Uchambuzi: Jinsi dhana ya "Utatu" na Mungu kuwa na "Mwana" inavyomshusha hadhi Mwenyezi Mungu

Mkono Mmoja

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2019
Posts
4,994
Reaction score
9,625
Ndugu zangu wa JamiiForums, amani iwe kwenu.

Leo nimeona niwaletee mada hii kwa ajili ya tafakari ya kina kuhusu sifa ambazo wanadamu wanampa Mungu. Katika maisha ya kila siku, tunajua kuwa sifa njema ni haki ya Mwenyezi Mungu, lakini ukweli ni kwamba sio kila sifa ambayo wanadamu wanamsifu nayo Mungu inastahili; baadhi ya sifa hizo kiuhalisia ni upotevu na zinashusha hadhi ya ukamilifu wake.

Lengo langu hapa ni kuangazia sifa mbili kuu ambazo ndugu zetu Wakristo wanampa Mungu, nazo ni:
1.Dhana ya Mungu kuwa na Mtoto.

2.Dhana ya Utatu Mtakatifu (kwamba Mungu ana nafsi tatu ambazo zote ni uungu mmoja).

Ukiangalia kwa jicho la tafakari ya kina na kiakili, sifa hizi zinaondoa sifa kuu ya Mungu ambayo ni Upekee na Utoshelevu (Al-Ahad na As-Samad).

Mungu haitaji msaidizi, mshirika, wala mrithi.Mwenyezi Mungu mwenyewe anakanusha kabisa sifa hizi za kibinadamu zilizofanywa kuwa za kiungu. Katika Qur'ani, Surat Al-Mu'minun (23:91-92), ukweli huu unawekwa wazi kabisa pale anaposema:

"Mwenyezi Mungu hakujifanyia mtoto yeyote, wala hakuwa pamoja naye mungu mwengine; (kama ingekuwa hivyo) hapo kila mungu angelichukua viumbe vyake alivyoviumba, na baadhi yao wangewashinda wengine. Mwenyezi Mungu ameepukana na yale wanayomsifu nayo! Mjuzi wa yaliyofichikana na yanayoonekana! Basi ametukuka na yale wanayomshirikisha nayo."

Kwanini sifa hizi ni upotevu kwa mujibu wa aya hizi?

1: Mungu Hana Uhitaji wa Mtoto: Kuwa na mtoto ni sifa ya viumbe wenye ukomo (kama wanadamu) ambao wanahitaji kuendeleza kizazi au wanahitaji msaada wa uzee. Mungu ni wa milele, hafi, na hahitaji mrithi. Kumsifu kwa kuwa na mtoto ni kumshusha hadhi na kumfanya afanane na viumbe vyake.

2: Utatu Unavunja Umoja wa Mungu:
Aya hiyo inasema wazi kuwa kama kungekuwa na miungu wengi au nafsi zenye mamlaka huru ya kiungu, kusingekuwa na mpangilio thabiti wa ulimwengu; kila mungu angetaka kutawala vyake na kusingekuwa na maelewano. Ulimwengu huu unafanya kazi kwa nidhamu moja kwa sababu Mungu ni Mmoja pekee, hana ushirika wa aina yoyote—iwe ni wa nafsi tatu au miungu miwili.

Mwenyezi Mungu ameepukana na sifa hizi ambazo wanadamu wanazitunga kwa kutumia akili zao finyu au falsafa zilizochanganywa. Sifa hizi sio utukufu kwake, bali ni upotevu unaomnyima Mungu sifa yake kuu ya kuwa Mmoja asiye na mfano.

Nawakaribisha jukwaani kwa hoja na staha

karibuni tujadili bila ya matusi wala kebehi.
 
Sio kila sifa watu wanayomsifu Mungu ni sahihi..nyingine ni sifa za upotevu na Mungu anazichukia sana kunasibishwa nazo. Miongoni mwa sifa hiso ni kudai Mungu ana mwana, Mungu amezaliwa, Mungu ana washirika katika uungu wake.
 
