Uchaguzi wa TFF: Wallace Karia achaguliwa kuwa rais mpya wa TFF

Uchaguzi wa TFF: Wallace Karia achaguliwa kuwa rais mpya wa TFF

Karia na Wambura wote ni Simba damu.
Sasa matopeni chezeni mpira visingizio vya Malinzi havitakuwepo tena.

Kamati ya mashindano ilijaa watu wenu lakini kila kitu ilikuwa Malinzi hiki, Malinzi kile.
Wataiendwsha TFF wanavyotaka au wanavyotakiwa na Katiba?

Vv
 
Karia anaonekana ni Gentleman ataipeleka TFF mahali namtabiria kufka kuvaa viatu vya Leodiga Tenga. ....naaamini wenye makundi na walioandaa watu wao wamekosa hiyo ni safi cz kutakua na doscpline
 
Japo tff imejaa mafisadi lkn mchezo uliokuwa unachezwa na viongoz wa serikali na wabunge wa ccm kutaka kufundisha wajumbe namna ya kupiga kura

Naamini kabisa wajumbe wamepiga kura za hasira kwa sababu tu walitaka kuwa proove wrong kuwa mpira hauendeshwi na siasa

Mwakyembe nyie na viongoz wengine nye ndo mliosababisha mayai tembele apigwe chin na wajumbe kwa hasira

Mayai naye ajifunze Mara ingne usmame wewe km wewe

Hongera warec karia angalau we huna siasa za manjano na wekundu

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
sisi vijana wa chama cha mashambani au kijani mtu.wetu kushindwa yule mwakalibela imetufedhehesha sana.
 
Wasifu wa huyo karia ni upi?? Mwageni CV yake hapa
 
wambura aliondoka simba kwa zengwe sa sijajua km ataibeba simba.
 
Pamoja na ujuaji wake mwingi na maneno neno mengi, ukijumlisha na tambo zake za kutumia radio na tv pedwa ya Clouds, Shafii Dauda ameangukia pua ktk uchaguzi wa leo wa TFF kuwania Ujumbe kuwakilisha Mkoa wa Dar es salam. Amebwagwa chini na mgombea asie na Jina Lameck Nyambaya. Mpira sio maneno bwana dauda ni vitendo

ORODHA YA WAJUMBE WAPYA WA KAMATI YA UTENDAJI YA TFF WALIOSHINDA


Kanda namba 13 -Dar es Salaam

Mshindi ni Lameck Nyambaya

Kanda namba 12 Kilimanjaro na Tanga

Mshindi ni Khalid Andallah

Kanda No 11 Pwani na Morogoro

Francis ni Ndulane ameshinda

Kanda Namba 10 (Dodoma na Singida)

Mshindi: Mohamed Abeid

Kanda Namba 9 (Lindi na Mtwara)

Mshindi: Dunstan Mkundi

Kanda namba 8 (Njombe na Ruvuma)

Mshindi: James Mhagama

Kanda namba 7 (Mbeya na Iringa)

Mshindi: Elias Mwanjala

Kanda Namba 6 (Katavi na Rukwa)

Kenneth Pesambili

Kanda namba 5 (Kigoma na Tabora)

Issa Bukuku

Kanda namba 4 (Arusha na Manyara)

Mshindi: Sarah Chao

Kanda namba 3 (Shinyanga, Simiyu)

Mshindi: Mbasha Matutu

Kanda namba 2 (Mara, Mwanza)

Mshindi: Vedastus Lufano

Kanda namba 1 (Kagera, Geita)

Mshindi: Salum Chama

Makamu wa Rais

Michael Wambura

NAFASI YA RAIS

Wallace Karia
 
Kwenye uchaguzi kushinda na kushindwa ni kawaida.
Tunamshukuru hata hivyo kwa kujituma kwake kutuletea habari na uchambuzi wa soka
 
hongereni kwa wote mliochaguliwa, maana hata tukilaumu sana hatuwezi kupindua matokeo.
Fanyeni kazi ili timu yetu ipande ktk viwango vya fifa, angalau iwe ktk top 60.
 
Uchaguzi TFF umeshafanyika jioni ya leo ambapo Rais, Makamu wa Rais na wajumbe kadhaa wamechaguliwa.

