Uchambuzi: Mambo ya msingi kabisa ya kuyatambua kuhusu mgogoro wa wapiganaji wa M23 na Congo DRC na mapendekezo ya nini kifanyike

waafrika na viongozi wake wanakosea sana wanapotaka kuifuta mipaka ya Berlin ya 1884-85, lazima tujifunze kuishi kwenye hii mipaka otherwise hatutawahi kuwa na amani hata siku moja, vitaifa vy africa vilikuwa vidogo vidogo visivyo na centralize goverments.

Rwanda na Uganda Lazima waache tamaa na kulitambua hili, otherwise baada M23, Congo, South Africa na Tanzania itawafungulia na kuwaachia Silaha Wahutu wa FLDR
 
Mkuu, wataalam husema kiini cha tatizo au kwa kiingereza "central to the problem" ni Goma.

Afrika kwa sasa khasa Congo DRC haiwezi kuachiwa ikae kihasara kutokana na uwingi wa madini yaliyopo pale.

Nchi zote za kibepari kuanzia Marekani, Uingereza, Ufaransa, Australia, Canada na zingine zote zina makampuni yao pale.

Huo mji wa Sake sasa hivi una wageni wengi wanojaribu kukimbia kisanga cha M23 ambao sasa wapo karibu.
 
Dawa ni kuivamia Rwanda kijeshi, hayo yote yatakoma.

Wapelekwe wanajeshi laki 5 kutoka Congo Dr, Tanzania, Zimbabwe na SA.
Wakifanya hivyo, milele hakutakuwa na vita ukanda huo.
wanajeshi laki 500,000 kwa population ya rwanda itakua mwanajeshi mmoja kwa kila raia 28 hakuna haja ya bunduki hapo ni marungu tu maana katika hao raia 28 majority ni wazee wanawake na watoto
 
Rwanda inataabika sana na huu mgogoro kuna Wakimbizi wengi wa Kinyamulenge Congolese Tutsis wako kwenye Makambi ya UNHCR ndani ya Rwanda.

Ili huu Mgogoro uishe Serikali ya DRC irudi Mezani na iache kuchochea Mauaji ya Kimbari dhidi ya Raia wake wa Kitutsi iache kuchonganisha Watu wake.

Kongo ilimegwa na Mfalme Leopold wa Ubelgiji hiyo Mipaka iliwekwa na Mkoloni huyo leo ukiamua kuwavua uraia kwa misingi ya Kikabila migogoro haiwezi kuisha.

Hata ukileta Majeshi kutoka Sayari ya Mars.
 
Hawa ni vijana wa kagame hivo tu. Kagame anataka Kivu kaskazini iwe sehemu ya Rwanda ndo maana vita haiishi
 
Lakini mgogoro huu kati ya wapiganaji hawa wa M23 na serikali ya Congo DRC waweza kutatuliwa endapo Serikali ya Congo DRC itaamua kumeza risasi na kuwaachia M23 wawe na Kivu yao ambayo ndo sehemu ya walipozaliwa baba zao na mama zao.
Hili haiwezekani, halafu hao M23 ni kivuli tu cha jeshi la Rwanda liliovamia Drc.
 
Mie nina swali moja tu,
Kama ni watutsi kwanini Kagame asikubali kuwapokea Rwanda na kuwafanya raia wa Rwanda badala ya kuwasaidia mapigano?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…