Mahondaw
JF-Expert Member
- Apr 9, 2013
- 75,495
- 185,562
Nawe wasapoti waandane lo!!!????
Nawe wasapoti waandane lo!!!????
Mtume alipambana kijeshi kuangusha utawala dhalimu wa makafiri wa Makkah
Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) alipokuwa Makkah hakupigana. Acha kupotosha. Na Mtume alipigana na makafiri wa Makkah baada ya kufanya Hijra kwenda Madinah na baada ya kuanzishwa Dola ya kwanza ya Kiislam huko Madinah. Mtume kapigana na makafiri wa Makkah wakati tayari Dola imesimama Madinah huko.
Kwahiyo ilikuwa ni Dola mbili tofauti kabisa zinapigana, moja ya Kiislam ikiongozwa na Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake), nyengine ya kikafiri chini ya makafiri wa kiquraysh. Na mwanzo Mtume alipigana defensive wars dhidi ya makafiri waliotaka kuivunja Dola ya Kiislam na baadae akaingia nao Mkataba wa Hudaybiya uliokuwa na terms ambazo zilionekana kuwa dhidi ya Waislam, na Mkataba wa Hudaybiya ulifanyika baada ya makafiri wa kiquraiysh kuwazuia Waislam kwenda Makkah kutekeleza Amri ya Allah, Waislam wakafanya Suluhu ya Hudaybiya tena kwa terms walizozitaka makafiri wenyewe na zilizoonekana harsh kwa Waislam (Sulhu ya Hudaybiya na matukio yaliyotokea kupelekea Sulhu hiyo, matukio wakati wa Sulhu hiyo, sulhu yenyewe na matukio baada yake kuna mazingatio makubwa mno kwetu). Ila makafiri wakauvunja mkataba baada ya miaka miwili, Mtume akaikomboa Makkah, tena bila umwagikaji mkubwa wa damu na wakati ambao Waislam wamepewa nguvu nyingi sana tayari, Dola ya Kiislam ilikuwa na nguvu nyingi tayari. Zingatia hilo. Zingatia hiyo context.
Hivyo unachotaka kufananisha havifanani.
Na Mtume hakuwa akipigania demokrasia. Wala Jihaad yake haikuwa kwa maandamano.
Na ni Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) ndio katukataza kabisa kufanya uasi dhidi ya mtawala Muislam anayetutawala hata kama atakuwa muovu na dhalimu na tukaambiwa tumsikilize na kumtii (katika yasiyo maasi).
Bali hata kama kafiri akitutawala (tukawa chini yake), iwapo kama kumtoa huyo kafiri anayetutawala kutasababisha fitna na umwagaji wa damu tumekatazwa kupambana naye na kufanya uasi dhidi yake, na tunapaswa kumsikiliza na kumtii katika yasiyo maasi.
Na ndio maana Wanachuoni wetu waliosimama sawa katika Sunnah waliwakataza waLibya kufanya uasi na kupambana na Gaddafi licha ya kuwa Wanachuoni walimkufurisha Gaddafi. Waliwakataza ili kuzuia madhara, fitna na ufisadi ambao ungeibuka. Ila watu wakafanya uasi na wakamuua Gaddafi, Libya mpaka leo wanajuta. Gaddafi alikuwa kafiri, na alikuwa mtawala dhalimu, jeuri, ila Wanachuoni walikataza uasi dhidi yake ili kuepusha fitna na kuchunga maslahi mapana ya Ummah, na Allah Aliwafungulia WaLibya katika Dunia yao wakati wa utawala wa Gaddafi licha ya ukafiri wake Gaddafi.
Wakafanya uasi dhidi ya Gaddafi na wakamuua. Itazame Libya leo.
Wanawachuoni walipinga maandamano ya kuuondoa utawala wa Bashar huko Syria, licha ya kuwa Bashar ni kafiri, matokeo yake Syria ikaingia vitani miaka 13, malaki ya watu wakauawa, milango ya fitna ikafunguka, nchi za makafiri zikapata upenyo wa kuivamia Syria.
Wakati wa baba yake Bashar, Hafez ambaye pia alikuwa kafiri, kuna watu walifanya uasi dhidi yake huko Hama, Syria, mwaka 1982 kukatokea mauaji mabaya mno na umwagaji mkubwa mno wa damu. Walioanzisha uasi ule walikosea.
Kama haifai kuwatoa watawala makafiri wa wazi kabisa iwapo kama kuwatoa kutasababisha umwagaji wa damu na fitna. Kufanya uasi dhidi ya watawala Waislam ndio kabisa imekatazwa, kabisa!
