Habari za muda huu wana Jf..
Baada ya kuibuka hivi karibuni matukio ya viongozi wa dini kulawiti na kupitia michango ya wadau mbalimbali humu kuna mambo nimeona muhimu kugusia.
Inapaswa kutambua kuwa kwa zama hizi suala la malezi na maadili linapitia wakati mgumu mno maana kila sehemu usalama mdogo na ukija kwenye miziki ,muvi na mitandao ya kijamii uovu unahamasiswa kwa kiasi kikubwa mara kama kuingiliana kinyume na maumbile,mapenzi ya jinsia moja ,Uzinzi nk kwa kiwango kikubwa hivyo wakati huu umakini katika malezi unahitajika sana.
Wiki za karibuni kuliibuka matukio ya Padri kulawiti vilevile kumewahi kuripotiwa matukio ya Shekhe kulawiti inasikitisha sana watu wanaacha kujadili njia bora za kukomesha na kuepukana na haya mambo na kuanza kukashifiana na kutukana na kuzuka vita za kidini wakati matukio hayo yapo katika jamii na binafsi nina amini hakuna dini inayoruhusu hayo mambo kabisa.
Japo vita za maneno zipo kwa watu wa pande zote ila kwa uchunguzi wangu baada ya kupitia nyuzi zote kwa umakini nimeona kuna utofauti mkubwa katika nyuzi zinazohusu Shekhe na Padri kulawiti mifano huu chini.
View attachment 2379870
Na
View attachment 2379880
Mara nyingi nyuzi zinahusu upande mmoja naona mara nyingi unashambuliwa kiasi ambacho uadilifu unakosekana mfano juzi ulianzishwa huu uzi wa Shekhe kulawiti mtoto wa miaka tisa kimara Bonyokwa mtu alianzisha tu bila kutaja majina na chanzo ghafla bila watu kuhoji kama taarifa za kweli au la na kufanya uchunguzi kisha kujadili kistaarabu matokeo yake ikawa tofauti naona uzi umefutwa tokea siku ile sababu nahisi ni taarifa ilikuwa ya uongo
View attachment 2379900
Hapa imhotep alionyaView attachment 2379903
Maoni Yangu Binafsi View attachment 2379905
Sikubaliani na naomi ya mrangi hapo juu kwani naamini hata mashuleni kuna uhuni mwingi kwa wale tuliosomea shule za kata tutakuwa mashidi maana kule kumezidi lakini hatuwezi kufikia hitimisho la kufuta shule na kutopeleka watoto wetu shule bali katika swala hili ninachokipendeza wazazi wawe wafuatiliaji wa kina kuhusu watoto wao kila siku pamoja kuchunguza na kuwapeleka sehemu bora bila kusahau mamlaka husika kuandaa mikakati bora ya kuziuia na kupunguza matukio kama hayo.
Mimi mwenyewe niliwahi kutoa pendekezo nyumbani kuwapigia marufuku ndugu zangu madrassa fulani walivyokuwa wanasoma niliona uhuni mwingi maana ilikuwa inaruhusu hata watu wa mtaani waje chuo kwa ajili ya kitengo cha madufu sasa hata wengine wahuni walikuwa wanakuja kwa malengo tofauti na nikaona mabadiliko mara wakati wa kwenda chuo kujiremba sana nikatoa tamko kama wanataka kweli kusoma waende madrassa ya kisunni msikiti ninaoswali ambao hakuna kuchanganyika Kati ya wanaume na wanawake ,uhuni ,hata ostazi hawezi kuona sura ya mwanafunzi wa kike na maOstaz wa hapo huwa wanafuatiliwa mienendo yao.
#UziUnaendelea
Kuna tatizo kubwa la maadili sasa hivi. Watu tunazembea sana katika dini au kuipuuzia kabisa.
Kuna wengine wanaweza kusema kama sababu ni kuzembea katika dini, inakuwaje kuna "masheikh" wanafanya haya na ndio viongozi wa hiyo dini. Bado hoja yangu iko pale pale, ni kuzembea katika dini na kufanya tunachokitaka sisi badala ya kufuata Dini inavyotaka.
Hao "masheikh" badala ya kufuata dini wao wanafuata matamanio ya nafsi zao kama vile watu wengine wengi katika jamii zetu sasa hivi.
Haya matatizo yanatokana na watu kuacha kushika dini kama ilivyo, kuzipuuza Sharia za Allah au kuzifuata kwa matamanio. Na baadhi ya watu, wanaoyafanya matatizo haya, ambao watu wanawadhania ni viongozi wa kiislam kiuhalisia hawako hivyo. Bali ni wahuni ambao hawana elimu kabisa ya Dini lakini wamevikwa "vilemba" vya Uongozi wa Dini. Au Wengine wana elimu lakini hawajashika Dini (hawafuati), wako mbali na mwenendo wa Mtume na ni watu wanaofuata matamanio yao. Badala ya kufuata Dini wao wanafuata mkumbo na kusombwa na upepo wa watu wajinga waliojaa katika jamii.
Uislam unakataza mambo machafu yanayofanyika katika jamii zetu, tena unayakataza vikali mno. Hivyo watu kuuhusisha Uislam na machafu haya, kwa sababu eti baadhi ya watu wanaoyafanya wana sura ya dini, ni dhulma. Kwa kuwa haya mambo hayapo katika Uislam na yanapigwa vita na kupingwa vikali, basi wanaoyafanya wanayatoa nje ya Uislam. Haya machafu hayajaletwa na Uislam.
Machafu haya (ya zinaa na liwati) yanapigiwa chapuo katika jamii kupitia miziki, mafilamu, vyombo vya habari na watu wengine wanaoyatangaza wazi. Na baadhi ya wahuni wanayabeba katika jamii bila kujali, na inapotokea yakapingwa baadhi ya watu hao watayatetea kwa nguvu kwamba yaachwe yafanywe, tusiwahukumu, na wakatazaji wanakejeliwa. Ndio matokeo yake haya yanatokea ya watoto kuharibiwa na baadhi ya watu kutoka jamii hiyo hiyo ya wahuni ambao baadhi yao (hao wahuni) wamejificha katika Dini, halafu baada ya kutokea hayo madhara baadhi ya watu hao hao katika jamii na wajinga wengine wanaopinga Dini wanalaumu Dini eti ndio zimesababisha.
Solution ni matendo haya machafu yapingwe vikali kwa watoto na wakubwa na watu wahimizwe kurudi katika Dini kwa kusoma Elimu (Dini) ya sawa sawa (Qur'an na Sunnah juu ya ufahamu wa Salaf) na kuufuata na wala sio kuhimizwa kuikimbia Dini (Uislam). Na watu wahuni wasipewe nafasi ya kuvaa "vilemba" vya usheikh.
Mwisho niseme haya mambo ya watoto kubakwa na kulawitiwa yanaonesha ishara ya kuharibika kwa jamii zetu.
Mchango wangu ndio huo. Mapungufu yoyote ya uandishi na mtiririko wa hoja ni katika upungufu wangu wa kibinadamu. Ukamilifu na Ujuzi wote ni wa Allah.
Allah atunusuru sisi na vizazi vyetu kutokana na machafu haya na athari zake.