Uchambuzi: Hivi ndivyo kesi ya Yanga na TFF itavyokuwa huko CAS

Uchambuzi: Hivi ndivyo kesi ya Yanga na TFF itavyokuwa huko CAS

Labani og

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2020
Posts
19,637
Reaction score
29,473
HII KESI YA YANGA NA TFF ITAKAVYOKUWA KWENYE MAHAKAMA YA SOKA CAS.

Kwa utaalamu wangu wa Sheria kutoka chuo Bora MZUMBE UNIVERSITY ( Harvard of Africa)

CAS: Tumepokea malalamika kutoka Yanga SC dhidi yenu kwa kuailisha mechi kati ya Yanga Sc na Simba SC bila kufuata taratibu na kanuni zenu! Ebu tuambie ilikuaje?

TFF: Ni kweli tulifanya hivyo baada ya kupokea malalamiko kutoka Simba Sc kwamba walinyimwa haki yao ya kufanya mazoezi kwenye uwanja husika siku moja kabla.

YANGA SC: Iambie mahakama ni nani aliwanyima haki yao ya kufanya mazoezi?

TFF: Walisema ni Mabaunsa wa Yanga SC ndio waliwazuia kufanya mazoezi ya mwisho.

CAS: Hawa Mabaunsa ni akina nani kwenye club yenu?

YANGA SC: Hata sisi tunashangaa kutuhusisha sisi na Mabaunsa, maana katika muundo wa timu yetu hatuna waajiliwa wanaitwa Mabaunsa hata TFF wenyewe wanajua!

TFF: Sisi tuliambiwa na Simba SC kwamba tumezuiliwa na Mabaunsa wa Yanga SC sisi hatujui lolote kuhusu Mabaunsa.

YANGA SC: Je kanuni zetu zinasemaje kuhusu team mgeni kupata haki yake ya kufanya mazoezi siku moja kabla?

CAS: TFF jibu swali hilo!

TFF: Kanuni zetu zinasema timu mgeni inatakiwa iwasiliane na timu mwenyeji pamoja na kamisaa wa mchezo ili wapate kibali cha kuingia uwanjani.

CAS: Je Simba Sc walifanya hivyo?

TFF: Hapana hawakufanya hivyo walijiendea wenyewe tu bila kutoa taarifa.

CAS: Sasa hiyo haki wanayolilia ni ipi wakati hawakufuata utaratibu?

TFF: oooh! ooh! hata sisi tulipata kigugumizi kuamua jambo lao mwisho wa siku tukafanya busara tu.

CAS: Kulingana na kanuni zenu Simba Sc wapo sahihi kugoma kuingia uwanjani?

TFF: Hapana! Walitakiwa wacheze alafu baada ya mechi ndio suala lao lifanyiwe uchunguzi na kushughulikiwa kwa kuiadhibu timu mwenyeji kama wamehusika na kosa hilo.

YANGA SC: Iambie mahakama mliahilisha mechi kwa kutumia kanuni zipi?

TFF: Hakuna kanuni tuliyotumia bali tulitumia busara tu ili kuweka mambo sawa.

CAS: Mpira unaongozwa na kanuni hiyo busara imetoka wapi?

TFF: Ooh! ooh! hapo tulikosea!

CAS: Ni adhabu ipi inapewa timu inayogoma kuingia uwanjani?

TFF: Kupokwa points 15, faini

At the end Yanga atashinda
1741629535039.jpg

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Jaji: Ko kama mtu haonekani sura ni misukule

Basi hata hao misukule they don't have any correlation with young Africans

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Simba sc: Mh naomba mahakama yako tukufu itambue kuwa hatuna mamlaka ya kuahirisha mechi na hata hivyo mlalamikaji hakuenda kwenye mechi pia ili kusitahili kupata haki ya kikanuni
 
YANGA SC: Iambie mahakama ni nani aliwanyima haki yao ya kufanya mazoezi?
TFF: Walisema ni Mabaunsa wa Yanga SC ndio waliwazuia kufanya mazoezi ya mwisho.
CAS: Hawa Mabaunsa ni akina nani kwenye club yenu?
YANGA SC: Hata sisi tunashangaa kutuhusisha sisi na Mabaunsa, maana katika muundo wa timu yetu hatuna waajiliwa wanaitwa Mabaunsa hata TFF wenyewe wanajua!
TFF: Hii hapa kauli ya mwanasheria wa Yanga kuonyesha ni kweli waliwazuia Simba kufanya mazoezi kwa kusema eti nao pia walizuiwa katika mechi ya kwanza

1741770905896.png
 
Hakuna mtu aliyesoma mzumbe ana akili mbovu kama za kwako. Wewe nachelea kuamini kua umesoma ..siamini..tena unatumia tecno..[emoji23] hata neno ignorant halikukai , labda stupidity..
 
Hakuna mtu aliyesoma mzumbe ana akili mbovu kama za kwako. Wewe nachelea kuamini kua umesoma ..siamini..tena unatumia tecno..[emoji23] hata neno ignorant halikukai , labda stupidity..
Fuatilia madini heavyweight ninayoyatoa ...then utajua kua Labani og ni real product ya MZUMBE UNIVERSITY

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom