Uchambuzi: Jinsi dhana ya "Utatu" na Mungu kuwa na "Mwana" inavyomshusha hadhi Mwenyezi Mungu

Uchambuzi: Jinsi dhana ya "Utatu" na Mungu kuwa na "Mwana" inavyomshusha hadhi Mwenyezi Mungu

Asante mkuu! unaposema ni mmoja kwanini kila dini ni tofauti na nyingine kiimani, nani aliyezileta!
ibilisi ndiye chanzo cha hizi njia zote za upotovu...kabla ya hapo Wanadamu wote walikuwa dini moja.

Quran 10:19

" Wala watu hawakuwa ila Umma mmoja tu. Kisha wakakhitalifiana. Na lau kuwa si neno lililo kwisha tangulia kutokana na Mola wako Mlezi, hapana shaka hukumu ingeli kwisha katwa baina yao katika hayo wanayo khitalifiana."
 
Mwenye nguvu, Anaye fanya analo litaka
Kwanini aweze kufanya atakalo halafu nyie mumkataze kuwa na mwana? Nani aliyeamua kuwa hilo aliwezekane na haramu kwake?

Msilisujudie jua wala mwezi, bali msujudieni Mwenyezi Mungu aliyeviumba
Mwezi ni ishara kubwa ili watu waweze kusujudu, angalau naona ikitendeka hivyo, lipo jiwe takatifu linazungukwa na kupewa busu, KUSUJUDU ni kufanya nini?

na hana yeyote/chochote anachofanana nacho,yeye ni wa pekee.
Hakuna sababu ya kukereka na walioamini kuwa UUMBAJI WA MTU NI KWA MFANO WAKE, pambanieni wanaojiita waislamu na hawaujui kabisa huo uislamu.

Wala watu hawakuwa ila Umma mmoja tu. Kisha wakakhitalifiana.
Hitilafu ilianzia wapi? SHIA na (H)AMADIYA ni matokeo ya hitulilafu hiyo?
 
Quran 59:22-24

" Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye tu. Mwenye kuyajua yaliyo fichikana na yanayo onekana. Yeye ndiye Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye tu. Mfalme, Mtakatifu, Mwenye salama, Mtoaji wa amani, Mwenye kuyaendesha Mwenyewe mambo yake, Mwenye nguvu, Anaye fanya analo litaka, Mkubwa, Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayo mshirikisha nayo.

Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Muumbaji, Mtengenezaji, Mtia sura, Mwenye majina mazuri kabisa. Kila kilioko katika mbingu na ardhi kinamtakasa, naye ni Mwenye kushinda, Mwenye hikima."
سبحان الله
Ametakasika Mwenyezi Mungu na wanayomzulia washirikina
Aya kama hizi hutozikuta kwenye kitabu kingine chochote, wala mfano wake.
Na hii ni sababu huwezi kukuta muislam hata layman akibabaika na ukweli juu ya dini yake, hilo wanabaki nalo washirikina na wenye akili isiyo salimika
Hakika Mwenyezi Mungu anamuongoza amtakaye.
 
Ndugu zangu wa JamiiForums, amani iwe kwenu.

Leo nimeona niwaletee mada hii kwa ajili ya tafakari ya kina kuhusu sifa ambazo wanadamu wanampa Mungu. Katika maisha ya kila siku, tunajua kuwa sifa njema ni haki ya Mwenyezi Mungu, lakini ukweli ni kwamba sio kila sifa ambayo wanadamu wanamsifu nayo Mungu inastahili; baadhi ya sifa hizo kiuhalisia ni upotevu na zinashusha hadhi ya ukamilifu wake.

Lengo langu hapa ni kuangazia sifa mbili kuu ambazo ndugu zetu Wakristo wanampa Mungu, nazo ni:
1.Dhana ya Mungu kuwa na Mtoto.

2.Dhana ya Utatu Mtakatifu (kwamba Mungu ana nafsi tatu ambazo zote ni uungu mmoja).

Ukiangalia kwa jicho la tafakari ya kina na kiakili, sifa hizi zinaondoa sifa kuu ya Mungu ambayo ni Upekee na Utoshelevu (Al-Ahad na As-Samad).

Mungu haitaji msaidizi, mshirika, wala mrithi.Mwenyezi Mungu mwenyewe anakanusha kabisa sifa hizi za kibinadamu zilizofanywa kuwa za kiungu. Katika Qur'ani, Surat Al-Mu'minun (23:91-92), ukweli huu unawekwa wazi kabisa pale anaposema:

"Mwenyezi Mungu hakujifanyia mtoto yeyote, wala hakuwa pamoja naye mungu mwengine; (kama ingekuwa hivyo) hapo kila mungu angelichukua viumbe vyake alivyoviumba, na baadhi yao wangewashinda wengine. Mwenyezi Mungu ameepukana na yale wanayomsifu nayo! Mjuzi wa yaliyofichikana na yanayoonekana! Basi ametukuka na yale wanayomshirikisha nayo."

Kwanini sifa hizi ni upotevu kwa mujibu wa aya hizi?