"Mungu anazichukia sana!" Anasubiri nini kuwafutilia mbali hao wanaodogosha ukuu wake?
 
Huwezi kuichambua Quran kwa kutumia Bible na huwezi kuichambua bible kwa kutumia Quran.
Ukitaka kuulewa ukristo nenda kabatizwe, vile vile ukitaka kuulewa uislam nenda kasilimu. Hapo ndio utaweza kuutafuta ukamilifu wa imani husika.
 
"Mungu anazichukia sana!" Anasubiri nini kuwafutilia mbali hao wanaodogosha ukuu wake?
Quran 3:178

"Wala wasidhani wale wanao kufuru kwamba huu muhula tunao wapa ni kheri yao. Hakika tunawapa muhula wazidi madhambi. Na yao wao ni adhabu ya kuwadhalilisha."

Quran 14:42
"Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na wanayo yafanya madhaalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatapo kodoka macho yao."
 
Unamkadili Mungu wa wa Kristu kwa jicho la Waislam., hautafanikiwa kwa sababu Mungu wa Wakristu YHWH siyo Allah.
Allah ni mungu wa waarab ndiyo maana kwenye shahada mnasema hakuna mungu isipokuwa Allah...Kama mungu na allah ni sawa hiyo shahada ingekuwa haina maana
 
Asante mkuu! MUNGU ni nani?
Quran 59:22-24

" Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye tu. Mwenye kuyajua yaliyo fichikana na yanayo onekana. Yeye ndiye Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye tu. Mfalme, Mtakatifu, Mwenye salama, Mtoaji wa amani, Mwenye kuyaendesha Mwenyewe mambo yake, Mwenye nguvu, Anaye fanya analo litaka, Mkubwa, Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayo mshirikisha nayo.

Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Muumbaji, Mtengenezaji, Mtia sura, Mwenye majina mazuri kabisa. Kila kilioko katika mbingu na ardhi kinamtakasa, naye ni Mwenye kushinda, Mwenye hikima."
 
Non sense endelea kusujudia kimondo
Quran 41:37

" “Na katika Ishara zake ni usiku na mchana, na jua na mwezi. Msilisujudie jua wala mwezi, bali msujudieni Mwenyezi Mungu aliyeviumba, ikiwa Yeye tu ndiye mnaemwabudu.”
 
Unamkadili Mungu wa wa Kristu kwa jicho la Waislam., hautafanikiwa kwa sababu Mungu wa Wakristu YHWH siyo Allah.
Allah ni mungu wa waarab ndiyo maana kwenye shahada mnasema hakuna mungu isipokuwa Allah...Kama mungu na allah ni sawa hiyo shahada ingekuwa haina maana
Quran 2:163

" Na Mungu wenu ni Mungu mmoja. Hapana mungu isipokuwa Yeye, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.”
 
Siamini Quran ni sawa na ungeniwea nukuu ya Veda.

Vipi hii Surat Al-Kafirun 109:6
For you is your religion, and for me is my religion."
 
Ndugu zangu wa JamiiForums, amani iwe kwenu.

Leo nimeona niwaletee mada hii kwa ajili ya tafakari ya kina kuhusu sifa ambazo wanadamu wanampa Mungu. Katika maisha ya kila siku, tunajua kuwa sifa njema ni haki ya Mwenyezi Mungu, lakini ukweli ni kwamba sio kila sifa ambayo wanadamu wanamsifu nayo Mungu inastahili; baadhi ya sifa hizo kiuhalisia ni upotevu na zinashusha hadhi ya ukamilifu wake.

Lengo langu hapa ni kuangazia sifa mbili kuu ambazo ndugu zetu Wakristo wanampa Mungu, nazo ni:
1.Dhana ya Mungu kuwa na Mtoto.

