Hawa kweli ni watetezi wa haki za wanyonge, na Mungu azidi kuwabariki, si Kwa Dunia hii iliyojaa uchawa!!
 
Mwabukusi ni mwanasiasa kwa 100%.
Kwanini asitumike kisiasa wakati kuchaguliwa kwake kumepitia misukosuko na harakati zote za kisiasa?
Ni wapi siasa unaweza ukaitengenisha na maisha ya kila siku?

Uwakili/Uanasheria ni taaluma...
Uanasiasa si wakati wote ni taaluma...

TLS ni taasisi ya mawakili yenye malengo yasio ya kisiasa..
 
Sio kwamba Mwambukusi ataisaidia CDM, la hasha, ushindi wa Mwambukusi ambaye ni mrengo wa CDM ni ishara nzuri ya wananchi kujitambua na kukataa hila za CCM kama ambavyo wamefanya kwenye uchaguzi huu. Kazi ipo bado.
 
Nchi nzima watu wamebubujikwa macho ya furaha.

Mwabukusi ni Mwana NCCR
 
Kwa nini unafikiri ni changamoto wakati ni wajibu wake? Wewe ndio unaona changamoto sababu kinywa na matendo havijazoeya kutenda ya haki. Kula chakula hakujawahi kuwa changamoto kwa binadamu au kiumbe hai yoyote, labda wawe wagonjwa
Muda utaamua mkuu
 
Leo itabidi niwachinjie Familia kuku kusherekea ushindi wa Mwabukusi.
 
Una uhakika siku Mwambukusi akiongea ukweli kuhusu Mbowe mtamwelewa?

Mwambukusi ni mkweli kupitiliza, mna uhakika mtakua nae siku zote?

Mnakumbuka ajenda ya katiba mpya?

Nasubiri...
 
TLS hakuna uhusiano na CHADEMA,

Mwambukusi kashinda yeye kama yeye Wala hakuhusiani na kuwa mwanachama wa chama chochote Cha kisiasa.

Anaweza kwa mwanachama wa chama chochote, lakini kugombea kwake TLS hakuhusiani na chama chake Cha siasa.
 
Rais wa TLS BAK Mwabukusi amemshukuru Rais Mstaafu wa TLS mh Tundu Lisu Kwa kum endorse na kumpigia Kura

Naye Tundu Lisu amezipokea Shukrani za BAK Mwabukusi na kusema wote Wawili msimamo wao ni Mmoja tu yaani " Haki Huliinua Taifa"

Sabato njema 😃
 
Naona umeumia sana kuona Mwabukusi ameshinda. Na sasa umeamua kujifariji kimtindo kwa blah blah. Pole sana, yajayo yanafurahisha zaidi, jiandae kuumia zaidi. Huku Mwabukusi kule MOSAD, mwaka mtamu huu!
Kiniumize nini? Hakuna impact yoyote huko kwangu wala kwa mwengine.

Huko huwa tunawapeleka wasema hovyo. Umesahau?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…