Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ngoja na mimi.niitafuteNimeangalia season yake Cohen inashangaza Sana.
HutojutiaNgoja na mimi.niitafute
Kitabu.Mossad
Mwandishi.Michael Bar Zohar & Nissim Mishal
Mchambuzi.Nanyaro
Chapter 14
“TODAY WE’LL BE AT WAR!”
Mwandishi anasema kuwa kijana mmoja mtanashati aliingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na binti wa Rais Nasser wa Misri.Kijana huyu aliitwa Ashraf Marwan alikuwa kijana anayependa anasa mno,aliishi maisha yasiyokuwa yake.
Baada ya kumwoa binti wa Rais aliomba kwenda London kuendelea na masomo,akiwa London alikula fedha zote,na akajikuta anakuwa Marioo,alijiingiza kwenye uhusiano wa mapenzi na binti kutoka Kuwait ambaye alimsaidia kupata ela ndogo ndogo,uhusiano mpya ulivuja na serikali ya Misri ikamrejesha Cairo,Rais Nasser alichukia mno na kumtaka Binti yake aachane na mzinzi…binti aligoma ikabidi Bwana Ashraf Marwan atakiwe kubaki nchini Misri na angeenda London wakati kuwasilisha ripoti kwa profesa wake tu!
Mwandishi anasema kuwa wakati Fulani bwana Ashraf alirejea London kuwasilisha ripoti,akiwa London alipiga simu ubalozi wa Israel nchini Uingereza na kujitambulisha kwa majina yake na akaomba kufanya kazi na Israel,baada ya kuchunguzwa wazayuni walikubali na kumpa jina code ya Angel…Mossad walikuja kutoa jina lake halisi mwaka 2004 miaka mingi baadae,inaaminika kuw huyu bwana ndio alikuwa double agent mkali zaidi na ambaye aliweza kuwafurahisha mabwana zake vizuri yaani Israel na Misri
Bwana Ashraf Marwan alikuwa na kinyongo na Baba mkwe wake,akaamua kumwaga mboga baada ya baba mkwe kumwaga ugali.Mossad walimpa kazi na mara moja wakampa ofa ya USD 100,000(kama milioni mia mbili na thelathini tshs) hii ilikuwa mwanzoni mwa miaka ya 1970.Wakati huu Nasser alikuwa amempa kazi mkwewe katika ofisi ya Rais.Ili kuonyesha kwa mossad kuwa anaweza kupata taarifa muhimu aliwapelekea Mossad muhutasari wa kikao cha Misri na USSR walichokaa January 22,1970,jijini Moscow ambako Misri waliomba wapewe silaha za kisasa na za masafa ya kati,na ndege ambazo zingeweza kufanya shambulizi ndani ya Israel.Baada ya kuchunguza waligundua huu ni muhutasari genuine usiokuwa na chembe ya mashaka!hapa mossad walifurahi kuwa wana hazina mkono mwao
Mossad walitengeneza watu wawili (watu kati) ambao ndio wangepewa taarifa watu ambao walikuwa sleeping agents wao..Bwana Ashraf aliwapa siri za kisiasa,kijeshi na kiuchumi za taifa la Misiri,ni wazi Misiri ilikuwa tupu mbele ya Wazayuni,kila walichopanga kilifika mkononi kilivo
Ashraf Marwan aliigharimu Israel kiasi cha usd 3mill(Dola milioni tatu)
Baada ya kifo cha Nasser baba Mkwe wa Ashraf,aliridhiwa na Sadat,bwana Ashraf alichanga karata vizuri na kujikuta amefanywa msahuri maalum wa rais wa mambo ya usalama,hivo akawa anaambatana na Rais kwenye vikao muhimu vya ndani na vya kikanda,kwa Mossad ilikuwa faida kubwa maana walikuwa na mtu ndani ambaye anatoa taarifa za nchi nyingine za kiarabu,kwa kadri Bwana Ashraf alivoaminiwa na Serikali ya Misri ndivo wigo wa kupata taarifa kwa Mossad ulivoongezeka!