2.Dhana ya Utatu Mtakatifu (kwamba Mungu ana nafsi tatu ambazo zote ni uungu mmoja).

Ukiangalia kwa jicho la tafakari ya kina na kiakili, sifa hizi zinaondoa sifa kuu ya Mungu ambayo ni Upekee na Utoshelevu (Al-Ahad na As-Samad).

Mungu haitaji msaidizi, mshirika, wala mrithi.Mwenyezi Mungu mwenyewe anakanusha kabisa sifa hizi za kibinadamu zilizofanywa kuwa za kiungu. Katika Qur'ani, Surat Al-Mu'minun (23:91-92), ukweli huu unawekwa wazi kabisa pale anaposema:

"Mwenyezi Mungu hakujifanyia mtoto yeyote, wala hakuwa pamoja naye mungu mwengine; (kama ingekuwa hivyo) hapo kila mungu angelichukua viumbe vyake alivyoviumba, na baadhi yao wangewashinda wengine. Mwenyezi Mungu ameepukana na yale wanayomsifu nayo! Mjuzi wa yaliyofichikana na yanayoonekana! Basi ametukuka na yale wanayomshirikisha nayo."

Kwanini sifa hizi ni upotevu kwa mujibu wa aya hizi?

1: Mungu Hana Uhitaji wa Mtoto: Kuwa na mtoto ni sifa ya viumbe wenye ukomo (kama wanadamu) ambao wanahitaji kuendeleza kizazi au wanahitaji msaada wa uzee. Mungu ni wa milele, hafi, na hahitaji mrithi. Kumsifu kwa kuwa na mtoto ni kumshusha hadhi na kumfanya afanane na viumbe vyake.

2: Utatu Unavunja Umoja wa Mungu:
Aya hiyo inasema wazi kuwa kama kungekuwa na miungu wengi au nafsi zenye mamlaka huru ya kiungu, kusingekuwa na mpangilio thabiti wa ulimwengu; kila mungu angetaka kutawala vyake na kusingekuwa na maelewano. Ulimwengu huu unafanya kazi kwa nidhamu moja kwa sababu Mungu ni Mmoja pekee, hana ushirika wa aina yoyote—iwe ni wa nafsi tatu au miungu miwili.

Mwenyezi Mungu ameepukana na sifa hizi ambazo wanadamu wanazitunga kwa kutumia akili zao finyu au falsafa zilizochanganywa. Sifa hizi sio utukufu kwake, bali ni upotevu unaomnyima Mungu sifa yake kuu ya kuwa Mmoja asiye na mfano.

Nawakaribisha jukwaani kwa hoja na staha

karibuni tujadili bila ya matusi wala kebehi.
Ushauri wangu kwako, endelea kujifunza utatu mtakatifi ni nini, na siku utakapojua nini kipo ndani yake huenda ukatafuta hii comment na ukaikosa. Asante
 
Quran 59:22-24

" Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye tu. Mwenye kuyajua yaliyo fichikana na yanayo onekana. Yeye ndiye Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye tu. Mfalme, Mtakatifu, Mwenye salama, Mtoaji wa amani, Mwenye kuyaendesha Mwenyewe mambo yake, Mwenye nguvu, Anaye fanya analo litaka, Mkubwa, Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayo mshirikisha nayo.

Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Muumbaji, Mtengenezaji, Mtia sura, Mwenye majina mazuri kabisa. Kila kilioko katika mbingu na ardhi kinamtakasa, naye ni Mwenye kushinda, Mwenye hikima."
Asante mkuu! unaposema ni mmoja kwanini kila dini ni tofauti na nyingine kiimani, nani aliyezileta!
 
Ndugu zangu wa JamiiForums, amani iwe kwenu.

