- Thread starter
- #41
Hizo Roho na Kiroho kuhusiana na ishu ya Papa au hiyo Roho na Kiroho kama vitu vilivyopo katika maisha ya binadamu?
Dini ni imani. Na imani unaweza kuiamini au kutoiamini.
Wewe kama huamini, tulia tu, haikuhusu.
Hizo Roho na Kiroho kuhusiana na ishu ya Papa au hiyo Roho na Kiroho kama vitu vilivyopo katika maisha ya binadamu?
Hakuna papa anaechaguliwa na mungu. Papa anapigiwa kura na makadinali ambao wote ni watu.
Kwanini ni wabaguzi wa rangi?Hakuna papa anaechaguliwa na mungu. Papa anapigiwa kura na makadinali ambao wote ni watu.
Wala hakuna wa kukushikia bunduki kwamba lazima ushiriki kuomba,waache watakaoshiriki washiriki kisha wewe baki na imani yako unayoiona bora sana.Kushiriki kuomba Mungu apatikane kiongozi ili aendeleze upagani wa kupotosha Injili ni dhihaka kwa Mungu. Binafsi sishiriki maombi hayo batili
Kinachofanyika kwenye kumchagua papa, ni hicho nilicho bold hapo. Hayo mengine ni porojo tuu manake hata yasipokuepo bado papa atapatikana tu.Papa anapigiwa kura na wanadamu KWA IMANI ya maongozi ya Mungu. Imani haithibitishwi kisayansi.
😀😀 wewe ndo Emporer Constantine?Dini ni imani. Na imani unaweza kuiamini au kutoiamini.
Wewe kama huamini, tulia tu, haikuhusu.
Hata uchaguzi wa ccn ni wa kiimanimwijaku
Mwijaku msemaji wa mamaHata uchaguzi wa ccn ni wa kiimani
Unaposema ubatizo kiroho una maana gani wakati anayekumwagia maji ya ubatizo ni kasisi? Unaposema kuokoka ni nchakato wa kiroho una maana gani wakati anayekuombea ni mchungaji/mtu? Roho Mtakatifu anafanya kazi kupitia watu wake.Unaposema mchakato ni wa kiroho unamaanisha nini wakati wanaopiga kura ni watu?
Sasa unaniuliza mimi tena?Unaposema ubatizo kiroho una maana gani wakati anayekumwagia maji ya ubatizo ni kasisi? Unaposema kuokoka ni nchakato wa kiroho una maana gani wakati anayekuombea ni mchungaji/mtu? Roho Mtakatifu anafanya kazi kupitia watu wake.
Papa haigizi kama hao wanaouza maji na udongoHivi papa huwa hawafanyi miujiza na ishara zozote zaroho mtakatifu? Binafsi sijawahi ona hata kamtoa mtu mapepo,au kamgusa Mgonjwa akapona!nk. Mbona Inakuaga anashangiliwa tuuu
Ni Mchakato wa Kiroho unaohusisha Roho Mtakatifu anayechagua kupitia kura zinazopigwa na Makardinali wanaoongozwa na Roho Mtakatifu.Sasa unaniuliza mimi tena?
Wewe una uhakika gani kwamba hao makadinali wanaongozwa na roho mtakatifu? Na kama roho mtakatifu ndio anachagua, hao makadinali wao kazi yao ni nini? Je, bila makadinali kupiga kura papa atapatikana?Ni Mchakato wa Kiroho unaohusisha Roho Mtakatifu anayechagua kupitia kura zinazopigwa na Makardinali wanaoongozwa na Roho Mtakatifu.
Kabisa!Wala hakuna wa kukushikia bunduki kwamba lazima ushiriki kuomba,waache watakaoshiriki washiriki kisha wewe baki na imani yako unayoiona bora sana.
Nguvu ya muujiza haipatikani kwa kila mtu mkuu, nikarama ambayo mtu amepewa,Hivi papa huwa hawafanyi miujiza na ishara zozote zaroho mtakatifu? Binafsi sijawahi ona hata kamtoa mtu mapepo,au kamgusa Mgonjwa akapona!nk. Mbona Inakuaga anashangiliwa tuuu
Mbona Mungu alidondosha mana na nyama kule jangwani bila kupitia mkono wa musa ama mwanadamu yeyote yule?!!!Ndugu yangu, kama umejengeka katika imani, utakuwa unafahamu kuwa Mungu hutenda kazi zake kuputia mikono ya wanadamu. Siyo kwa hiyo namna unaifikiria.
Waliokolewa na mafuriko, ilikuwa kwa mkono wa Nubu.
Wayahudi waliokolewa kutoka utumwani Misri kwa mkono wa Musa.