Ashraf akaingia tamaa akaanza kuuza siri kwa wakala wengine wa siri,yaani aliamua kuwa wakala kwa mashirika mengine kwa siri,bila shirika A kutambua….mwandishi anamwelezea kama a real double agent.Kwa mujibu wa CIA aliwatumikia kwa miaka zaidi ya 20.Mwisho kabisa Ashraf aliamua kustaafu mambo ya Espionage…baada ya kustaafu alianzsisha biashara London ikiwepo kununua sehemu ya Chelsea mwanzoni mwa miaka ya 2000,alikuwa mmoja wa Wamisiri waliokuwa na nguvu pale London akiwa pamoja na Baba yake Diana,anayemiliki store maarufu ya Harrods na timu ya mpira ya Fullam.
Kwa kuwa hakuna siri Duniani Misri walikuja kugundua baadae sana kuwa Asharaf alikuwa double agent,hivo wakamlia timing akiwa barazani kwake kwenye jumba la kifahari London wakamwua!(Adhabu ya kuifanyia ujasusi nchi yako ni kifo)
Ukitulia utaelewa content kwanza kumbuka hiki kitabu ni taarifa za Mosaad ambazo zimekuwa classfied na kutolewa kwa umma,kwa malengo ambayo Mossad tu ndio wanajuaKuna sehemu sijakubaliana na huyu mchambuzi, pale anaposema eti mossad walitoa hadharani jina la Ashraf Marwan (The angel).
Kwenye hiki kitabu inaonyesha alieanza ku-hint kuhusu jina halisi la the angel ni mwandishi wa vitabu Aharon Bergmann na baadaye mkuu wa kitengo cha ushushushu wa jeshini (Aman) aliyeondolewa kufuatia kupuuzia taarifa ya vita, akathibitishq haradhan kwamba ni kweli the angel alikuwa ashraf marwan.
Kwenye hiki kitabu, hakuna sehem wameonyesha kama hawa walikuwa sehem ya mossad.
Ukitulia utaelewa content kwanza kumbuka hiki kitabu ni taarifa za Mosaad ambazo zimekuwa classfied na kutolewa kwa umma,kwa malengo ambayo Mossad tu ndio wanajua
Sasa hivi Mossad naijua kuliko hata TISS
Hahahaha ,kwani hakuna maandishi ya matukio ya hao jamaa
Na ndo maana halisi ya Secret Service. Mission na Kazi zake za Kiusalama zinatakiwa zifanyike kwa siri na kificho. Raia wa kawaida hawatakiwi hata kujua hata jina la Secret Service Agency linaitwaje.Uyatolee wapi wanafanya matukio kwa uficho sana
[emoji23][emoji23][emoji23]Hawa mawakala wa ujasusi kwenye mafunzo yao wanafundishwa na somo la kutongoza. Kumtongoza naibu waziri akukubali akupe siri na kitumbua chake, si mchezo.
Naitafuta ila jitihada zangu zimegonga nanga ssa kama una link plz naombaNimeangalia season yake Cohen inashangaza Sana.
Kitabu.Mossad
Mwandishi.Michael Bar Zohar & Nissim Mishal
Mchambuzi.Nanyaro EJ
Chapter 6
“BRING EICHMANN DEAD OR ALIVE!”
Mwandishi anasema kuwa mwaka 1957 walipokea ujumbe kutoka Frankfurt kuwa mjerumani mmoja aliyeheshimika sana Dr Fritz Bauer alitaka kutoa taarifa nyeti kwa Mossad.Fritz alikuwa mjerumani mwenye asili ya Israel ambaye aliwekwa kwenye kambi za mateso kabla ya kutoroka,baadae akawa mpinzani mkubwa wa sera za chama cha Nazi
Huyu dr Fritz alirejea Ujerumani baada ya anguko la Hitler na alikuwa msitari wa mbele katika kuhakikisha wote walioshiriki wanafikishwa mbele ya sharia,hata hivo hakuridhishwa na jinsi mamlaka za ujerumani zilivoshughulikia swala zima.
