Kitabu.Mossad
Mwandishi.Michael Bar Zohar & Nissim Mishal
Mchambuzi.Nanyaro EJ
Sehemu ya 9
OUR MAN IN DAMASCUS
Mwandishi anaanza kwa barua hii ….Mpenzi Mke wangu Nadia,nakuandikia haya maneno machache nikitarajia kuwa utabaki salama,naomba unisamehe na jitahidi kumsomesha mtoto wetu apate elimu bora,Mpenzi wangu Nadia kama itakupendeza unaweza kuolewa tena na mwanamume utakayempenda wewe,ili watoto wetu wawe na malezi ya Baba,nakuomba sana usiomboleze juu yangu wala usitazame ya nyuma,bali songa mbele.Niombee kwa mola.Wako Elie
Hii ni barua ilifika ofisi za Mosad Mei 1965,kutoka kwa jasusi bobevu la wakati wote Elie Cohen,aliandika barua hii dakika chache kabla ya kunyongwa Jijini Damascuss akiwa na mikono inayotetemeka…kwenye kifo hakuna jasusi
Maisha ya usiri wa hali ya juu ya Elie Cohen yalianza na kudumu kwa miaka Zaidi ya 20.Huyu jamaa alikuwa mzayuni aliyekulia nchini Misiri,ambako alifanya kazi ya ujasusi akafanikiwa kupenya kwenye vyombo vya ulinzi na usalama ambako aliajiriwa
Kufuatia Syria kuanza kuwa adui wa Israel Mossad waliagiza Uniti 131 kuanza operesheni maalum yenye lengo la kujua na kutambua mipango yote ya Syria,ambayo ilianza harakati za kutaka eneo la Golan Heightes pamoja na kugawa maji ya mto Jordan,chanzo muhimu cha maji kwa nchi ya Wazayuni hivo Elie Cohen alipewa jukumu hili zito,kabla ya kupewa kazi hii alifanyiwa mafunzo maalum ikiwepo,jinsi ya kuwa na kumbukumbu bila usaidizi
Somo la mwisho kwa huyu Elie Cohen ilikuwa kupewa passport ya Misiri akatakiwa aseme kuwa yeye ni Mmisiri aende Jerusalem kwa siku kumi,ndani ya hizo siku kumi atengeneze mtandao wake,marafiki,alipaswa aongee kifaransa na kiarabu tu,na kuwa ajitambulishe kama mtalii kutoka Misri amekuja kutembea.Alipaswa asijulikane kwa utambulisho wake halisi na ahakikishe kuwa hakuna mtu anamstukia wala kumfuatilia.Alihitimu vizuri baada ya siku kumi kisha ikafuatiwa na kufunzwa masomo Fulani ya Kurani takatifu…baada ya haya alipaswa kusafiri kwenda nchi Fulani nje ambako alipaswa aishi kama Mwislamu na ategeneze mtandao wake,sasa basi huyu Elie Cohan alibadilishwa jina na akaitwa Kamal Amin Tabet,mama yake mzazi ataitwa Saida Ibrahim na alikuwa na dada ambao wametangulia mbele ya haki,walizaliwa Beirut nchini Lebanon na alipokuwa na miaka mitatu wazazi wake walihamia Alexandria nchini Misiri.Wazazi wake wote wawili ni kutoka nchini Syria,Mjomba wako alihamia nchini Argentina 1946 na mwaka mmoja baadae 1947 mjomba aliwakaribisha wazazi wako nchini Argentina ambako walipata fursa ya kufungua kiwanda kidogo cha ushonaji,hata hivo kilifilisika na baba kufariki kutokana na stress za maisha,miezi sita baadae mama yako alifariki kwa msongo wa mawazo,hivo mjomba wako aliendelea kukulea.Baadae ulipata kazi kwenye shirika moja la usafirishaji kisha ukajiajiri baadae sana na ukafanikiwa.
