Felix Aweda
JF-Expert Member
- Jun 23, 2012
- 507
- 145
Keep on updating us
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu wataingia roundi ya pili, hapo ndipo uhuru atabwaga na raila.Ndugu zangu,
Afrika ukikuta jogoo wawili wanagombana, basi, hapo hapakosi mashabiki. Na kila shabiki aliyesimama kutazama mpambano wa majogoo hao, ujue, kuwa ana jogoo wake anayemshabikia.
Na jogoo anayemshabikia akishindwa pambano, shabiki ataondoka akisononeka. Kuna ambao watakosa hata hamu ya chakula siku hiyo. Kisa? Jogoo wake kagalagazwa!
Na kama jogoo mmoja ni mnene na mwingine ni mwembamba, ujue, kuwa jogoo mwembamba ana mashabiki wengi.
Ukifuatilia mwenendo wa Uchaguzi wa Kenya kuna dalili kuwa Uhuru Kenyatta ambaye pia anatuhumiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai anaelekea kwenye kupata ushindi.
Moja ya tafsiri ya jambo hili ni ilivyo kwenye fikra za wapiga kura ambao ni wengi ni watu wa kawaida- kuwa Uhuru anaonewa, hata na mataifa ya nje. Kwamba mambo ya Kenya yao yanaingiliwa pia na wasio Wakenya, tena Wazungu.
Wakenya wana historia ya mapambano magumu ya kudai uhuru kutoka kwa ' Wazungu'- ni tangu enzi za Mau Mau.
Pamoja na utajiri wake, bado Wakenya wengi wa kawaida wanamwona Uhuru kama mtu wanayefanana naye. Ni mwanadamu kama wengine. Hujo nyuma Uhuru amekuwa na historia ya matatizo binafsi pia ya kimaisha, ikiwamo matatizo ya pombe, hivyo ya kifamilia pia. Wakenya wengi wanaishi wakijisikia kuwa wananyanyaswa na kuonewa. Wanamwona Uhuru Kenyatta kuwa ni mtu anayeonewa pia.
Hivyo, yawezekana kuna kura za ' kuonewa huruma' ambazo Uhuru Kenyatta anaweza kuzipata, hata kutoka kwa watu wa kabila la Wajaluo. Wanaojiona ' wanafanana naye'.
Na lingine ambalo laweza kutokea ni ukweli, kuwa katika matatizo mengi wanayoyakabili Wakenya kwa sasa, kuna ambao wanaikumbuka ' Bora ya jana' ya Mzee Jommo Kenyatta. Wanaikumbuka historia. hivyo, kuna Wakenya waliopiga kura za ' nostalgie'- Kura za ' Zilipendwa'.
Kuna Wakenya wengi walimpenda Mzee Jommo Kenyatta. Bado wanakumbukumbu za ' Fuata Nyayo'. Na Uhuru naye anaitwa ' Kenyatta'- Jina lake la pili. Ni mwana wa Mzee wa ' Fuata Nyayo.
Naam, Nyayo zilishapotea. Kuna wenye hamu ya kuzitafuta. Wanaamini Uhuru atawasaidia kuziona. Na tusubiri tuone.
Maggid Mjengwa,
Msamvu, Morogoro
Acha fikra za kufanya maisha ya watu majaribio....yaani wewe unataka Uhuru Kenyatta ashinde ili uone itakuwaje ICC??? Vipi maisha ya wakenya kwa miaka mingine mitano??wacha Wakenya wawakomeshe wanafiki na ICC yao. Wacha Kenyatta na arap Ruto washinde ndio tuone test of the ICC laws itakiwaje a sitting president na vice president kama Fatou Mbesuda atawasimamisha kizimbani. Natamani Kenyatta ashinde nione nguvu za ICC.
Mkuu wataingia roundi ya pili, hapo ndipo uhuru atabwaga na raila.
Subirini tume ya uchaguzi itoe matokeo ya jumla. kufanya hivi ni kuchochea hisia kufarakanisha.
Kenya Live Updates: Registered voters 14,410996, Counted votes so far 3,526,332, Uhuru 1,904,528 (54%), Raila 1,458,624 (42%). Turnout 24%
Mkuu mbona Uhuru Kenyatta alisha wahi kuwania Uraisi zaidi ya mara mbili na akashindwa, kama alikuwa anapendwa kupindukia nchini Kenya angeshinda kwenye attempt ya kwanza; mimi nafikili upigaji wa kura wakat mwingine huko highly unpredictable uwezi kujua mpiga kura amehamkaje siku ya upigaji KURA!
Mpaka sasa hivi ni karibu robo tu ya idadi za kura zimehesabiwa, kwa hiyo ni premature kumuhesabu Kenyatta kama mshidi wa kinyangilo hicho - Kumbuka OBAMA kura za mwanzo alionekana vipi? Watu wengi walifikili atashindwa.
...Tujikumbushe...
...Uhuru Kenyatta amegombea kabla Urais mara moja tu, mwaka 2002, akiwa kijana mchanga miaka 4 tu baada ya kuingia Bungeni, hii sasa ni mara yake ya pili wakati Raila Odinga anagombea kwa mara ya tatu sasa, bahati mbaya sana fate yake inalingana na ya Baba yake...
profesa arudi chuoni bado tunahitaji sana vitabu vyake vya sheria.ukishafikia level ya uprofessa unatakiwa kukosoa na kutoa dira tuu ila ukiambiwa wewe uongoze haiwezekaniki ona sasa anagaragazwa na vijanacord wanaanza kupiga mayowe. Nasikia prof. Anyang nyong anapiga yowe
Wale ambao walikuwa na ufahamu wa kutosha enzi za Kenyatta, ningeomba wanipe ABC za Jomo Kenyatta(babae Uhuru) VS Jaramong Oginga Odinga(Babae Raila)