Sasa basi huyu Dr Frits alikuwa na taarifa nyeti,ambayo aliiwasilisha Mossad kuhusu bwana Eichmann,bwana Eichman alikuwa mchinjaji na muuaji maarufu wakati wa Hitler,na baada ya anguko la Hitler alikimbilia Argentina.Ni kwamba baada ya Hitler kujiua Israel ilianzisha operesheni ya siri sana kwa lengo la kulipiza kisasi kwa wahusika wote walioshiriki kuwaua wayahudi wenzao.Na wengi wa wafuasi wa Nazi walikimbilia Argentina wakabadili majina na mfumo mzima wa maisha.Hivo basi bwana Frits alitoa taarifa za sehemu anakoishi Eichman kufuatia kujulishwa nab inti yake ambaye alikuwa anaishi huko sasa Mossad wakaanzisha rasmi operesheni ya kumkamata na kumrejesha Eichman nchini kwao akiwa hai au mfu.Mossad walianza operesheni hii kutafuta hasa kama kweli Eichman alikuwa bado anaishi baada ya upepelezi wa muda mrefu waligundua kitongoji ambacho alikuwa anaishi akiwa na jina lingine na utambulisho tofauti kabisa ambao ilikuwa sio rahisi kugundulika
Sasa basi Mossad walimpa kazi jasusi mmoja aliyeitwa Ahoron alikuwa kijana mdogo mwenye akili nyingi,alifika Argentina katika jiji la Buenos Aires,hapa aliweza kupata taarifa za sehemu bwana Eichman alikokuwa anaishi,na jina jipya alilojibadilisha alikuwa anaitwa Ricardo Klement,baada ya kufika mtaa walikoelekezwa walikuta nyumba ikiwa haina mtu ni gofu,hapa ilibidi sasa wao Mossad waende kwenye wakala wa kupeleka vifurushi wakatengeneza zawadi ya na kumtaka wakala awasilishe kwa muhusika,hii kampuni ya uwakala ikaanza kazi ya kutafuta makazi ya Bwana Eichman (Ricardo) na baada ya siku mbili wakafanikiwa kupapata na kumkabidhi mzigo wake,wakati wote agenti wa siri wa Mossad alikuwa nyuma kumfuatilia yule wakala wa kusambaza zawadi.Sasa baada ya kupata nyumbani kwa bwana Ricardo yule Jasusi alifika hapo kesho yake akiwa amevalia suti ya kimarekani ambako alijitambulisha kama mfanyabiashara kutoka kampuni moja kutoka USA na wanataka kuwekeza kiwanda hapo,hivo wanataka kununua eneo lote hilo kwa matumizi yao,wakati akijieleza alikuwa na camera ndogo ambayo haikuonekana akawa anapiga picha mbalimbali maeneo hayo,yule jirani akajibu kuwa hawatauza ila ngoja aongee na familia yake kesho yake angetoa majibu.Bwana Ahoron Jasus wa Mossad alirejea alikofikia na kwa kutumia uzoefu wake aliingiza zile picha kwenye mfumo wa masjila ya mji wa Buenos Aires ambako ilionyesha kuwa ni eneo binafsi mali ya Ms.Vera Liebl de Eichmann,huu ubini ukawa moja ya kielelezo muhimu kuwa mwenye nyumba ni ndugu na Ricardo mtu wanayemtafuta>Baadae walikuja kugundua kuwa Vera ni mke wa Eichman ingawa walishaachana kitambo ila kwa tamaduni za Argentina bado mke ataendelea kutumia ubini wa mumewe.
