Ndo tunarudi pale pale... sidhani kama kuna kosa hapo limefanyika. Tusisahau, Ndugai ni Spika ambae jina lake lilipitishwa na chama.
At the same time, Kanuni ya 7 ya Bunge, Kifungu cha 3 kuhusu utaratibi wa uteuzi na uchaguzi wa Spika inasema:-
View attachment 2095216
Kumbe, Spika, kwa muktadha huu Ndugai, wala sio kwamba alipeleka mwenyewe jina lake kwa Katibu wa BUnge bali CHAMA chake ndicho kiliwasilisha jina la Ndugai kwa Katibu wa Bunge!!
Sasa Spika anapotaka kujiuzulu, sioni ni namna gani atapeleka barua moja kwa moja kwa Katibu wa Bunge badala ya kupeleka barua kwa chama chake kwamba "...ile kazi mliyonituma, imenishinda"!
Sasa chama kikishapata barua ya mtu ambae ilimtuma akawe spika kwamba anajiuzulu, ndipo nacho kitaandika taarifa kuipeleka kwa Katibu wa Bunge kwamba "yule mtu ambae tuliwaletea, effective to this date" amejiuzulu nafasi yake ya uspika!
Taarifa kama hiyo pia itawekwa public. Katibu wa Bunge nae akishapata taarifa atalitaarifu bunge na umma!