Uchakavu wa noti uliokithiri katika mkoa wa Iringa na Njombe, je Benki kuu inaweza kuwa na mchango kulikabili hili?

Uchakavu wa noti uliokithiri katika mkoa wa Iringa na Njombe, je Benki kuu inaweza kuwa na mchango kulikabili hili?

init

Senior Member
Joined
Mar 22, 2021
Posts
115
Reaction score
109
Awali ya yote nipende kumshukuru yeyote atakaye nusa au kuuweka machoni uzi huu.

Nime kuwapo katika mikoa tajwa apo juu kwa vipindi tofauti tofauti. Katika vipindi hivyo vyote nimekuwa shuhuda wa tatizo hilo, noti zinazotumika katika mikoa tajwa zina hali mbaya. Kwa tizama yangu sabubu kuu ya uchakavu ni uhifadhi mbaya wa noti hizo, wakazi wengi huzifinyanga noti na hili nalitoa katika nilicho kiona.

Hivi karibuni tumeuona waraka wa Benki kuu ulio piga marufuku kugalagazwa kwa noti katika masherehe ikawa ni moja ya jitihada ya kuzuia uchakavu wa noti.

Swali langu kwenu ni je Benki Kuu hususani tawi la nyanda za juu kusini (Mbeya) au Mtwara wanawezachukua hatua gani kudhibiti uchakavu wa not sehemu hizo husika(Mapendekezo).
 
Back
Top Bottom