Mwandishi anasema kuwa baada ya kugundua makazi haya ilitumwa timu ya watu 12,ili kumkamata na ilipendekezwa akamatwe na apelekwe Israel akiwa hai yaani alikuwa na dhamani kubwa akiwa hai kuliko akiwa mfu.Mossad wana tabia ya kuingia kwenye nchi nyingine kijasusi na mar azote hutokea nchi jirani…huwa na paspoti za mataifa mengine ili kuficha utambulisho wao,na huingia kama watalii au wawekezaji.Sasa hawa watu 12 wote waliingia Argentina kila mmoja kutoka sehemu tofauti na wakiwa na paspoti tofauti,walipofika Argentina walikutana na kutengeneza NGOME na kugawana majukumu ya namna bora ya kumteka Eichman..Sasa basi Mossad wakaweka mtego na ikatokea bahati nzuri kulikuwa na maadhimisho ya kitaofa nchini Argentina ambako Serikali ya Israel ilikuwa inawakilishwa na waziri wake wa Elimu,hii ilikuwa fursa kubwa kwa Mossad hivo wakaazimia kuwa waziri asafiri na ndege binafsi,hili jambo lilifanywa bila waziri kujulishwa msingi wake,kuanzia rubani hadi wahudumu wa ndege walichaguliwa na Mossad na wengi walikuwa majasusi.Kule nchini Argentina kile kikosi cha watu kumi na mbili kiliendelea na mipango na walikodisha apartment ambayo iliwekewa mfumo wote wa ulinzi na uokozi,ikiwepo hadi handaki la kutoroka ikitokea polisi wa Argentina wamegundua kuhusu mpango kabla
Sasa mpango kamili ukawa kama ifuatavyo siku ya kutekwa Eichman angekamatwa akiwa anaingia nyumbani kwake,Mossad walikodisha gari mbili moja ya kumteka na moja kwa ajili ya ulinzi,ile ya kumteka ingeegeshwa nje kidogo ya nyumbani kwa Eichman alafu ingefanywa kama vile imeharibika na moja ya Mossad angeingia chini kama anaitengeneza(Kumbuka walishamfuatilia Eichman kwa muda mrefu na walikuwa wanajua muda wa kuingia nyumbani jioni)siku ya tukio walipanga kumsubiri hadi saa mbili kamili usiku awe amefika na ikatokea kuwa hajatokea basi waondoke,wale jamaa wakasubiri hadi saa mbili na robo Eichman alikuwa hajatokea,wakaongeza dakika kumi Zaidi wakiwa katika kukata tamaa ghafla wakaona basi limeshusha abiria kumbe ni Eichman sasa yule jasusi aliyepangwa akamsemesha Eichman alipogeuza shingo akarukiwa chapu na kuingizwa kwenye gari wakamtaka atii sharia bila shuruti…gari zikaondoka mwendo wa kasi hadi kwenye ile Apartment…baada ya kumgagua kwa kina wakajiridhisha kwa kina kuwa ndie muhusika wao..baadae alihojiwa majina yake,na namba yake ya Nazi,namba ya kiatu etc,bwana Eichman alitoa ushirikiano mkubwa kujibu maswali yote.Eichmann alieleza yote baada ya kugundua kuwa ametiwa nguvuni na watu ambao alikuwa amewatoroka kwa miaka mingi,alieleza jinsi alivojibadilisha majina na kupata Uraia wa Argentina na jinsi ambavo chama cha Nazi kilikuwa kinawaunga mkono kupitia taasisi zao za siri,alifikiri kuwa sasa angemalizia maisha yaliyobaki kwa Amani
Sasa ikatokea kitu ambacho hakikutarajiwa ile sherehe iilikuwa ifanyike May 10 ikasogezwa mbele hadi Mei 19,hivo walilazimika kukaa na mteka kwa siku tisa jambo ambalo ni hatari sana.Kiongozi wa hii operesheni akalazimika kuwaelekeza wale majasusi waliomshikilia Eichman kuwa ikatokea wakakamatwa na polisi basi wajitambulishe kwa utambilisho rasmi kuwa wao ni Waisrael wamemkamata mtuhumiwa namba moja wa Nazi(kumbuka hawa majasusi walikuwa na utambulisho tofauti tofauti)..pia ikatengeneza document feki inayoonyesha kuwa Eichman amekiri makossa yake na ameomba kupelekwa Israel ili akashtakiwe mahakamani
I, the undersigned Adolf Eichmann, of my own free will hereby declare: now that my real identity has been discovered, I recognize that there is no further use in trying to evade the course of justice. I agree to be taken to Israel and stand trial before a qualified tribunal. It is understood that I shall be given the assistance of an advocate and that I shall be permitted to lay before the court, without travesty of the facts, an account of the last years of my service in Germany, so that a truthful description of those events may be passed on to the future generations.I am making this declaration of my own accord. Nothing has been promised to me and I have not been threatened. My desire is to find inner peace at last. As I am unable to remember all the details,and may become confused when stating the facts, I ask that the relevant documents and testimonies be placed at my disposal to help me in my efforts to establish the truth. Adolf Eichmann, Buenos Aires,May 1960.
