Mimi sijui unaelewaje kaka kuhusu hizo SAM systems. Labda nikuambie tu hakuna SAM yenye uwezo wa kudhibiti makombora au ndege/drone 100% duniani. Nadhani kama wewe ni mfuatiliaji wa mambo utakua umeona mara ngapi Israeli inaharibu mifumo ya kulinda anga ya Syria ambayo nayo ni ya mrusi.
Cha kujua tu ni kwamba hakuna SAM itakayolinda sehem 100%. Hata S-400 na s-500 SAM ina limit ya targets inayoweza kukabiliana nazo kwa wakati mmoja nadhani 100, kwahiyo yakirushwa makombora 100 kwa ajili ya kuharibu SAM na interception rate yake ni 83% bado makombora 17 yataziharbu.
Kwa Ukraine bado sehem nyingi wana ulinzi wa SAM japo nyingi zimeharibiwa(ambacho sio kitu cha kushangaza sana kwenye vita). Urusi inatumia makombora ya mbali kwa sababu haiwezi kutumia ndege zake kwa uhuru Ukraine bado. Na siku russia wanacontrol anga la ukraine 100% vita itakua imeisha hapo.