NA miujiza yote Yesu masiha aliitenda akiwa ameubeba mwili wa kibinadamu.
Miujiza mingi ilifanyika kwa mikono ya mitume.
Mwanadamu huumbwa na Mungu kuoitia mume na mke.
Goliath aliuawa na Mungu kwa kulitia mkono wa Daud.
NB. Ukisikia kitu hiki kimedondoshwa na Mungu moja kwa moja, weka alama ya kuuliza. Maana huo siyo utendaji kazi wa Mungu.
Janja janja uchaguzi ni ule ule kama wa ccmWengi wakisikia uchaguzi wa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki, wanadhani ni uchaguzi kama hizi chaguzi tunaazozifanya kuwachagua viongozi wa kijamii.
Mchakato wa Uchaguzi wa kumpata Papa, ni mrefu na mgumu kwa sababu umejengwa kwa msingi wa kiimani kuliko werevu wa kibinadamu. Mambo muhimu yanayoonesha utofauti mkubwa wa uchaguzi wa Papa na Chaguzi nyingine za kawaida:
1. Hairuhusiwi kupiga kampeni yoyote ile.
2. Hakuna majina ya wagombea, iwe ni wao wenyewe kwa kutaka au kupendekezwa.
3. Uchaguzi kura hupigwa mara 2 kwa siku, asubuhi na mchana, kwa kutumia maboksi mawili tofauti.
4. Kila kadinali anatakiwa kuandika jina la mtu anayemfikiria anafaa kuwa kiongozi mkuu wa kanisa, bila ya yeye kujadiliana na mtu mwingine yeyote. Mtu huyo anayestahili kuwa Papa anaweza kuwa miongoni mwa makadinali au hata asiye kadinali alimradi ana daraja la uaskofu.
4. Kila zoezi linapokamilika, kura huhesabiwa, na anayekuwa amependekezwa na makadinali wengi, lazima iwe kuanzia theluthi 2 kwenda juu , ndiye anayetangazwa kuwa Papa.
5. Kama hatapatikana aliyepata theluthi 2 kwenda juu, zoezi hurudiwa kwa siku 3 mfululizo.
6. Kama hata baada ya siku 3, hakuna aliyepata kura kuanzia kura theluthi 2 kwenda juu, waumini wanatengaziwa kuwa papa hajapatikana, bila hata ya kusomewa matokeo, kujua nani wamepigiwa kura na wamepata kura ngapi kila mmoja.
7. Kama Papa hakupatikana baada ya siku 3 mfululizo za kupiga kura, uchaguzi husimamishwa, na makadinali huingia katika maombi maalum. Kisha zoezi hurudiwa.
A. Wakati wote, makadinali wanapoingia kwenye maombi na wakati upigaji kura unaendelea, wakristo wengi huwa nje, nao wakifunga na kuomba ili Mungu amteue kiongozi wake mkuu wa Kanisa la hapa Duniani, kupitia kura zinazopigwa na makadinali.
NB: Historia inaonesha kuwa kuna wakati baada ya kupita miezi 6 bila ya kupatikana papa, waumini waliokuwa nje wakiomba na kufunga, huku kipindi cha baridi kikiwa kimeingia, walikasirika na kwenda kuvunja paa la jengo ambalo makadinali walikuwa wamejifungia. Waumini hao walidai kuwa makadinali walikosa imani ndiyo maana papa ameshindwa kupatikana. Makadinali wakapigwa na baridi kali, baada ya siku chache, Papa alipatikana.
Mpaka sasa, rekodi inayoonesha papa alipatikana kwa taabu sana, baada ya miaka mitatu, ni wa mwaka 1268, kufuatia kifo cha Papa Clement wa 4. Sababu zinazotajwa ni kwamba kulikuwepo makadinali waliotaka kutumia mbinu za kisiasa kuipata nafasi hiyo.
Kati ya mapapa wanaotajwa kupatikama kwa urahisi kabisa, ni Papa John Paulo wa pili, ambaye mzunguko wa kwanza tu, tayari kura zilitimia, na mchakato ukawa umekamilika.
Waumini wakatoliki na wasio wakatoliki, tumwombe Mungu amteue mtumishi afaaye kwa nafasi hiyo ya juu kabisa ya taasisi mojawapo kubwa kabisa ya kidini, yenye nafasi ya kugusa maisha ya watu wengi bila ya kujali imani zao
Huo no uchaguzi kama chaguzi zingine tu,tena hu-condpire nani aweAcha kufuru! Au unamaanisha ni imani kwa ule upande wa pili? Yaani imani iliyomwegemea ibilisi?
Mkuu umesema kuna rumours...... Rumours it's un official thing. Period.Kama ndivyo then why kuwe na rumours kuhusu yule jamaa wa ghana?