Kuwatii watawala wanaotutawala na kuwasikiliza katika yasiyo maasi na kutowafanyia uasi na kutopigana nao na kutowasema hadharani, hayo ni Mafundisho ya Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake).
Sio kila mwenye ndevu ni sheikh wengine ni vichaaUislamu haisapoti wahuni kwaiyo masheihk wako sawa
Mimi niletewe kile kifungu kinachokataza mwanamke kuwa kiongozi tuone kama wako sahihiMoja kwa moja..
Kumekuwa na hoja miongoni mwa watu kuwa viongozi wa dini wa Kiislamu hawatetei haki wapo nyuma katika yale yanayoendelea nchini au wamepewa posho . Sasa nataka nichambue na tujadiliane wote kistaarabu kutokana na uelewa wangu wa kidini na kiulimwengu kutoka na hoja hizo.
Kwanza kabisa dini ya Uislamu inapinga mauji ya watu wasio na hatia , na dhuluma juu ya kiumbe chochote awe Muislamu, mkiristo , Yahudi hata adui yako nk haitakiwi kumfanyi dhuluma , kama aya inavyoeleza 👇👇
" ...Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni audilifu . Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamungu.." {5 : 8}
View attachment 3506997
Na Uislamu unapinga mauji yeyote ya dhuluma na adhabu yake ni Kali mno kama kama inavyosema Aya hapo ,👇👇
"...kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote.." {5 : 32 }
View attachment 3507000
📝 MIONGONI MWA SABABU ZA KISHERIA ZINAZOFANYA MASHEIK NA WAISLAMU KUKAA MBALI NA MAANDAMANO.
NB : Kuna watu wanasema Masheik wanaona kiongozi ni Muislamu mwenzao ndio maana hawaonyeshi kuunga mkono maandamano, hoja hizo hazina nguvu sababu zinazofanya wasiunge mkono maandamano sio aliyopo ni Muislamu bali hata wakati wa Magu hali haikuwa tofauti walikuwa watii kwa Mamlaka.
1. Hakuna maelekekezo kutoka kwenye maandiko yanayotaka kuandamana katika kudai haki .
Masheik wanasimamia dini na dini ya Uislamu imetoa muongozo katika kila majambo hata jinsi ya kuyaendea .
Muongozo wa Uislamu umeelekeza kwanza kutii Mtawala hata akiwa sio Muislamu maadamu hakuamrishi katika maasi , na ikiwa atakuamrisha maasi hautomtii kwenye huo uasi anaokuamarisha bali utamtii kwenye majambo mengine. Kama inavyoeleza katika Aya hii 👇👇
" Enyi mlio amini! Mtiini Mwenyezi Mungu, na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi " { 4 : 59 }
Je , kiongozi akizidi ujeuri na dhuluma hatuna nafasi ya kujinasua ?
Kiongozi ni product ya jamii , Jamii ikiwa ya hovyo lazima watapatikana viongozi wa hovyo hakuna namna ndio maana sisi kwa sisi tunafanyiana dhuluma sana mtu hata apewe kitengo kidogo cha kukusanya pesa ya rambirambi unakuta huko mtu anachukichia sasa mtu kama huyo akija kupata madaraka atakuwa fisadi zaidi.
Katika Uislamu kutengeneza Jamii lazima utengeneze watu na kutengeneza watu ni lazima kuanzie katika Misingi ya chini kwenye Familia , malezi na Elimu na wao wenyewe kuwa waadilifu na wachamungu kabla ya kutaka viongozi wao wawe waadilifu. 👇👇
" ..Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo nafsini mwao.. " { 13 : 11 }
View attachment 3507007
Je , hatuwezi kutoka kupigana na kufanya Uasi katika kujinasua ?
Kabla ya kutaka kupigana au kufanya Uasi kwanza anagalia haya ;👇
a) Uwezo wa kupigana unao yaani umejipanga ?
Kama mnakumbukumbu siku za mwanzo wa shambulio la October 7 Waislamu baadhi waliwashangilia Hamas na kuona vidume wanapigania haki hawataki uonevu lakini Mimi nikisikitika na kuonya kuwa wamefanya upuuzi na utawaponza mno sababu .
i)Hamas walikuwa kama wamekurupuka hawakujipanga kivita bali ni kufanya ambush na ufedhuli .
ii) Hamas hawezi KuBattle na so called Israel state sababu ukiCompare uwezo wa kijeshi na allies Hamas wameachwa mbali mno.
iii) Retaliation ya Netanyahu itakuwa haina huruma kabisa jamaa ni mwendawazimu.
