Uchambuzi: Hali ya Uwanja wa ndege wa Kimataifa Chato baada ya Magufuli kustaafu

Zahabu????
 
Maendeleo ya Chato ni sehemu ya Tanzania. Kama mikakati ikiwekwa hasa katika sekta ya Utalii na Wiwanda. Ndege zitatua tu hata kama Raisi wa Sasa Hatokuwepo Madarakani.
Mfano, Musoma kuna uwanja wa ndege lakini uwanja wa Bukoba hata kabla ya kuwa upgraded ulikuwa na ndege nyingi kuzidi Musoma. PW walikuwa wanaenda kila siku na hata mara mbili kwa baadhi ya siku, Auric walikuwa wanaenda mara tatu kila siku nk na sasa baada ya kuwekwa lami umeshamiri zaidi wakati una mita 1,200 tu!
Kwa hiyo kibiashara unajaribu soko kwanza alafu unaangalia mwelekeo, unajenga airstrip ya molam na ukiona mwitikio una upgrade. Kwa 3km x 45m ni sawa na mtu ambaye hajawahi hata kupanga chumba kuanza kwa kujenga ghorofa kwenye kiwanja cha square meter 3,000!
 

UtaKua na utindio kutoka Heita hadi Chato ni 3hrs kwann usijengwe geita..

Kitendo cha kuandika herufi kubwa tu kinaonyesha akili yako ilivyo ndogo
 
Sawa.. Nakubaliana na Wewe. Lakini pia na wewe kubariana na mimi
 
Mkuu uwanja Wa ndege ni muhimu katika kila Mji maana sometimes unatumika hata kuchukua wagojwa mahututu na kuwawahisha hospitali kubwa,lkn Kwa Mji Wa chato na hiyo miradi sijui ya migodi nk nadhani ilikuwa inatosha kabisa kujenga uwanja Mdogo Wa ndege kama Wa Arusha maana maana Kwa mbuga hiyo ya wanyama na cjui mgodi sidhani km kuna ndege kubwa km Boeing 737 itaenda huko.
 
Wilaya ya Chato, Ngara, Biharamulo, Kahama na Bukombe zipo katikati ya ukanda wa nchi za maziwa makuu.
Uwanja huo kujengwa Wilaya ya Chato si tu kwa kuwa Rais anatoka huko, bali kijiografia Chato iko kama ilivyo Mwanza/Ilemela hivyo kufaa kwa ujenzi huo.
Lakini pia ujenzi huo utasisimua ujenzi wa miundombinu mingine ya kiuchumi kama vile biashara ya utalii, ujenzi ya mahoteli makubwa ya kisasa katika visiwa vinavyozunguka ziwa Victoria, Viwanda vikubwa vya samaki na nyama na kukuza biashara katika nchi za maziwa makuu (Congo, Rwanda, Uganda, Burundi, Tanzania na Zambia).
Ingelikuwa vyema iwapo wale wanaolalamika wangelifanya study tour ya kujionea fursa zilizoko ukanda huo hususani Wilaya ya Chato na Wilaya jirani, visiwa vinavyozunguka Ziwa Victoria na mandhali za kiutalii.

Ziwa Victoria ni muhimu katika ukanda wa maziwa makuu, hivyo hatuna budi kujenga miundombinu ya kisasa kulizunguka (kuanzia Mkoa wa Mara, Simiyu, Mwanza, Geita, Kagera).

Mojawapo ya mtaji wa kutuondolea utegemezi ni kulitumia ziwa Victoria katika utalii, biashara, usafirishaji, viwanda n. k,

Ni suala la kupanga na kuchagua ili baadae nguvu itakayotumika itumike pia katika maeneo mengine kwa awamu,kama ilivyo kwa ujenzi wa miundombinu ya maji na barabara, Usafiri wa Anga, (DSM) ,

Ujenzi wa reli ya kati SGR (DSM, Moro, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Mwanza na Kigoma) n. k

Tushikamane tuijenge Tanzania.
 
Maendeleo ya Chato ni sehemu ya Tanzania. Kama mikakati ikiwekwa hasa katika sekta ya Utalii na Wiwanda. Ndege zitatua tu hata kama Raisi wa Sasa Hatokuwepo Madarakani.
Of coz naunga mkono hoja ya kujenga Viwanja vya ndege katika kila miji nchini maana vinasaidia hata kukimbiza wagonjwa mahututi kwenye hispitali kubwa Kwa ndege za Kukodi, ila nadhani Viwanja vya kawaida tu vinatosha na si lazima kujenga Viwanja vya kurushia mindege mikubwa
 
Ni kweli mkuu....
 
Umenena vyema mkuu
 
Naona unaonyesha Usukuma wako
 
Maendeleo ya Chato ni sehemu ya Tanzania. Kama mikakati ikiwekwa hasa katika sekta ya Utalii na Wiwanda. Ndege zitatua tu hata kama Raisi wa Sasa Hatokuwepo Madarakani.
Kwa mwendo huu tungekuwa na viwanja Butiama, Kisiju, Lupaso kule Masasi na Msoga
 
Ila wapinzani wa Tanzania hadi kero ase
Sasa hata makao makuu ya serikali Dodoma hakuna uwanja kama wa Chato!! Huoni ajabu?! Chato ilistahili air strip na uwanja mkubwa huo ungelijengwa Geita mkoani , wala mtu asingelilalamika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…