Sioni kosa kwa huo mtazamo wa Rais, hiyo dhana ya kila Rais kuja na mtazamo wake imeasisiwa na watangulizi wake, hivyo naye sio wa kwanza, japo hii tabia kwa namna fulani inachangia kuturudisha nyuma kitaifa, binafsi ningependa pawe na kitu kama succession plan kwa hawa viongozi wetu, anapomalizia mmoja ndipo aanzie mwingine.
Kuhusu kuvutia wawekezaji yupo sawa, hawa watu tunawahitaji na dollar zao watasaidia kwa namna kupunguza tatizo la ajira nchini, na kuongeza mzunguko wa pesa kwa watanzania kama anavyojinasibisha Rais, japo anatakiwa kuwa na tahadhari ahakikishe analinda maslahi yetu kama taifa.
Mfano. Alipozungumzia uchimbwaji wa madini ya Hellium yaliyopo kwenye mbuga fulani akasema Simba hawayali yale, sawa hawayali, lakini awe makini kwenye mikataba serikali yake itakayoingia na wawekezaji coz record za mikataba na wawekezaji kwa viongozi wa awamu zilizopita ni mbovu.
Mwisho kabisa unajinasibu kwa ujamaa kwa kusema wewe unaamini maendeleo ya mwafrika yataletwa na mwafrika mwenyewe, hiyo dhana kiukweli kwangu imepitwa na wakati, huu ujamaa wa mwafrika utaleta maendeleo gani bila kuwa na teknolojia, capital, na skilled man power inayohitajika? hapa unanikumbusha ile kauli ya Nyerere aliposema madini yaachwe ardhini yatachimbwa na mtanzania akiwa tayari.
Sasa kuliko kuendelea kusubiri huo utayari kwa serikali hii ya CCM ambayo imekuwa ikipigana na maadui watatu (ujinga, umaskini, maradhi) toka tupate uhuru zaidi ya miaka sitini sasa, huo utayari wa kuchimba wenyewe tutaupata lini? naona bora tuwape wazungu wachimbe, lakini tuhakikishe tunapata faida badala ya kuwaachia wazungu waondoke na faida huku viongozi wetu wakipata 10% na sisi kuachiwa mashimo.