Nilitegemea vitabu kama hivyo vibebe mambo ya ndani yaliyotokea kwenye uongozi wao ambayo hatuyajui kabisa lakini naona mengi ni yale yaliyokuwa wazi. Kusema Mrema na Mtikila walimsumbua hilo lilijulikana na siyo jipya.
Mfano mzuri wa hilo unalolisema ni kitabu cha Mkapa.
Mkapa kawa serikalini tangu miaka ya sitini.
Tena kawa mhariri wa magazeti ya serikali kwa miaka mingi, kaona mengi.
Wakati Kambona anafarakana na Nyerere, Mkapa ndiye alikuwa mtu wa kwanza kumwambia Nyerere kuwa Kambona anakusema vibaya, kwa kuwa Mkapa alikuwa na waandishi wanaomfuatilia Kambona.
Nyerere hakutaka kumuamini Mkapa, kwa sababu alimpenda sana Kambona.
Mpaka mwishoni Nyerere akajiridhisha.
Lakini, ukitaka kusoma habari hizi, itabidi usome vitabu vya waandishi wa nje kama Paul Bjerk , Thomas Moloney au William Edgett Smith.
Kitabu cha Mkapa hakikuandika ugomvi wa Nyerere na Kambona licha ya Mkapa kujua mengi sana firsthand kuhusu hili.
In fact, hata kwenye mambo yasiyo ya kisiasa Mkapa kashindwa kuwa muwazi.
Katika kutaja watoto wa familia yake, kamtenga Peter, hakumtaja kabisa!