Hifadhi ya wanyama ya kisiwa cha Rubondo ipo Geita na kisiwa hicho kipo karibia na Chato,Mgodi wa dhahabu wa GGM upo karibia na Chato hapa kuliko mtu kutoka Geita then apite Sengerema kisha avuke maji afike wilaya ya Misungwi kisha aende Usagara kisha Buhongwa kisha Mkolani then Mkuyuni atoboe Pepsi kisha Mwanza Mjini Nara,Makongoro,apite Taqwa High School kisha kona ya bwiru aende Pasiansi kisha saba saba atoboe Ilemela ndio aingie airport Mwanza bora atoke Geita apite Buselesele kisha anaibukia Chato anakwea zake pipa
Wilaya ya Chato, Ngara, Biharamulo, Kahama na Bukombe zipo katikati ya ukanda wa nchi za maziwa makuu.
Uwanja huo kujengwa Wilaya ya Chato si tu kwa kuwa Rais anatoka huko, bali kijiografia Chato iko kama ilivyo Mwanza/Ilemela hivyo kufaa kwa ujenzi huo.
Lakini pia ujenzi huo utasisimua ujenzi wa miundombinu mingine ya kiuchumi kama vile biashara ya utalii, ujenzi ya mahoteli makubwa ya kisasa katika visiwa vinavyozunguka ziwa Victoria, Viwanda vikubwa vya samaki na nyama na kukuza biashara katika nchi za maziwa makuu (Congo, Rwanda, Uganda, Burundi, Tanzania na Zambia).
Ingelikuwa vyema iwapo wale wanaolalamika wangelifanya study tour ya kujionea fursa zilizoko ukanda huo hususani Wilaya ya Chato na Wilaya jirani, visiwa vinavyozunguka Ziwa Victoria na mandhali za kiutalii.
Ziwa Victoria ni muhimu katika ukanda wa maziwa makuu, hivyo hatuna budi kujenga miundombinu ya kisasa kulizunguka (kuanzia Mkoa wa Mara, Simiyu, Mwanza, Geita, Kagera).
Mojawapo ya mtaji wa kutuondolea utegemezi ni kulitumia ziwa Victoria katika utalii, biashara, usafirishaji, viwanda n. k,
Ni suala la kupanga na kuchagua ili baadae nguvu itakayotumika itumike pia katika maeneo mengine kwa awamu,kama ilivyo kwa ujenzi wa miundombinu ya maji na barabara, Usafiri wa Anga, (DSM) ,
Ujenzi wa reli ya kati SGR (DSM, Moro, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Mwanza na Kigoma) n. k
Tushikamane tuijenge Tanzania.