Mwandishi anasema kuwa Bwana Elie Cohen aliporejea nyumbani kwake alimwambia mkewe kuwa amepata kazi kwenye kamouni binafsi inayofanya kazi na wizara ya mambo ya nje na hivo wamemwajiri na atakuwa anasafiri ulaya mara kwa mara na wakati mwingine kukaa huko kwa muda…hii Kamba mke alielewa maana sasa maisha yalikuwa yanabadilika na mumewe angelipwa fedha za kutosha….
Mto Jordan ndio uti wa mgongo wa Taifa la Israel,bila mto Jordan Israel haiwezi kuishi
Mwaka 1961 Elie Cohel alisafiri akiwa na passport yake halisi kwenda Zurich ambako alipokelewa na mtu ambaye alimpatia passpot ingine ya nchi ya Ulaya ikiwa na viza ya nchi ya Chile na Argentina.Siku iliyofuata alisafiri tena kwenda Argentina na alipewa anuani ya mahali pa kufikia,alipofika alipokelewa na kupewa utambulisho mpya sasa wa Kamali
Miezi mitatu baadae Elie alikuwa amejifunza Spanish,na alikuwa analijua kila kichochoro cha Jiji la Buenos Aires,na aliishi kama raia kutoka Uarabuni.Hapa alipaswa sasa kuanza kutembelea migahawa na vijiwe ambavo waarabu walipendelea,na kutakiwa kutengeneza marafiki na mtandao mkubwa kwa kadri awezavyo.Hii ilikuwa rahisi maana Mossad walimjaza hela za kutosha hivo alikuwa analipa bill na kutoa mchango wa fedha sana kwa jamii ya watu kutoka uarabuni,yaani alijifanya mwarabu hasa
Mossad walimfungulia kampuni ambayo yeye ndio alikuwa mkurugenzi,na kupitia kampuni hii akaanzisha mfuko maalum kwa ajili ya kusaidia jamii ya waarabu.Kufuatia kujiamini kwake,ucheshi na ukarimu wake haikuchukua muda akajikuta mtu muhimu sana kwenye jamii ya waarabu,na aliaminika sana.Bwana Elie aka Kamali alikuwa mtu mwenye akili nyingi sana,mbele ya macho ya Wasyria walioishi Argentina alionekana kama shujaa na mzalendo,siku moja alifika Ubalozi wa Syria nchini Argentina ambako alishatengeneza mtadao wake na kuomba apewe barua ya utambulisho ili arejee nchini kwao ambako anaipenda sana maana hakumjua mtu yoyote.Ubalozi haukusita wala kuwa na wasiwasi nae,akaandikiwa barua za utambulisho kwenye vyombo mbalimbali nchini Syria
Mwisho wa mwaka 1961 Elie aka Kamali alipanda ndege kwenda Zurich kisha Munich,ambako alikutana na Mossad wakampa tiketi na passpot ya Israel ili arejee kwanza nchini kwao kwa muda mfupi.Kipindi hii alikitumia kusoma saana kuhusu silaha za Syria,jeshi lake,mfumo wake wa mawasiliano jeshini etc.Alirejea Zurich kisha kupanda ndege ya kwenda Damascuss
Wakati anafika Damascuss uhusiano na Israel ulikuwa tete sana
Sasa basi Elie Cohen alipewa kila aina ya vifaa kuanzia redio maalum,hadi vidonge vya kujiua ikibidi kufanya hivo.Alifanikiwa kuingia nchini huko kwa msaada wa rushwa,kwa kuwa alitaka kujulikana mapema aliamua kutafuta apatmenti nzuri jirani na makao makuu ya jeshi la Syria,aliamini akiishi eneo hili atakuwa salama na hakuna mtu atakuja kukagua apartment iliyo jirani na makao makuu ya jeshi.Sasa zile barua za utambulisho alizopewa nchini Argentina alizitumia vizuri sana,ndani ya muda mfupi alikuwa ameweza kupenya kwenye chama tawala,ambako alitoa msaada wa fedha,na kwa maofisa kadhaa wenye ushawishi serikali…alionekana kijana mwenye mafanikio makubwa na anayependa nchi yake na watu wake,aliendelea kutoa misaada kwa watu maskini katika jiji la Damascus.Wakati akiendelea kujipenyeza ndani ya serikali alitumia pia muda huo kuseti mitambo yake,alifunga transmita iliyoingilia mawasiliano ya jeshi na kuyapeleka nchini Israel makao makuu ya Mossad,mitambo hii aliifunga kwenye moja ya vyumba katika apartment yake aliyokuwa ameinunua,hapo jirani na makao makuu ya jeshi la Syria