This declaration, of course, had no legal validity.
Mei 20 ndege ilipangwa kuondoka,hivo Mossad walimvalisha Eichman kama muhudumu wa ndege na wakatengeneza ripoti feki ya kitabibu kuwa muhudumu ameugua na yupo hoi kwenye kiti cha kubebea wagonjwa.Eichman aliingizwa uwanjani kwa utaratibu huo(Mossad walikuwa wanatembea na kila kitu ikiwepo mtambo maalum wa kutengeneza kila aina ya nyaraka iliyohitajika ikiwepo vitambulisho,pamoja na pasi mbalimbali).Mwaka 1961 Eichman alifikishwa kortini kujibu tuhuma zake mahakama ilimkuta na hatia na alihukumiwa kunyongwa hadi kufa,haya ndio maneno yake ya mwisho
: “We’ll meet again …I have lived,believing in God …I obeyed the laws of war and was loyal to my flag …”
Hiyo SALA yao ipoje, tunaomba maneno yake.Kitabu.Mossad
Mwandishi.Michael Bar Zohar & Nissim Mishal
Mchambuzi.Nanyaro EJ
Chapter 21
FROM THE LAND OF THE QUEEN OF SHEBA
Mwandishi anasema kuwa haya yalikuwa mashairi ya mshairi maarufu Haim Idissis,maneno ya mashairi haya yaliongeza ladha kwenye safari,sawa na zile nyimbo wakati wa kutwanga mahindi!
The moon is watching from above On my back is a small bag of food
The desert beneath us has no end ahead And my mother promises my little brothers:
“A little more, a little more, Lift up your legs, a last push Toward Jerusalem.” Kama tuliviona huko nyuma jamii ya Wazayuni ilitapakaa hadi Ethiopia,mwandishi anasema kuwa hii ni moja ya jamii ambayo iliteseka sana katika mpango wao wa kurejea kwenye nchi ya ahadi,huko nchini Ethiopia waliishi kwenye milima na mabonde na kwa miaka mingi waliishi Bibilia
Hawa WaIsrael, wa Ethiopia waliitwa jina maarufu FALASHA,neno Falasha lililenga kuwashusha hadhi yao,yaani Wa Israel kutoka pembe nyingine za dunia waliwaona hawa wa Ethiopia kama watu washamba,ambao wapo chini ya kiwango,kwa kawaida hata kabla ya kuundwa kwa Taifa la Israel,huwa na utamaduni wa kwenda kuhiji Yerusalem,lakini hawa Falasha waliishi miaka mingi pasipo kwenda
Mwaka 1977 ndio Serikali ya Israel chini ya waziri mkuu Menachem Begin alipoitaka Mossad wafanye kila waliwezalo wawarejeshe Falasha katika nchi ya ahadi,itakumbukwa kuwa uanzishwaji wa Taifa la Israel ulienda sambamba na kuwarejesha Waisrael katika ardhi waliyopora kutoka kwa Wapalestina
Wakati mpango huu unaanza Ethiopia ilikuwa kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe,hivo Israel ikaingia dili na serikali ya Mengistu kuwa wao Israel itaisadia Ethiopia vifaa vya kivita,lakini ndege hiyo itakayokuja na silaha ndio itaondoka ikiwa imejaa waisrael kuwarejesha kwao,hivo ndege kubwa ikawa inatua na mzigo wa silaha inaondoka na abria ikiwa imejaa,mpango huu ulidumu kwa miezi sita tu na kuja kuvunjika baada ya ulimi wa Waziri wa mambo ya nje ya Israel bwana Moshe Dayan,kuteleza wakati anahojiwa na gazeti moja la uswisi,ambako alikiri kuwa ni kweli Israel wanatoa msaada wa silaha za kivita kwa utawala wa Ethiopia,hii habari ilimkasirisha Bwana Mengistu hivo akatupilia mbali makubaliano na Mossad hapo hapo
