Uchaguzi wa Tanzania umeporwa

Kiukweli Geza mimi hii kitu imenifanya niwenahamu yakujiunga na siasa rasimi. Hasa kupitia Chadema. Sio kwa sababu Magufuli sio raisi mzuri..Lakini kwa sababu nivyema kwa nchi makini kuweza kuwa na mawazo yenye mlengo tofauti kuwezesha kupata maendeleo thabiti...Bila upinzani CCM isingeweza kufanya yale wanayoyafanya leo. Kiongozi mzuri anatokana na upinzani dhabiti ndani ya nchi.
 
Hakuna jinsi Mkuu zaidi ya kupambana na kuuweka ukweli hadharani. Matakwa ya Watanzania ya kuchagua viongozi wanaostahili yataporwa hadi lini? Matakwa ya Watanzania kutaka Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi yatapuuzwa hadi lini!?
Hii nchi yetu sote...Naamini wataibuka wapinzani wapya wengi na hasa wenye fikra bora kuliko hata za Tundu Lissu.
 
Askofu kachanganyikiwa; sasa hajui kama Mungu yupo au la. Atajuta kujichanganya kwenye siasa.
Lakini hiyo haimnyimi haki yakuongea kile anachoamini. Ukweli lazima usemwe. It can take years to build a country but it can only be destroyed within a day for such things.
 
Huwezi amini Kama huu uzi kaanzisha geza😂😂
Sio Geza tu. Tupo wengi kwa Sasa. Msione tunasifia mazuri humu ndani. Lakini na mabaya tunayaona. Ni lazima ukweli usemwe. CCM imefanya kosa kubwa Sana.
 

Naona Wakenya mnapambana kweli ili na sisi tuwe kwenye meli moja na ninyi, sisi hatuendi hiyo njia yenu, nyie kaeni na Demokrasia yenu ya kuandika Katiba mpya kila siku, BTW watu wengi zaidi huuliwa na kuumizwa Kenya kwenye kila uchaguzi kuliko Tanzania yetu pamoja na Katiba yenu mpya na sijui Tume huru ambayo bado pia hamuitaki na sasa hivi mnataka nyingine sababu tu imeshindwa kumpa Raila Uraisi.

Mtalia na kupiga kelele muwezavyo lkn Tanzania yetu hatufwati hiyo njia yengu, Watanzania walio wengi wako poa na jinsi tulivyo na nchi yetu inavyokwenda hao wanaopiga kelele mitandaoni ni wengi wao ni machotara wachache na hawaishi Tanzania.
 
Wakenya walitegemea kile kilichltokea zanzibar juzi kingetokea Tanzania nzima, hawajajua tu watanzania ni watu wa aina gani
 
Aiseee dahh! Askofuu ww kwishneei!! hujipendi eti mazeee. Kim jon jiweee atakutanguliza mbele za hakii!
 
Mtulie hivyo hivyo yenu yanakuwa mchinjane

Sent from my H3223 using JamiiForums mobile app
 
Duh! Huyo askofu ameamua kujitoa kafara, anadiriki kutamka maneno mazito sana na kutuhumu bila kuficha.
Yaani Tanzania bana! Vitu zingine zinafanyika huko hadi naona wakati wa zama zile za kanu. Huyu ndio askofu Njoya wa Tanzania sasa. Ajitayarishe kichapo siku zijazo katika mkondo wake ameuchukua wa kuwa moja wapo wa wakombozi wa taifa lake.
 
expand...
Ni mataahira (mental retards) pekee ndiyo wanaweza kushangilia eti CCM na Magufuli wameshinda uchaguzi huu wa 2020.
 

Hamna namna Wakenya tunaweza kuwabadilisha Watanzania mfikie level yetu, haiwezekani kwa muda mfupi, itawachukua miaka mingi sana maana hivyo mlivyo ni zao la alichowafanya Nyerere kwenye ujamaa wake, alikua na nia njema ila akaishia kuwaponza. Yaani mpo mpo tu, wanyonge na dhaifu kupita maelezo.

Mimi hapa ni wale huwa mnaita mataga, yaani mataga wa Kikenya maana muda mwingi naunga juhudi za serikali mkono, naegemea sana kwenye hatua za serikali, ila moja nalojua haingetokea nikakubali serikali yetu ifanye hicho mlichokifanya huko, kwanza hapa kwetu kingenuka, hakungekalika, hauwezi ukasindika kura za Wakenya kihivyo na ukabaki salama, kha eti kwa wabunge 229 naona CCM imechukua 227 na upinzani wakaambulia wabunge wawili, jaribu upumbavu kama huo hapa kwetu ndio uone kama utatawala, mambo kama hayo hufanyiwa maiti sio watu.
Mimi pamoja na kwamba huwa nampigia rais Uhuru kura, ila ningekua wa kwanza kuingia barabarani kudai haki kwa ajili ya upinzani...

Nyie kilichosalia kwa sasa mjaribu hizo siasa za chama kimoja kwa miaka ijayo mitano, muone kama itakua nafuu ili upinzani ufutwe kabisa, ni kweli kwa mifumo ya kijamaa huwa haiendi kwa kutumia upinzani maana wananchi wamezoea kuswagwa na kushikiliwa akili, ukiwatisha kidogo tu wote chali. Ndio maana nikasema ili mfikie level ya Wakenya, itawachukua miaka mingi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…