisi mojawapo kubwa kabisa ya kidini, yenye nafasi ya kugusa maisha ya watu wengi bila ya kujali imani zao
Kushiriki kuomba Mungu apatikane kiongozi ili aendeleze upagani wa kupotosha Injili ni dhihaka kwa Mungu. Binafsi sishiriki maombi hayo batili
 
Mwanadamu yeyote hana uwezo wa kufanya miujiza. Miujiza hufanywa ama na Mungu ama shetani. Ukisikia mtumishi wa Mungu anasema kuwa yeye anafanya miujiza, ujue ni tapeli. Lakini Mungu, kwa gekima yake anaweza kufanya miujiza kwa kupitia mikono ya wanadamu. Hata shetani anaweza kufanya miujiza kwa kuputia mikono ya wanadamu.

Hata mitume, japo walifanya miujiza, lakini haikuwa wakati wote, bali ni wakati maalum, kwa kutegemea hekima yake.

Wapo mapapa ambao kwa mikono yao, miujiza ilifanyika, lakini siyo wakati wote. Hata huyu Papa Francus, kwa mkono wake, mara kadhaa miujiza ilitendeka:

Pope Francis may yet earn the accolade "The Healing Pope" for the miracles he has been performing when touching people with serious health problems.

When the Pope flew to New York last week as part of his six-day apostolic visit to the United States, he once again showed his healing power when he blessed a 12-year-old girl who was one of those who greeted him at JFK Airport, The Gospel Herald said.

Julia Bruzzese of Brooklyn, New York was in a wheelchair when the smiling Pope stopped by, touched her face and blessed her. She had been using the wheelchair ever since she suffered a sudden paralysis whose cause puzzled her doctors no end.

Her doctors said she seemed to exhibit symptoms of Lyme disease. But the problem was that her blood tests showed she was negative for that disease.

Tofauti kubwa ya wakatoliki na makanisa ya kiroho, hawajatanguliza miujiza kama msingi wa imani. Hivyo miujiza ya uponyaji hawaitangazi sana kwa sababu kuitangaza sana na kuihusisha na mtu fulani, inakuwa ni kutaka kupokonya utukufu, ukuu na sifa ya Mungu, ambaye ndiye hasa mponyaji.
Acha vituko leta vifungu vya biblia😁 Yesu aliponya na alituambia watakuja nyumayake wataotenda miujiza zaidi yake Yohana 14:12!! Sote tunajua miujiza/uponyaji CHANZO ni Mungu.
Tatizo wazungu wamekushikeni akili hamuwezi kuchambua neno mnasikiliza wanachotaka kuwaambia. Mnaambiwa msiabudu sanamu hamsikii bado mnabusu sanamu ya kizungu Hii sisawa kabisa.
Biblia imeandika Yesu alivyoponya na yeye kutufundisha tuwe na Imani tutafanya kama au zaidi yake. Leo unasema haifai kuonesha matendo ya miujiza afanyayo Mwenyezi Mungu what is that?
 
Acha kufuru! Au unamaanisha ni imani kwa ule upande wa pili? Yaani imani iliyomwegemea ibilisi
Hapo kufuru iko wapi?
Hakuna sehemu isiyo na siasa
Mnajuaje kama hawaongei
Unafikiri makadinari hawajui mtizamo wa kila mmoja kwenye masuala ya jumla
 
Papa ni kiongozi wa Kiroho, unasemaje ni c
Cheo cha kiroho kipoje?

heo cha kijamii?

Kwasababu RC ni taasisi ya KIJAMII inayoendeshwa na JAMII (WATU)...
Kura wanapiga binadamu kulingana na matakwa ya nafsi zao..
Roho ni mahusiano binafsi kati ya Binadamu na Mungu na hayana UWINGI wala UMOJA,,, kwenye ROHO hakuna WENGI wape bali KIKAMILIFU ndo kipite na tena hakuna wakala wala dalali...

Kama hawa wazee wangekuwa ni wa Kiroho mngeacha Roho ziamue?...
 
Wapo ambao wanatazamwa na wengi, mfano yule Cardinal wa Philipines. Hao ndiyo hupigiwa kura kwa sababu ubora wao mara nyingi huonekana na hutambulika ila mpaka wafikishe 2/3 ya kura zote.
aaah kumbe. Ahsante kwa kunijuza
 
Kwasababu RC ni taasisi ya KIJAMII inayoendeshwa na JAMII (WATU)...
Kura wanapiga binadamu kulingana na matakwa ya nafsi zao..
Roho ni mahusiano binafsi kati ya Binadamu na Mungu na hayana UWINGI wala UMOJA,,, kwenye ROHO hakuna WENGI wape bali KIKAMILIFU ndo kipite na tena hakuna wakala wala dalali...

