adriz
JF-Expert Member
- Sep 2, 2017
- 12,207
- 26,521
Habari za muda huu wana JF
Baada ya kuibuka hivi karibuni matukio ya viongozi wa dini kulawiti na kupitia michango ya wadau mbalimbali humu kuna mambo nimeona muhimu kugusia.
Inapaswa kutambua kuwa kwa zama hizi suala la malezi na maadili linapitia wakati mgumu mno maana kila sehemu usalama mdogo na ukija kwenye miziki, muvi na mitandao ya kijamii uovu unahamasiswa kwa kiasi kikubwa mara kama kuingiliana kinyume na maumbile, mapenzi ya jinsia moja, Uzinzi nk kwa kiwango kikubwa hivyo wakati huu umakini katika malezi unahitajika sana.
Wiki za karibuni kuliibuka matukio ya Padri kulawiti vilevile kumewahi kuripotiwa matukio ya Shekhe kulawiti inasikitisha sana watu wanaacha kujadili njia bora za kukomesha na kuepukana na haya mambo na kuanza kukashifiana na kutukana na kuzuka vita za kidini wakati matukio hayo yapo katika jamii na binafsi nina amini hakuna dini inayoruhusu hayo mambo kabisa.
Japo vita za maneno zipo kwa watu wa pande zote ila kwa uchunguzi wangu baada ya kupitia nyuzi zote kwa umakini nimeona kuna utofauti mkubwa katika nyuzi zinazohusu Shekhe na Padri kulawiti mifano huu chini.
Na
Mara nyingi nyuzi zinahusu upande mmoja naona mara nyingi unashambuliwa kiasi ambacho uadilifu unakosekana mfano juzi ulianzishwa huu uzi wa Shekhe kulawiti mtoto wa miaka tisa kimara Bonyokwa mtu alianzisha tu bila kutaja majina na chanzo ghafla bila watu kuhoji kama taarifa za kweli au la na kufanya uchunguzi kisha kujadili kistaarabu matokeo yake ikawa tofauti naona uzi umefutwa tokea siku ile sababu nahisi ni taarifa ilikuwa ya uongo
Hapa imhotep alionya
Maoni Yangu Binafsi
Sikubaliani na naomi ya mrangi hapo juu kwani naamini hata mashuleni kuna uhuni mwingi kwa wale tuliosomea shule za kata tutakuwa mashidi maana kule kumezidi lakini hatuwezi kufikia hitimisho la kufuta shule na kutopeleka watoto wetu shule bali katika swala hili ninachokipendeza wazazi wawe wafuatiliaji wa kina kuhusu watoto wao kila siku pamoja kuchunguza na kuwapeleka sehemu bora bila kusahau mamlaka husika kuandaa mikakati bora ya kuziuia na kupunguza matukio kama hayo.
Mimi mwenyewe niliwahi kutoa pendekezo nyumbani kuwapigia marufuku ndugu zangu madrassa fulani walivyokuwa wanasoma niliona uhuni mwingi maana ilikuwa inaruhusu hata watu wa mtaani waje chuo kwa ajili ya kitengo cha madufu sasa hata wengine wahuni walikuwa wanakuja kwa malengo tofauti na nikaona mabadiliko mara wakati wa kwenda chuo kujiremba sana nikatoa tamko kama wanataka kweli kusoma waende madrassa ya kisunni msikiti ninaoswali ambao hakuna kuchanganyika Kati ya wanaume na wanawake ,uhuni ,hata ostazi hawezi kuona sura ya mwanafunzi wa kike na maOstaz wa hapo huwa wanafuatiliwa mienendo yao.
#UziUnaendelea