Uchaguzi wa Papa ni wa kiimani, siyo uchaguzi kama tulivyozoea

Uchaguzi wa Papa ni wa kiimani, siyo uchaguzi kama tulivyozoea

Nguvu ya muujiza haipatikani kwa kila mtu mkuu, nikarama ambayo mtu amepewa,
Ooh imeandikwa wapi hiyo mkuu? Maana Yesu alisema mkiwa na Imani mtahamisha milima Wala hakusema baadhi ya wenyeimani....
Kiongozi mkuu wa kiimani lazima aoneshe Imani inavyotenda makuu ili wasiyonayo wawenayo!!
 
Wewe huna uelewa wowote. Utabakia kuwa mjinga wa neno la Mungu kama hujibidishi. Kwa sababu u aisoma biblia kama kitabu cha hadithi. Huelewi hata maana ya sanamu!

Mikuulize swali dogo, kwa vile beno hilo sanamu limetafsiriwa kutoka biblia ya kale zaidi ya Kigiriki, hilo neno 'sanamu', kwa kigiriki, lilitumika neno gani? Na maana yake halisi ni nini? Je, kwa uelewa wako, sanamu ni nini? Je, sanduku la Agano la kale unaweza kuliita ni sanamu? Je, msalaba wa Yesu unaweza kuuita ni sanamu? Je, zile mbao 2 za amri za Mungu, zina sifa ya kuitwa sanamu? Na vipi yule nyoka wa shaba, anaweza kuitwa sanamu?
KUTOKA 20:4-6 Usiwe mbumbumbu wa neno hujui hata amri kumi yet unajidai uko deep.
Mnabusu sanamu la mzungu mnaomwita Yesu nahiyo ni makosa.
Unabishana hurejei kitabu chochote unaleta stories unazoadithiwa tuu kigangoni.
Soma neno bwamdogo! Usishikiwe akili na wazungu
 
Makadinari sio malaika ni binadamu nakuambia hivi figisu zipo na wanapiga kampeni hata chini kwa chini.
 
Wengi wakisikia uchaguzi wa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki, wanadhani ni uchaguzi kama hizi chaguzi tunaazozifanya kuwachagua viongozi wa kijamii.

Mchakato wa Uchaguzi wa kumpata Papa, ni mrefu na mgumu kwa sababu umejengwa kwa msingi wa kiimani kuliko werevu wa kibinadamu. Mambo muhimu yanayoonesha utofauti mkubwa wa uchaguzi wa Papa na Chaguzi nyingine za kawaida:

1. Hairuhusiwi kupiga kampeni yoyote ile.

2. Hakuna majina ya wagombea, iwe ni wao wenyewe kwa kutaka au kupendekezwa.

3. Uchaguzi kura hupigwa mara 2 kwa siku, asubuhi na mchana, kwa kutumia maboksi mawili tofauti.

4. Kila kadinali anatakiwa kuandika jina la mtu anayemfikiria anafaa kuwa kiongozi mkuu wa kanisa, bila ya yeye kujadiliana na mtu mwingine yeyote. Mtu huyo anayestahili kuwa Papa anaweza kuwa miongoni mwa makadinali au hata asiye kadinali alimradi ana daraja la uaskofu.

4. Kila zoezi linapokamilika, kura huhesabiwa, na anayekuwa amependekezwa na makadinali wengi, lazima iwe kuanzia theluthi 2 kwenda juu , ndiye anayetangazwa kuwa Papa.

5. Kama hatapatikana aliyepata theluthi 2 kwenda juu, zoezi hurudiwa kwa siku 3 mfululizo.

6. Kama hata baada ya siku 3, hakuna aliyepata kura kuanzia kura theluthi 2 kwenda juu, waumini wanatengaziwa kuwa papa hajapatikana, bila hata ya kusomewa matokeo, kujua nani wamepigiwa kura na wamepata kura ngapi kila mmoja.

7. Kama Papa hakupatikana baada ya siku 3 mfululizo za kupiga kura, uchaguzi husimamishwa, na makadinali huingia katika maombi maalum. Kisha zoezi hurudiwa.

A. Wakati wote, makadinali wanapoingia kwenye maombi na wakati upigaji kura unaendelea, wakristo wengi huwa nje, nao wakifunga na kuomba ili Mungu amteue kiongozi wake mkuu wa Kanisa la hapa Duniani, kupitia kura zinazopigwa na makadinali.

NB: Historia inaonesha kuwa kuna wakati baada ya kupita miezi 6 bila ya kupatikana papa, waumini waliokuwa nje wakiomba na kufunga, huku kipindi cha baridi kikiwa kimeingia, walikasirika na kwenda kuvunja paa la jengo ambalo makadinali walikuwa wamejifungia. Waumini hao walidai kuwa makadinali walikosa imani ndiyo maana papa ameshindwa kupatikana. Makadinali wakapigwa na baridi kali, baada ya siku chache, Papa alipatikana.

Mpaka sasa, rekodi inayoonesha papa alipatikana kwa taabu sana, baada ya miaka mitatu, ni wa mwaka 1268, kufuatia kifo cha Papa Clement wa 4. Sababu zinazotajwa ni kwamba kulikuwepo makadinali waliotaka kutumia mbinu za kisiasa kuipata nafasi hiyo.

Kati ya mapapa wanaotajwa kupatikama kwa urahisi kabisa, ni Papa John Paulo wa pili, ambaye mzunguko wa kwanza tu, tayari kura zilitimia, na mchakato ukawa umekamilika.

Waumini wakatoliki na wasio wakatoliki, tumwombe Mungu amteue mtumishi afaaye kwa nafasi hiyo ya juu kabisa ya taasisi mojawapo kubwa kabisa ya kidini, yenye nafasi ya kugusa maisha ya watu wengi bila ya kujali imani zao
Kwa mchakato huu, ni wazi kwamba papa anapatikana kwa maamuzi ya mungu mwenyewe kwa kuwafunulia makadinali wa kanisa mtu ambae mungu anamtaka.

Kama utaratibu huu ndio huo huo uliotumika kumpata papa wa sasa aliefariki ambapo mungu aliwapa maono makadinali wamchague yeye aje kutangaza ndoa za mashoga kanisani?

Kwa maana nyingine ni kwamba mungu ndio ameruhusu kupitia Papa Francis ndoa za mashoga zifungishwe kanisani na zipate baraka zake mungu mwenyewe.

Dini hupumbaza sana watu.
 
Back
Top Bottom