Rais mteule ni Wallace Karia, Makamu wa Rais ni Michael Wambura.

View attachment 564289

Mchanganuo wa Kura kwa nafasi ya Urais:-
Jumla ya Kura zilizopigwa - 128
Kura zilizoharibika - 3

Wallace Karia - 95
Ally Mayay - 9
Shija Richard - 9
Iman Madega- 8
Mwakalebela- 3
Emmanuel Kimbe- 1

View attachment 564180
Wallace Karia


Wajumbe waliochaguliwa ni kama ifuatavyo:

Zone 1: Saloum Chama
Zone 2: Vedastus Lufano
Zone 3: Mbasha Matutu
Zone 4: Sarah Chao
Zone 5: Issa Bukuku
Zone 6: Kenneth Pesambili
Zone 7: Elias Mwanjala
Zone 8: James Mhagama
Zone 9: Dunstan Mkundi
Zone 10: Mohamed Aden
Zone 11: Francis Ndulane
Zone 12: Khalid Abdallah
Zone 13: Lameck Nyambaya

======
STORY:

KUFUATIA Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) uliofanyika leo katika Ukumbi wa St Gasper Mjini Dodoma na kumalizika jioni ya leo, Mwenyekiti wa Kamati ya TFF, wakili Revocatus Kuuli ametangaza matokeo ya Uchaguzi huo Wallace Karia ameshinda nafasi hiyo kwa jumla ya kura 95 kati ya kura halali 125 zilizopigwa huku kura tatu zikiharibika na Michael Wambura akichaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho hilo..

Wagombea wengine wa Urais pamoja na kura walizopata ni Ally Mayay Tembele (9), Shija Richard (9), Iman Madega (8), Frederick Mwakalebela (3) na Emmanuel Kimbe (1).

Mohamed Abeid (Dodoma na Singida), Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Sarah Chao (Arusha na Manyara), Dustan Ditopile (Lindi na Mtwara), Elias Mwanjala (Mbeya na Iringa), Francis (Pwani na Morogoro), Vedastus Lufano (Mara na Mwanza), Lameck Nyangaya (Dar es salaam), Kenneth Pesambili (Rukwa na Katavi), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga), Issa Mrisho (Kigoma na Tabora) na James Patrick (Njombe).

Rais wa Shirikisho hilo, Wallace Karia, Makamu wa Rais, Michael Richard Wambura pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliochaguliwa wameapishwa leo mjini Dodoma muda mfupi baada ya matokeo ya ushindi wao katika uchaguzi huo kutangazwa.

Akitoa hotuba yake muda mfupi baada ya kuapishwa kwake, Rais wa Shirikisho hilo (Wallace Karia) amesema kuwa amepigiwa simu na Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino pamoja na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad Ahmad na wote wamelipongeza Shirikisho hilo kwa uamuzi ulioufanya na kuutakia uongozi mpya mafanikio mema.

Aidha Karia amesema TFF itawapa waandishi wa habari elimu ili kujua mambo gani ya kuzingatia kuweza kuinua soka la Tanzania, huku akitangaza kuanzia leo, soka la Tanzania halitakuwa na ubabaishaji.

Kwa upande wake, Waziri mwenye dhamana ya Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ameiagiza TFF kuweka utaratibu wa kuchapisha taarifa ya mapato na matumizi kwenye magazeti ili wananchi wajue.

Ally Mayai alipiga kampeni kwa wanamichezo na media nakuwaacha wapiga kurahalisi next time anapakuanzia. Kusema turudishieni mpira wetu was the worst slogan and its failed kuwaunganisha wapigakura, kwa maoni yangu mayai angekuwa malinzi mwingine iwapo angeshinda (timua timua)
Dauda simwelewi na sijawahi kumwelewa kama kiongozi wa mpira, heko kwa ndondo cup although haina future mwenye kuendeleza soka letu ila kwa burudani sawa. And its known CMG inatoa back up kubwa kwa ndondo cup ukibisha subiria ya mkoani haitakuwa na utofauti na logi za TFF.

LAST Karia wape league vilabu wewe baki na taifa stars.
 
Back
Top Bottom