Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Ndivyo watakavyojibu. Japo kwa mujibu wa Katiba ya JMT, mhimili wa mahakama, ndio the custodian wa Katiba. Bunge lilitunga sheriaKwa hiyo mahakama watajenga hoja kwamba hawawezi kuingilia maswala ya mhimili mwingine, siyo? vipi swala la kuvunja katiba.....
batili ya kipengele cha mgombea uongozi kudhaminiwa na chama cha siasa, Mtikila akafungua kesi Mahakama Kuu kupinga kipengele hicho, akashinda, Mahakama Kuu ikatoa uamuzi kipengele hicho ni batili kwasababu kinakwenda kinyume cha katiba. Serikali ikakata rufaa, ikashindwa.
Ili kumkomoa Mtikila na kuidharau mahakama, Serikali ikapeleka bungeni sheria ya mabadiliko ya katiba kwa hati ya dharura na kukichomeka kipengele hicho batili ndani ya katiba, ili kuhalalisha sasa kiko kikatiba. Mtikila akapinga tena na akashinda tena kwa mahakama kutamka mabadiliko hayo ya katiba ni mabadiliko batili.
Serikali ikakata rufaa na mahakama ya rufaa Tanzania ikafikia uamuzi wa ajabu kuwahi kutokea Tanzania, ikatamka Mahakama haina uwezo wa kuliingilia Bunge na
kupinga kipengele chochote Bunge lilichokiingiza kwenye ndani ya katiba!.
Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
Wanabodi, Shurti la Mgombea Uongozi wa Umma, Kudhaminiwa na Chama cha Siasa ni Sheria Mbovu, ni... Kinyume cha Katiba, Kinyume cha Universal Declaration of Human Rights Kinyume cha The United Nations Human Rights Committee, Kinyume cha African Chatter of People and Political Rights Inaminya...