Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 790
- 1,316
Moja ya hotuba maarufu sana ya baba wa Taifa ilikuwa ni ile ya mwaka 1995 ambapo pamoja na mambo mengine alizungumzia nyufa za muungano.
Katika kipindi cha Urais wa Samia tumesikia mambo mengi, hususani kutoka kwa viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo ambao katika maeneo tofauti wamekuwa wakimtaja kama mzanzibari.
Ielewe kuwa Rais Samia maadam ni mtumishi wa Watanzania hawezi kukwepa kukosolewa, kushashauriwa na hata kupongezwa na waajiri wake. Lakini katika nchi iliyokwisha vuka viunzi vya ukabila, inashangaza kuona ukosoaji dhidi yake unapoambatanishwa na uzawa wake. Tabia hii kwa mujibu wa Mwl. Nyerere ni ukaburu, na inaibua hisia za ubaguzi dhidi yake.
Ukosoaji wenye sura niliyoitaja unaiweka nchi njia panda, kwani kura yoyote ya kumpinga Rais itaweza kuhusishwa na hisia za ubaguzi. Ingawa ushindi wa Rais Samia kwa hali ya kisiasa ilivyo upo dhahiri, na bila shaka CCM wamejipanga kumpigania, ukubwa wa ushindi wake utakuwa ni ujumbe wa uimara wa muungano wetu.