PostGE2025 Uchambuzi: Je, MaSheikh wapo sawa kutounga mkono maandamano kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu?

PostGE2025 Uchambuzi: Je, MaSheikh wapo sawa kutounga mkono maandamano kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Vipi kuhusu kutukata vichwa?
Makosa makubwa Sheikh aliyetoa Hilo tamko katika kwa jazba na mihemko huenda ni mjinga , akili yake ndogo au muhuni.
 
Busu la Kenge mkuu hebu njoo na ushahidi wa imam alipoandamana kuupigania uislam!
Mcheki mwamba hapo chini sura ya kazi mkombozi wa waislamu kipenzi chetu cha dhati Imam Hussain Ibn Ali alipokuwa anaelekea Karbala kuutetea, kuupigania na kuulinda uislam dhidi ya dhulma, ukandamizaji, udhalilishaji na uonevu.
Screenshot_2025-07-11-11-53-45-34_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12~2.jpg
Screenshot_2025-07-11-11-53-58-13_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12~3.jpg

adriz de mbusii
 
Nimekopi andiko katika Uzi wa safuher , ameongea point sana Wazee wa mihemko watapinga . Uhai wako una thamani sana usikubali upotezwe kizembe .

Imeshazungumzwa sana makosa yaliyofanyika kwa upande wa mamlaka, lakini ni vyema tukageuza upande wa pili wa shilingi.

Kwa nini nasema mange hathamini uhai wa watanzania bali anajithamini yeye tu uhai wake?

Gwajima alipokuwa anakemea utekaji alitolea mifano kwa watoto wa viongozi akimaanisha kwamba Uhai wa mtu yeyote una thamani bila kujali ana nafasi gani,hata mange anaungs moono jambo hili.

Kama Uhai wa watu wote sawa bila kujali nafasi ya mtu mbona mange kimambi alijificha kwenye gari marekani kwenye maandamano ya daispora akiogopa kudhurika, lakini mange huyu huyu anawaambia watanzania wasijifiche watoke nje waandamane?

Kwa nini asiwape strategy yake aliyoitumia marekani ya kukaa kwemye gari au ndani ili asidhurike abaki hai?

Mbona watanzania anawaambia watoke nje wakaandamane, je hathamini uhai wa watanzania ndio maana anawashauri mambo ambayo yeye hayafanyi?

Uhai wa mange, uhai wa gwajima,uhai wa mtoto wa kiongozi yeyote ni sawa hakuna mwenye haki ya kuishi kuliko mwenzie.

Hivyo mange kama ambavyo yeye alifanya kila namna(kujificha)ili abaki kuwa hai basi ilitakiwa awape nammna hizo watanzania ili na wao wabaki kuwa hai.
 
Haifai kufanya uasi dhidi ya mtawala Muislam hata kama atakuwa ni muovu. Na atasikilizwa na kutiiwa (katika yasiyokuwa maasi)

Na kama mtawala ni kafiri basi haifai kumtoa kama kumtoa kutasabisha umwagaji wa damu na fitna. Hivyo atasikilizwa na kutiiwa katika yasiyo maasi.

Uislam una misingi thabiti mno kuchunga maslahi na kuondoa madhara.

Mtume alipambana kijeshi kuangusha utawala dhalimu wa makafiri wa Makkah
 
Ulitaka nife ungeingiza pesa kiasi gani?
Hahahahaha !! kumbe una akili . Kwa hiyo haukutoka siku hiyo ?

Kongole kwa kulinda uhai wako maana ungewapa huzuninna hasara wazazi na watu wako wa karibu .
 
Hahahahaha !! kumbe una akili . Kwa hiyo haukutoka siku hiyo ?

Kongole kwa kulinda uhai wako maana ungewapa huzuninna hasara wazazi na watu wako wa karibu .
Nilitoka ila kufa sikufa, nashangaa wewe unayeniombea kifo mchana kweupe!
 
Mtume alipambana kijeshi kuangusha utawala dhalimu wa makafiri wa Makka
Mapambano ya vita (Jihad ) dhidi ya Makafiri hayakupuganwa Maka mpaka alipotengeneza Dola na kuwa na utawala na Jeshi kamili Madina ndipo mapambano yalianza.

Kipindi Cha Makka Mtume (Peace and blessings be upon Him) na Maswahaba wake (Allaah awaridhie) walipata shida nyingi na Mateso lakini hawakuamrishwa kupigana Wala hawakupigana kutokana na hawakuwa na uwezo , Dola pamoja na madhara makubwa yanapatikana kipindi hiko .

Tena mateso yalikuwa makali sana na wengine waliuwawa lakini waliambiwa hakuna kupigana wawe na subira.

Kama haumani tumia hata Ai au gugo uliza kama kuliwahi kuwa na vita yeyote katika miaka yote mingi ya maisha ya Makkah ? na ukisoma vitabu utaelewa zaidi.
 
Vita vya Badr waislamu walikuwa wamezidiwa takriban mara tatu au nne. Ushindi wao haukutokana na uimara wa jeshi lao au mbinu zao za kijeshi bali ulitokana na DIRECT INTERVENTION ya ALLAH, aliwatumia malaika wakawa wanapambana bega kwa bega na waumini.

Tunarudi palepale, Kama kuuondoa uovu kwa mkono wako huwezi basi kemea. Njia moja ya kukemea ni kuzungumza maneno ya kweli na kutoa matamko ya kweli ya kukemea maovu hayo nchini kama vile utekaji watu, kutumia mahakama kuiba haki za watu badala ya kuwapa haki zao n.k. Tulitegemea kuwaona Masheikh maadamu hawana ubavu wa kuondoa uovu huu kwa mikono yao basi WAKEMEE KWA NGUVU ZOTE!, Sasa wao hawakemei,wanangoja Maaskofu Wakemee halafu wao waje wawakemee Maaskofu!.

Kama wanaweza kuwakemea maaskofu basi kumbe wanaweza kukemea wizi wa kura, ufisadi, rushwa, utekaji, umangimeza na mambo kibao maovu, lakini unfortunately hawafanyi!
 
Juulize kwa nini hakupigana Makkah licha ya mateso makubwa waliyopitia Waislamu kipindi wako huko mpaka wakakimbilia Ethiopia Kisha wakaja kupigana Badri baada ya miaka kibao kupitia .

Kukemea ipo lakini Kuna njia zake , Kuna muongozo wa Uislamu katika Hilo na ipo hadithi inataka mtawala asikosolewe hadharani na kumuamrisha bali kumnasihi kwa Siri . Vilevile inatakiwa kupima madhara kwenye moto usiweke moto hali ya sasa tension ni kubwa MaSheikh kuanza kupiga spana hadharani ni kuingiza nchi kwenye ghasia kubwa .
 
Kitabu hakiruhusu maandamano? Sawa. Vipi kuhusu kuongozwa na Mwanamke? Kinaruhusu jambo hilo?
 
Back
Top Bottom