Leo nimeona niwaletee mada hii kwa ajili ya tafakari ya kina kuhusu sifa ambazo wanadamu wanampa Mungu. Katika maisha ya kila siku, tunajua kuwa sifa njema ni haki ya Mwenyezi Mungu, lakini ukweli ni kwamba sio kila sifa ambayo wanadamu wanamsifu nayo Mungu inastahili; baadhi ya sifa hizo kiuhalisia ni upotevu na zinashusha hadhi ya ukamilifu wake.

Lengo langu hapa ni kuangazia sifa mbili kuu ambazo ndugu zetu Wakristo wanampa Mungu, nazo ni:
1.Dhana ya Mungu kuwa na Mtoto.

2.Dhana ya Utatu Mtakatifu (kwamba Mungu ana nafsi tatu ambazo zote ni uungu mmoja).

Ukiangalia kwa jicho la tafakari ya kina na kiakili, sifa hizi zinaondoa sifa kuu ya Mungu ambayo ni Upekee na Utoshelevu (Al-Ahad na As-Samad).

Mungu haitaji msaidizi, mshirika, wala mrithi.Mwenyezi Mungu mwenyewe anakanusha kabisa sifa hizi za kibinadamu zilizofanywa kuwa za kiungu. Katika Qur'ani, Surat Al-Mu'minun (23:91-92), ukweli huu unawekwa wazi kabisa pale anaposema:

"Mwenyezi Mungu hakujifanyia mtoto yeyote, wala hakuwa pamoja naye mungu mwengine; (kama ingekuwa hivyo) hapo kila mungu angelichukua viumbe vyake alivyoviumba, na baadhi yao wangewashinda wengine. Mwenyezi Mungu ameepukana na yale wanayomsifu nayo! Mjuzi wa yaliyofichikana na yanayoonekana! Basi ametukuka na yale wanayomshirikisha nayo."

Kwanini sifa hizi ni upotevu kwa mujibu wa aya hizi?

1: Mungu Hana Uhitaji wa Mtoto: Kuwa na mtoto ni sifa ya viumbe wenye ukomo (kama wanadamu) ambao wanahitaji kuendeleza kizazi au wanahitaji msaada wa uzee. Mungu ni wa milele, hafi, na hahitaji mrithi. Kumsifu kwa kuwa na mtoto ni kumshusha hadhi na kumfanya afanane na viumbe vyake.

2: Utatu Unavunja Umoja wa Mungu:
Aya hiyo inasema wazi kuwa kama kungekuwa na miungu wengi au nafsi zenye mamlaka huru ya kiungu, kusingekuwa na mpangilio thabiti wa ulimwengu; kila mungu angetaka kutawala vyake na kusingekuwa na maelewano. Ulimwengu huu unafanya kazi kwa nidhamu moja kwa sababu Mungu ni Mmoja pekee, hana ushirika wa aina yoyote—iwe ni wa nafsi tatu au miungu miwili.

Mwenyezi Mungu ameepukana na sifa hizi ambazo wanadamu wanazitunga kwa kutumia akili zao finyu au falsafa zilizochanganywa. Sifa hizi sio utukufu kwake, bali ni upotevu unaomnyima Mungu sifa yake kuu ya kuwa Mmoja asiye na mfano.

Nawakaribisha jukwaani kwa hoja na staha

karibuni tujadili bila ya matusi wala kebehi.
Upo sahihi sana,wenye imani hii nina uhakika hata wao wenyew inawachanganya sana....lakini pia kwa ukitaka ujue jambo hilo haliingii akilini mchukue mtoto wa miaka 8 au 10 kisha mwambia MUNGU,NI BABA,MWANA NA ROHO MTAKATIFU,afu msikilize huyo mtoto maswali atakayokupiga.

Ndugu zangu Mungu ni mmoja tu,ndiye muumbaji wa kila kitu unavyoviona na usivyoviona...hajazaa wala hajazaliwa na hana yeyote/chochote anachofanana nacho,yeye ni wa pekee.
 
Back
Top Bottom