Usipokuwa na uwezo wa KuBattle na mpinzani wako Wala kujipanga kisasawa ni sawa na kujiua kizembe Kwa sababu hizo MaSheikh hawawezi kuwaambia waumini wao watoke wakati ;
i) Polisi ana Gun na mabomu , halafu raia wana mawe na fimbo .
ii) Ukichaa wa Polisi na ukatili wao unafahamika ukikutana nao katika mazingira hayo hakuna chance ya kuBattle wakati raia mpo peke yenu bare hands hata kama mpo wengi.
Msingi huu upo hata katika Jihad za kisheria kiongozi wa Dola ya Kiislamu katika nchi ya Kiislamu haurusiwi kutoa jeshi ukiwa disorganized na uwezo wako ni mdogo kuBatte na mpinzani .Inachotakiwa ni kujipanga kwanza kikamilifu Kisha kujiingiza vitani. Ndio maana hata vita ikawekewa nidhamu na watu kiasi gani mpambane na watu kiasi gani na sio kwenda kizembe mkafyekwa wote 👇👇
" Kwa hivyo wakiwa wapo watu mia moja kati yenu wenye kusubiri watawashinda mia mbili. Na wakiwapo elfu moja watawashinda elfu mbili, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na ( 8 : 66 )
Vilevile kukawekwa nidhamu ya kujiandaa kwa uwezo wote dhidi ya adui na sio kwenda kizembe au kukaa kizembe bila maandalizi , isiwe adui ana Hypersonic ballistic missile na Nyuklia wewe vibomu vya kawaida , adui yako ana Gun wewe una panga na fimbo . Muislamu hatakiwi kwenda front vita kama hiyo 👇👇
View attachment 3507020
b) Kupima madhara yake kabla ya uasi na vita.
Kanuni ya msingi katika Uislamu likiwa jambo lina Faida na madhara , basi unaangalia kipi kitazidi mizani kati ya Faida na madhara au Faida zitakuwa chache lakini madhara makubwa ? Kama jambo lina Faida lakini madhara ni makubwa basi tunaacha kwani kuondosha madhara makubwa ndio kunapaswa.
kutangulizwa kwanza kuliko kuangalia Faida zitakazopatikana .
Ndio maana niliwasikitia WaPalestina since day one kabla ya kilicho wakuta sababu nilijua jinsi hali Yao ilivyo na adui wao alivyo katili...
NB : Episode ya kwanza imeisha uzi utaendelee na episode ya pili ambayo panapo majaliwa utaeleza sababu nyingine na kuchambua ;
1. Je , inaruhusiwa kukalia maovu kimya bila kukemea ?
2. Je , Kuna njia ngapi za kukema maovu na ipi Bora kutumika kwa wakati upi ?
3. Uchambuzi wa kuhusu kipi Cha kufanya juu mtawala muovu kwa mujibu wa mafundisho sahihi ya Uislamu.
Huu Uzi nimeuketa sababu Kuna Waislamu waliniomba hapa jukwaani live na wengine kunifuata PM kutaka nifafanulie kwa mujibu wa Uislamu niweke na dalili kuhusu wajibu wetu sisi Waislamu kwa yanayoendelea tukiwa kama sehemu ya nchi na Jamii kwa ujumla.
Mtume hakuishi Makkah tu, aliishi Makkah na Madina, ni nchi ileile ya Hijaz.
Makkah na Madina ilikuwa Dola moja? Wakati Mtume anahama kuhamia Madinah, hii Miji miwili ilikuwa Dola moja? Hijaz ilikuwa na Dola ngapi? Makuraish wa Makkah walikuwa wanatawala mpaka Madinah? Huelewi nini hapo?
Mtume alihama kutoka Makkah akaenda Madinah wakati huo hizo ni territories mbili tofauti.
Kwani, kwa mfano, ukanda kuitwa Afrika ya Mashariki hiyo maana yake ni nchi moja hiyo? Si kuna Tanzania, Kenya, Uganda, Somalia, Rwanda, Burundi, Sudan Kusini na DRC, si Dola tofauti kabisa hizo? Kama ikatokea baadae nchi hizi zikaungana kuunda Dola/Taifa moja, inaondoa ukweli kuwa zilikuwa ni Dola tofauti zamani? Hata hii Tanzania si kitambo kidogo tu hapo kulikuwa kuna kingdoms na Dola tofauti tofauti ndani yake? Wachaga walikuwa na Dola yao, Wanyamwezi walikuwa na Dola yao, Wahehe walikuwa na Dola yao, Wasambaa nao walikuwa na Dola yao. Kulikuwa kuna mpaka Dola ya Kiislam huko nyuma. Ila sasa hivi kuna Tanzania.
