Duduwasha
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 5,703
- 3,658
Hiyo ni list ya wenye damu za kunguniKibadeni vp! Kaukwaa ujumbe?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hiyo ni list ya wenye damu za kunguniKibadeni vp! Kaukwaa ujumbe?
Wataiendwsha TFF wanavyotaka au wanavyotakiwa na Katiba?Karia na Wambura wote ni Simba damu.
Sasa matopeni chezeni mpira visingizio vya Malinzi havitakuwepo tena.
Kamati ya mashindano ilijaa watu wenu lakini kila kitu ilikuwa Malinzi hiki, Malinzi kile.
sisi vijana wa chama cha mashambani au kijani mtu.wetu kushindwa yule mwakalibela imetufedhehesha sana.Japo tff imejaa mafisadi lkn mchezo uliokuwa unachezwa na viongoz wa serikali na wabunge wa ccm kutaka kufundisha wajumbe namna ya kupiga kura
Naamini kabisa wajumbe wamepiga kura za hasira kwa sababu tu walitaka kuwa proove wrong kuwa mpira hauendeshwi na siasa
Mwakyembe nyie na viongoz wengine nye ndo mliosababisha mayai tembele apigwe chin na wajumbe kwa hasira
Mayai naye ajifunze Mara ingne usmame wewe km wewe
Hongera warec karia angalau we huna siasa za manjano na wekundu
mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
Hata sisi hatujui kwa nini jamaa hali mayaiMbona walioshindwa kwa nafasi ya urais ni watano,kwanini ali mayay
Bless I
Alikuwa Ded mvomeroWasifu wa huyo karia ni upi?? Mwageni CV yake hapa
Mission inaweza kuwa mbaya au nzuriMbona huko Mara alikochaguliwa hajafanya lolote kwenye soka? Mwenzie Mwakalebera kapambana Lipuli imepanda daraja
Uchaguzi TFF umeshafanyika jioni ya leo ambapo Rais, Makamu wa Rais na wajumbe kadhaa wamechaguliwa.
Rais mteule ni Wallace Karia, Makamu wa Rais ni Michael Wambura.
View attachment 564289
Mchanganuo wa Kura kwa nafasi ya Urais:-
Jumla ya Kura zilizopigwa - 128
Kura zilizoharibika - 3
Wallace Karia - 95
Ally Mayay - 9
Shija Richard - 9
Iman Madega- 8
Mwakalebela- 3
Emmanuel Kimbe- 1
View attachment 564180
Wallace Karia
Wajumbe waliochaguliwa ni kama ifuatavyo:
Zone 1: Saloum Chama
Zone 2: Vedastus Lufano
Zone 3: Mbasha Matutu
Zone 4: Sarah Chao
Zone 5: Issa Bukuku
Zone 6: Kenneth Pesambili
Zone 7: Elias Mwanjala
Zone 8: James Mhagama
Zone 9: Dunstan Mkundi
Zone 10: Mohamed Aden
Zone 11: Francis Ndulane
Zone 12: Khalid Abdallah
Zone 13: Lameck Nyambaya
======
STORY:
KUFUATIA Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) uliofanyika leo katika Ukumbi wa St Gasper Mjini Dodoma na kumalizika jioni ya leo, Mwenyekiti wa Kamati ya TFF, wakili Revocatus Kuuli ametangaza matokeo ya Uchaguzi huo Wallace Karia ameshinda nafasi hiyo kwa jumla ya kura 95 kati ya kura halali 125 zilizopigwa huku kura tatu zikiharibika na Michael Wambura akichaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho hilo..
Wagombea wengine wa Urais pamoja na kura walizopata ni Ally Mayay Tembele (9), Shija Richard (9), Iman Madega (8), Frederick Mwakalebela (3) na Emmanuel Kimbe (1).
Mohamed Abeid (Dodoma na Singida), Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Sarah Chao (Arusha na Manyara), Dustan Ditopile (Lindi na Mtwara), Elias Mwanjala (Mbeya na Iringa), Francis (Pwani na Morogoro), Vedastus Lufano (Mara na Mwanza), Lameck Nyangaya (Dar es salaam), Kenneth Pesambili (Rukwa na Katavi), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga), Issa Mrisho (Kigoma na Tabora) na James Patrick (Njombe).
Rais wa Shirikisho hilo, Wallace Karia, Makamu wa Rais, Michael Richard Wambura pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliochaguliwa wameapishwa leo mjini Dodoma muda mfupi baada ya matokeo ya ushindi wao katika uchaguzi huo kutangazwa.
Akitoa hotuba yake muda mfupi baada ya kuapishwa kwake, Rais wa Shirikisho hilo (Wallace Karia) amesema kuwa amepigiwa simu na Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino pamoja na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad Ahmad na wote wamelipongeza Shirikisho hilo kwa uamuzi ulioufanya na kuutakia uongozi mpya mafanikio mema.
Aidha Karia amesema TFF itawapa waandishi wa habari elimu ili kujua mambo gani ya kuzingatia kuweza kuinua soka la Tanzania, huku akitangaza kuanzia leo, soka la Tanzania halitakuwa na ubabaishaji.
Kwa upande wake, Waziri mwenye dhamana ya Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ameiagiza TFF kuweka utaratibu wa kuchapisha taarifa ya mapato na matumizi kwenye magazeti ili wananchi wajue.