Mwandishi anasema kuwa ilitokea kama ngekewa mwaka 1963 yule jamaa aliyekuwa amewambdikia barua za utambulisho bwana Kamali nchini Argentina,alikuja kuteuliwa Waziri wa Ulinzi wa Syria,huyu alikuwa rafiki binafsi wa Kamali,ndio kusema sasa mossad walikuwa na mtu ndani kabisa ya yaani inner circle of power.Kamali akaanza kutengeneza sherehe na hafla mbalimbali nyumbani kwake,na kuwaalika majenerali wa jeshi pamoja mawaziri,,unaambiwa hapo nyumbani kwake magari ya kifahari ya wakubwa na wafanyabiashara maarufu yalikuwa hayakauki..alifuata ile falsafa ya magharibi …kuwa mweke rafiki yako karibu nawe ila adui yako mweke karibu Zaidi….Kamali alikuwa anawanunulia hadi zawadi za gharama kubwa.Kamali akawa mtu ndani ya Syria na akaanza kukaribishwa kwenye vikao vikubwa vya chama tawala kisha baadae akawa miongoni mwa watu wanaotoa ushauri kuhusu mambo ya uchumi ndani ya serikali
Kwa kuwa alikuwa ndani ya serikali alipata taarifa zote za kijeshi ambazo alizipeleka Israel kwa njia ya Transmita maalum,yaani kila siku alirusha transmita kupeleka taarifa sahihi.Kamali alifanikiwa kuaminisha jeshini kuwa anaichukia Israel kwenye mazungumzo yake,hii ilifanya aaminiwe na majeneral wakawa wanamtembeza kwenye kambi mbalimbali za kijeshi hata zile ambazo hakuna raia anaruhusiwa kufika…yaani Syria wakawa wanamwachia fisi bucha……
Pamoja na Udhaifu wa Syria lakini walingamua kuwa kuna jinsi taarifa zao zinavuja,walijua sasa wanauzwa,ila nani anawauza? Waligundua kuwa tangu mwaka 1964 kila uamuzi uliofanywa na Syria usiku au mchana ulikuwa unatumwa kwa lugha ya kiarabu nchini Israel,sasa wakaagiza shirika lao la siri Mukhabarat liingie kazini.Syria walijikuta wapo uchi mbele ya Wazayuni,hata uamuzi uliofanywa na watu watatu bado Wazayuni waliupata.Walihangaika kutafuta hii transmita kwa miezi sita bila mafanikio ila sasa walitambua tu kuwa kuna transmita swali likawa itakuwa wapi?
Syria walilazimika kuzima mitambo yote jeshini nchin nzima ili kutafuta hii transmita,ofisa aliyekuwa zamu aligundua mawimbi ambako walianza kutafuta yanarushwa kutoka wapi.Kabla ya kufika haya mawimbi na transmita vilizima ghafla ikawa kazi tena,,ila angalau walikisia eneo ambalo ni nyumba ya bwana Kamal,ofisa alishindwa kukubali kuwa bwana Kamali ambaye alitarajiwa kuteuliwa waziri kwenye baraza lijalo angeweza kuwa jasusi.Jioni ya siku hiyo ile transmita iliendelea na sasa waliamua kuvamia jengo la kifahari la bwana Kamali…katika hali ya kutoamini macho yao walimkuta bwana Kamali akiwa anafanya kazi yake ya kupeleka taarifa,akiwa na vifaa vyake,vifaa vya kila aina…yalikuwa maajabu hakuna aliyeamini,milionare,rafiki wa Rais,rafiki wa chama,mtu makini mwenye upendo anawezaje kuwa msaliti?ilikuwa ngumu kuamini lakini ushahidi ulikuwa wazi…ilibidi hata Rais aje amhoji,Rais wa Syria wakati huo alinukuliwa akisema alipomwangalia kwa makini akiwa selo aligundua kuwa huyu sio mwarabu bali ni Mzayuni…alishinndwa kutaja hata sura ya kwanza ya kurani…..