Wewe chukua hii kuwa Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) katukataza kuwapiga vita watawala wetu na kuwafanyia uasi dhidi yao. Na madhara ya kufanya hivyo yapo wazi yameshuhudiwa tokea zamani na mpaka sasa tunayashuhudia. Madhara yake ni makubwa zaidi.
Na kuna maelezo marefu kidogo nimeyaandika kwenye ile comment yangu, yazingatie nakunasihi.
Allah Aniongoze mimi na wewe katika njia ikiyonyooka, Aamiin.
Sasa kwanini BAKWATA wako ktk kumlinda hivyo?Hakiruhusu Mwanamke wala demokrasia
Hata sielewi nini kimeikutaVipi mkuu mbona akaunti mpya ya Zamani Ina shida gani ?
Kwa hiyo unataka kutwambia Waislamu nchini tusijiunge na vyama vya upinzani kupinga sera za mtawala ambazo tunadhani siyo sahihi ili tumg'oe madarakani tuiongoze nchi?.
Kwa hiyo waislamu kule Zanzibar wanafanya makosa kujiunga na ACT ili kumng'oa Hussein Mwinyi?
Omar alipingana na watawala wa Makkah waziwazi akiwa ndani ya Makkah kabla hata ya kufanya Hijra, Alitangaza kabisa, akawaambia kuwa yeye sasa anahamia Madina, basi yeyote anayetaka kuacha mjane amfuate nyuma.
Nabii Musa alipingana na Firauni waziwazi.
Nabii Ibraahiym (Amani iwe juu yake) alipigana nae? Aliandamana? Mjadala aliofanya nae si ulikuwa mbele yake yule mfalme?Nabii Ibrahim alivunja masanamu, na alimchallenge mfalme wa nchi yake waziwazi.
Maandamano ni haramu katika Uislam. Na sio njia ya kuamrisha mema wala kukataza maovu wala sio katika Jihaad. Sio katika Qur-aan wala Sunnah ya Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) na hakuna katika Wema waliotangulia (Maswahaba zake Mtume Swala na Salamu ziwe juu yake (Allah Awaridhie) na waliofuata njia yao katika vizazi vya kwanza bora) aliyekutangulia kufanya maandamano na wao ndio ufahamu wao wa Qur-aan na Sunnah tumetakiwa kuufuata. Bali maandamano ni katika mitindo ambayo asili yake sio Waislam, ni katika mila za makafiri na ni kinyume na Uislam.Hakuna mahali uislamu umekataza demokrasia, kama una hadithi au aya uislamu ukisema kuwa demokrasia ni haramu ilete hapa.
Hakuna mahali uislamu umekataza maandamano, ndiyo maana masheikh wetu huko Zanzibar mara kibao wameongoza maandamano ya kutaka mamlaka kamili na ndiyo maana waislamu hapa nchini washaandamana sana kudai haki zao. Usitake kusema kuwa walikosea.
Mafundisho ya Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) kuhusiana na namna ya kuamiliana na watawala ni yapi?
Waislam hawakupigana kabisa walipokuwa Makkah, bali waliamrishwa kuzuia mikono yao.
Ilikuwa kwa maandamano? Au kwa kumpinga kwenye majukwaa ya hadharani? Au majukwaa ya kisiasa na mikutano ya hadhara? Ilikuwa ni mbele yake Fir'awn . Tena Allah (Subhaanahu Wa Ta'ala) Akawaamrisha Nabii Mussa na ndugu yake Nabii Harun (Amani iwe juu yao kwa kuwaambia;
فَقُولَا لَهُ قَوْلًا لَّيِّنًا لَّعَلَّهُ يَتَذَكَّرُ أَوْ يَخْشَىٰ﴾
[ طه: 44]
Mwambieni maneno laini, huenda akazingatia au akaogopa.
Fikiria Fir'awn alivyochupa mipaka mpaka akajiita mungu, ila angalia maagizo ya Allah kwa Mitume wake ya namna ya kuamiliana na Fir'awn. Zingatia hilo!
Na pia zingatia, walimnasihi mbele yake, walimfuata wakamnasihi mbele yake. Hawakumsema nyuma ya kisogo chake.