1: Mungu Hana Uhitaji wa Mtoto: Kuwa na mtoto ni sifa ya viumbe wenye ukomo (kama wanadamu) ambao wanahitaji kuendeleza kizazi au wanahitaji msaada wa uzee. Mungu ni wa milele, hafi, na hahitaji mrithi. Kumsifu kwa kuwa na mtoto ni kumshusha hadhi na kumfanya afanane na viumbe vyake.

2: Utatu Unavunja Umoja wa Mungu:
Aya hiyo inasema wazi kuwa kama kungekuwa na miungu wengi au nafsi zenye mamlaka huru ya kiungu, kusingekuwa na mpangilio thabiti wa ulimwengu; kila mungu angetaka kutawala vyake na kusingekuwa na maelewano. Ulimwengu huu unafanya kazi kwa nidhamu moja kwa sababu Mungu ni Mmoja pekee, hana ushirika wa aina yoyote—iwe ni wa nafsi tatu au miungu miwili.


Mwenyezi Mungu ameepukana na sifa hizi ambazo wanadamu wanazitunga kwa kutumia akili zao finyu au falsafa zilizochanganywa. Sifa hizi sio utukufu kwake, bali ni upotevu unaomnyima Mungu sifa yake kuu ya kuwa Mmoja asiye na mfano.

Nawakaribisha jukwaani kwa hoja na staha

karibuni tujadili bila ya matusi wala kebehi.
kabla hujaenda mbali kwanza jibu maswali haya.
Mungu ninini?
Mungu ninani?
kuabudu ni kufanya nini?
then binadamu anafananaje na Mungu? mengina utajibiwa ila sio utakavyo.ila kwa mujibu wa maandiko.
 
Ushauri wangu kwako, endelea kujifunza utatu mtakatifi ni nini, na siku utakapojua nini kipo ndani yake huenda ukatafuta hii comment na ukaikosa. Asante
Quran 4:171
Enyi Watu wa Kitabu! Msipite kiasi katika dini yenu, wala msimseme Mwenyezi Mungu ila kwa lilio kweli. Hakika Masihi Isa mwana wa Maryamu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na neno lake tu alilo mpelekea Maryamu, na ni roho iliyo toka kwake. Basi Muaminini Mwenyezi Mungu na Mitume wake. Wala msiseme: Utatu. Komeni! Itakuwa kheri kwenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja tu. Ametukuka Yeye na kuwa na mwana. Ni vyake Yeye vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mtegemewa wa kutosha."
"
 
Kwanini aweze kufanya atakalo halafu nyie mumkataze kuwa na mwana? Nani aliyeamua kuwa hilo aliwezekane na haramu kwake?


Mwezi ni ishara kubwa ili watu waweze kusujudu, angalau naona ikitendeka hivyo, lipo jiwe takatifu linazungukwa na kupewa busu, KUSUJUDU ni kufanya nini?


Hakuna sababu ya kukereka na walioamini kuwa UUMBAJI WA MTU NI KWA MFANO WAKE, pambanieni wanaojiita waislamu na hawaujui kabisa huo uislamu.


Hitilafu ilianzia wapi? SHIA na (H)AMADIYA ni matokeo ya hitulilafu hiyo?
Kuna Sifa hazimpasi Mungu kuwa nazo..ikiwemo hiyo kuwa na Mwana, kuwa na mke n.k hizi zote ni sifa zenye mapungufu kwake. Ni sawa unasibishe sifa ya ujinga na Mungu, au useme Mungu analala, au Mungu huwa anachoka, Au Mungu huwa anasikia njaa....

hizi ni sifa zenye mapungufu ambazo zote zinakinzana na sifa yake ya UKAMILIFU na UTAKATIFU. Umeeelewa?
 
Kuna Sifa hazimpasi Mungu kuwa nazo..ikiwemo hiyo kuwa na Mwana, kuwa na mke n.k hizi zote ni sifa zenye mapungufu kwake. Ni sawa unasibishe sifa ya ujinga na Mungu, au useme Mungu analala, au Mungu huwa anachoka, Au Mungu huwa anasikia njaa....

hizi ni sifa zenye mapungufu ambazo zote zinakinzana na sifa yake ya UKAMILIFU na UTAKATIFU. Umeeelewa?
..sifa hazimpasi Mungu kuwa nazo...?

UKAMILIFU na UTAKATIFU ni nini?

Ukamilifu na utakatifu huo ni kwa mujibu wa imani au uelewa upi?

Ujinga...si kweli, huwezi kumpa hata mtu unayemuheshimu, sembuse tunayeamini kuwa ni Muumba?

Kulala na kuchoka ni hoja zenu kubwa katika kumpinga Yesu sio?

Sasa, Isa ni nani kwa mujibu wa kitabu cha kikureshi?
  • ni roho, pumzi, maruhani au uchawi wa allah kwa Mariamu?
  • Nani mwingine alipatikana kwa njia hiyo?
  • Nani alipata sifa ya kuumba akiwa duniani?
  • Nani atamuhukumu Muhammad siku ya kiama?
  • Mwanamke yupi ni bora zaidi kuliko wote kwa mujibu wa kitabu cha kikureshi?
  • Qutham ni nani?
  • Wazazi wa Qutham watakuwa wapi muda huu kwa mujibu wa kitabu cha kikureshi?
  • n.k
 
Back
Top Bottom