Jamaa walisindika hadi imewauma hata baadhi MaCCM kindaki ndaki, hao wasimamizi wa uchaguzi kila mmoja aliogopa asiwe wa kwanza kutangaza ushindi wa kiongozi yeyote wa upinzani.
Hapa hamna namna, wamlilie Magufuli akubali kubadilisha katiba iwape tume uhuru wa kusimamia uchaguzi bila kuingiliwa au kubabaishwa na dola, Nyerere alishawaonya siku hiyo katiba yao mbovu itakamatwa na kiongozi aina fulani watakoma, wanayaona.....leo hii unakuta mtu amevaa mavazi ya CCM full kijani lakini moyoni yuko upinzani.
Magufuli akibembelezwa vizuri anaweza akakubali irekebishwe maana yeye yuko kwenye hatamu ya mwisho na sidhani kama ana haja ya kuendelea kushikilia uongozi, jamhuri iko mikononi mwake 100%, afanye chochote akitakacho, aidha aandike historia upya na nzuri au aharibu kabisa.
Duh! Ama kwa kweli Watanzania, ukiondoa hawa wapiga makelele wa Jamii Forums, huwa ni watu wapole sana na wanyonge, yaani wananywea hadi huruma. Mzee Magufuli awahurumie watu wake na kurekebisha jameni.