Na pia Nabii Mussa na Nabii Harun (Amani iwe juu yao) walipigana na Fir'awn? Waliandamana dhidi yake?
Halafu Mtume wa Mwisho, Muhammad (Swala na Salamu ziwe juu yake) aliyekuja na Shari'ah ya mwisho itakayobaki mpaka Qiyama katufundisha nini kuhusiana na namna ya kuamiliana na mtawala?
Nabii Ibraahiym (Amani iwe juu yake) alipigana nae? Aliandamana? Mjadala aliofanya nae si ulikuwa mbele yake yule mfalme?
Maandamano ni haramu katika Uislam. Na sio njia ya kuamrisha mema wala kukataza maovu wala sio katika Jihaad. Sio katika Qur-aan wala Sunnah ya Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) na hakuna katika Wema waliotangulia (Maswahaba zake Mtume Swala na Salamu ziwe juu yake (Allah Awaridhie) na waliofuata njia yao katika vizazi vya kwanza bora) aliyekutangulia kufanya maandamano na wao ndio ufahamu wao wa Qur-aan na Sunnah tumetakiwa kuufuata. Bali maandamano ni katika mitindo ambayo asili yake sio Waislam, ni katika mila za makafiri na ni kinyume na Uislam.
Na demokrasia sio katika Uislam. Misingi yake mingi mikubwa iko kinyume na Uislam, bali mengine ni kufru kabisa. Ni katika demokrasia ndio utakuta baba na mtoto ni sawa kabisa hawana tofauti. Ni katika demokrasia ndio mwanachuoni na mpumbavu wa mwisho kabisa wanawekwa daraja moja. Eti watu wanajitungia sheria zao wenyewe na wao wanajiamulia kila kitu kinyume kabisa na Shari'ah za Allah. Kuna mitazamo potofu mingi sana.
Maandamano ni haramu hata kama kuna Waislam waliyafanya na wanayafanya. Ni katika mila za makafiri ambazo cha kusikitisha sana baadhi yetu Waislam tumeziiga kinyume na Dini yetu na kuacha Muongozo wa Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) na ndio maana udhalili kwetu Waislam hauishi na unyonge umekuwa mwingi kwa sababu ya kwenda kinyume na Muongozo wa Mtume wetu (Swala na Salamu ziwe juu yake). Na wengi wanafanya kwa ujinga, hawajui.
Namuomba Allah Atusamehe sisi na ndugu zetu. Na Atuongoze na Atuunganishe katika Tawheed na Sunnah na Atufishe sote katika Tawheed na Sunnah, Aamiin.
Hakuna Nabii yeyote (Amani iwe juu yake) aliyedai demokrasia wala kuilingania. Hakuna yoyote katika Salaf aliyekutangulia kuruhusu maandamano, bali hili jambo halikuwepo kabisa kwao. Na hakuna hata mmoja wao aliyedai demokrasia wala kuilingania.
Mbona utamtizamo finyu ?1. Lete aya na hadithi wapi maandamano ni haramu. Huo mtizamo unaouleta ni mtizamo wako na wa baadhi ya masheikh hasa wa Kisalafi hatukubali kila kitu wanachokisema. Ni masheikh wanaotumiwa na dola za wafalme wa kiarabu wa siku hizi wanaotaka waislamu walale usingizi wa pono wasiinuke kuwang'oa madarakani kwa udhalimu wao
2. Masheikh wetu hapa Tanzania waliongoza harakati za kumng'oa mkoloni. Kwa mantiki yako unayoleta, unawaona masheikh wetu kama waasi wa watawala, na ungependa wamtii mkoloni, maana ndiye aliyekuwa mtawala wao.
3. Waislamu nchi hii wameandamana kupinga mabucha ya nguruwe ktk makazi yao, kupinga uonevu ktk usahihishaji wa somo la Dini uliokuwa unafanyika NECTA, Na masheikh wetu waliandamana kudai mamlaka kamili Zanzibar. Sasa wewe unataka kutwambia kuwa hawa wote hawaijui dini?
5. Mbona falme za kiarabu nyingi hazikuwatii Masultani wa Ottoman, waliwaasi wakaanzisha tawala za kisasa za kiarabu. Hao masheikh fatawa zao ziko wapi kuwaira walioipinga dola ya othmaniyya kuwa walifanya kitendo ambacho si cha kiislamu?
4. Narudia tena, kama huna hadithi au aya inayosema kuwa maandamano yote ni haramu, basi baki na mtizamo wako usiosawa.
Asante sana mkuuDuh ! pole sana na karibu tena jukwaani kiongozi