Baada ya haya makubaliano kuvunjika ilibidi Waisrael watoroshwe kwa siri kupitia Sudan,wakati huo Sudan ilikuwa hasimu wa Israel ,hivo ikalazimu utoroshaji ufanyike kupitia makambi ya wakimbizi,Wazayuni walilazimika kusafiri kwa miguu umbali mrefu porini,huku wakigongwa na nyoka na nge,na wengine kufa njaa au kiu,wengne walivamiwa na watu wabaya na kunyanganywa kila walichokuwa nacho,ilikuwa safari ngumu hasa kwa wanawake na watoto,lakini tumaini lao ilikuwa kufikia nchi ya ahadi(Safari hii ni kama ile ya waisrael kutoka utumwani misri)
Wakati huo Baba mmoja alipoteza wa.toto wanne kwa mpigo,Kila asubuhi wasafiri walihesabu maiti za ndugu jamaa na marafiki waliokufa,angalau kila familia kulikuwa na msiba
Hadi mwaka 1981 angalau wazayuni 4000(elfu nne) walipoteza maisha katika harakati za kurudi nchini kwao,nchi ya ahadi…hii ni idadi ya Waisrael kutoka kushi tu
Baada ya hali kuwa mbaya yaani kushindwa kuwachukua wenzao kutoka Addis na kushindwa kupitia Sudan Mossad walianzisha kampuni ya Utalii na usafiri iliyosajiliwa Ulaya.Hii kampuni ambayo ilikuwa ni cover ilitafuta beach huko Sudan na kuinunua kwa lengo la kuweka hapo hotel ya Kitalii na kufanya mambo mbalimbali ya kitalii,hii kampuni ya Mossad iliingia mkataba na Serikali ya Sudan na ikawa inalipwa kodi na tozo mbalimbali.Mossad wakafungua Hotel iliyoitwa Arous Resort.Hapo walijenga vyumba vichache na mahema(Majengo ambayo sio ya kudumu).Wale maofisa wa Mossad ambao walikuwa wamepeana nafasi mbalimbali za menejimenti hapo Hotelini walikuwa na kazi moja tu usiku kwenda kwenye kambi za wakimbizi,na maeneo ambayo waliishi Waisrael na kujitambulisha kwao,moja ya utambulisho muhimu ilikuwa SALA(Waisrael wana aina yao ya SALA ambayo ni Uniform duniani kote)popote ambako utata ulitokea SALA ndio iliyoondoa utata huo! Wakishafikishwa hotelini walisafirishwa usiku kupitia bahari nyekundu kuelekea Israel,zoezi hili lilifanyika kwa usiri mkubwa sana kuepuka kushtukiwa na mamlaka za Sudan na Ethiopia
Mwandishi anasema kuwa kulikuwa na Waisrael weusi kabisa ambao hawakuamini kuwa kua Waisrael weupe(Kuna Waisrael weusi kabisa na Waisrael weupe,na wale wa kati kama Waarabu)..sasa hawa weusi wa Ethiopia waliishi milimani,maisha duni ya upweke na hawakujua kuwa kuna wenzao weupe,ila walijua kuwa kuna nchi ya ahadi…hawa SALA ndio iliwaunganisha!Pale hotelini wafanyakazi wazawa walihisi kuna kitu kisicho cha kawaida ila hawakujali sana kwa kuwa waliona hayawahusu alimradi wanalipwa mshahara wao!