Taarifa za kukamatwa kwa Bwana Kamali,tajiri zilienea kama moto wa kifuu na hakuna aliyeamini
Akiwa kizuizini Kamali alipata kila aina ya mateso yampasayo Msaliti,aliteswa na kichapo cha kila aina hapa Duniani,alingolewa kucha,baada ya mateso makali alikiri kuwa hakuwa Kamali Tabet bali aliitwa Elie Cohen,haraka sana Damascuss ilitangaza kumkata jasusi wa Kizayuni.Watu 400 walihojiwa na 70 walikutwa na kesi ya kujibu,kitu cha ajabu ni kuwa robo tatu ya wanasiasa wa chama tawala cha Syria walikutwa walikuwa watu wa karibu sana na Elie,wapelelezi walishindwa kuwataja au kuwahoji kwa kuwa nchi ingepasuka vipande vipande
Serikali ya Israel iliamua kujaribu kumsaidia Elie hivo waliajiri wakili bora na maarufu kutoka Ufaransa kwa niaba ya familia.Wakili anasema alipofika tu Damascuss aligundua ameshashindwa tayari.Mamlaka za Syria zilihofia kuwa akiruhusiwa kupewa wakili ataeleza kila kitu mahakani hivo iliamuliwa kuwa hakuna mtu yoyote kuruhusiwa kumwona wala huduma ya wakili.Bwana Elie alipelekwa kwenye mahakama ya kijeshi ambako hakuruhusiwa kujitetea wala kusema chochote,alipoomba kuwa anahitaji wakili jaji akamjibu kuwa“You don’t need a defender.All the corrupt press is on your side, and all the enemies of the revolution are your defenders.” Huyu Jaji ambaye kabla alikuwa rafiki wa karibu wa Elie alikuwa Jenerali wa jeshi.Hii ndio kesi pekee ambayo Jaji alikuwa ndio yeye Mwendesha mashtaka,ndio yeye mjibu mashtaka,ndio yeye mlalamikaji na ndio jaji.Moja ya kichekesho kwenyen hili shauri ilikuwa swali ambalo Jaji alimwuliza mshtakiwa..(kimsingi walifahamiana sana na jaji alikuwa na hofu) akamwuliza unamfahamu jaji akataja jina lake..yeye Elie akamjibu hapana simwoni hapa chumbani…..
Jitihada kadhaa za Israel ikiwepo kutoa madawa pamoja na teknolojia ya kilimo,vyenye gharama ya mamilioni ya dola vilikataliwa….Israel ikatoa ofa ya pili ya kuwaachia majasusi 11 wa Syria waliokuwa wameshikiliwa nayo ikakataliwa…..mwisho Israel ikwatumia viongozi wakubwa akiwepo Pope Paul VI Mwanafalsafa wa Uingireza Bertrand Russell;Malikia wa Ubeligiji,wabunge 21 wa Uingereza na watu wengine wengi lakini haikufua dafu….walikataliwa
Mwisho alinyongwa na kabla ya kunyongwa alipewa fursa ya kuandika barua kwa famila yake.Ndiyo ile barua mwanzoni kabisa.Kifo chake cha kunyongwa kilirushwa mubashara kwenye TV zote za Syria
Hadi leo ndani ya Mossad Elie Cohen ni moja ya watu mashuhuri kabisa na wanaamini kuwa alikufa kifo ambacho wakala makini huwa wanakufa.