Kama hawa wazee wangekuwa ni wa Kiroho mngeacha Roho ziamue?...
Sijui kama unaelewa unachokiandika. RC ni Kanisa la Kristu sio taasisi ya kijamii, Ni kanisa na mwili wa Kristu. Inawezekana linamiliki taasisi kadhaa lakini Kanisa litabaki kuwa kanisa na Mwili wa Kristu. Pili Unaposema Roho ni mahusiano kati yetu na Mungu bila shaka unamaanisha yetu sisi (Kimwili, Kijamii, na yale yote yanayotuzunguka aliyoyaumba Mungu) Kiroho, Kimwili na Nafsi. Hivyo yale yote yanayotendeka Rohoni yanaonekana Katika ulimwengu wa Mwili. Hivyo Katika Roho Mungu alipomwita Daudi kuwa Mfalme au alipoinua baadhi ya wafalme, hakuja na kutanga kwa watu kwamba fulani ni Mfalme, Bali aliruhusu mchakato, na katika mchakato huo ndipo alipatikana yule aliyemchagua. Hivyo Mchakato Mzima wa kumpata mrithi wa Kiti cha Mtume Petro ni wa Kiroho na yule anayechaguliwa iwe kwa namna yeyote ile yote yapo katika Mpango wa Mungu kwa kanisa lake. Mungu humpitisha yule mkamilifu kwa njia hiyo ya kura, Roho Mtakatifu ndiye anaamua kupitia watumishi wake .
 
Thibitisha roho na kiroho
 
Imani haliwezi chagua mtu mweusi? Mnamkosea Mungu sana, matapeli, Nyie ndo mnafanya wakristo tuonekane wa hovyo
 
Unaposema mchakato ni wa kiroho unamaanisha nini wakati wanaopiga kura ni watu?
 
Acha vituko leta vifungu vya biblia😁 Yesu aliponya na alituambia watakuja nyumayake wataotenda miujiza zaidi yake Yohana 14:12!! Sote tunajua miujiza/uponyaji CHANZO ni Mungu.
Tatizo wazungu wamekushikeni akili hamuwezi kuchambua neno mnasikiliza wanachotaka kuwaambia. Mnaambiwa msiabudu sanamu hamsikii bado mnabusu sanamu ya kizungu Hii sisawa kabisa.
Biblia imeandika Yesu alivyoponya na yeye kutufundisha tuwe na Imani tutafanya kama au zaidi yake. Leo unasema haifai kuonesha matendo ya miujiza afanyayo Mwenyezi Mungu what is that?

Wewe huna uelewa wowote. Utabakia kuwa mjinga wa neno la Mungu kama hujibidishi. Kwa sababu u aisoma biblia kama kitabu cha hadithi. Huelewi hata maana ya sanamu!

Mikuulize swali dogo, kwa vile beno hilo sanamu limetafsiriwa kutoka biblia ya kale zaidi ya Kigiriki, hilo neno 'sanamu', kwa kigiriki, lilitumika neno gani? Na maana yake halisi ni nini? Je, kwa uelewa wako, sanamu ni nini? Je, sanduku la Agano la kale unaweza kuliita ni sanamu? Je, msalaba wa Yesu unaweza kuuita ni sanamu? Je, zile mbao 2 za amri za Mungu, zina sifa ya kuitwa sanamu? Na vipi yule nyoka wa shaba, anaweza kuitwa sanamu?
 
Imani haliwezi chagua mtu mweusi? Mnamkosea Mungu sana, matapeli, Nyie ndo mnafanya wakristo tuonekane wa hovyo
Usiwe unaandika vitu vya kipuuzi kwenye jambo ambalo huna uhakika nalo.

Wapo watu weusi ambao waliwahi kuwa mapapa. Lakini ujue kuwa hakuna mhindi au mchina amewahi kuwa Papa! Miongoni mwa mitume wa Yesu, aliwahi kuwepo mzungu, mhindi, mchina au mwafrika? Kwa sababu hawakuwepo, basi ina maana wote wamebaguliwa?
 
Back
Top Bottom