Waliendelea na utaratibu huu kwa muda lakini ilikuwa inawachukua muda mrefu,maana watu walikuwa ni wengi.Siku moja watalii na wateja waliamka asubuhi na kukuta menejimenti nzima haipo,wale waajiriwa wachache wenyeji walikuta barua kutoka kwa menejimenti kuwa wameshindwa kuendelea na biashara hivo kila anayedai atalipwa kwa njia benki ndani ya wiki mbili,na wateja waliokuwa wamefanya booking watarejeshewa fedha zao.Hapo ukawa mwisho wa Arous Resort!
Mossad wakaamua kuja na mpango mwingine mwaka 1982,mpango hatari lakini wenye ufanisi mkubwa..Mossad waliamua kutuma vijana wao Sudan ambao walitafuta eneo fulani kisha wakalitengeneza kama uwanja wa ndege,hapo Mossad walipanga kurusha ndege ambayo ingetua kwenye uwanja huo ili kuwatorosha wenzao.Mpango huu ulifanikiwa ambako ndege ya abiria ilichukua watu 213,kazi hii iliendelea kwa wiki kadhaa ila baadae Serikali ya Sudan ilishtuka,Mossad wakatelekeza ule uwanja wa kwanza kisha wakaenda mbali kuweka uwanja mwingine,safari hii walikuwa wanaleta ndege saba zenye uwezo wa kubeba abria 200 kila mmoja
Kati ya 1982 hadi 1984 zaidi ya Waisrael wenye asili ya Ethiopia(Waethiopia wenye asili ya Israel) laki moja na nusu walisafirishwa kurejeshwa kwao na Mossad
Mwanzoni mwa 1985 hali ya uchumi ya Sudan ilidorora na usalama ukawa shakani,Serikali ya Sudan ikaomba msaada wa chakula na silaha kutoka Washington,mara moja Mossad wakajua na wakaomba USA iwaachie hiyo kazi ambayo Israel ingetoa silaha na chakula cha msaada,kwa masharti ya Serikali ya Sudan kuruhusu ndege za Israel kutua na kuchukua raia wake(Mwenye njaa hana tabia) Sudani ilikubali sharti hili na mara moja Mossad wakatekeleza hii iliitwa operesheni Musa………………katika kipindi cha siku arobaini Zaidi ya wazayuni 8000 walirejeshwa nchi yao ya ahadi
Mwaka 1991 Israel ilianzisha operesheni Solomon kwenye moja ya matukio muhimu Ndege ilibeba abiria 1087 ila wakati wa kushuka ikawa na abiria 1088,mama mmoja alikuwa amejifungua ndani ya ndege! Hadi mwaka huo operesheni zote,Musa,Solomoni,Queen Sheba zilifanikiwa kurejesha Waisrael laki tano(nusu milioni) katika nchi yao.
Mwandishi anasema kuwa bado jitihada zinaendelea hadi leo kuhakikisha kuwa inawarejesha wenzao(makabila kadhaa)yaliyopo nchini Ethiopia,ila kumekuwa na ugumu mno wa kukamilisha kazi hii….inasemekana bado kuna kazi ya siri inaendelea kufanyika,ila siku ya mwisho wote watarejea kwao!
…………………………………Mwisho……………………………
Mpenzi msomaji ni matarajio yangu kuwa uchambuzi huu umekuwa wa kuburudisha,kuelimisha na kukupa hari ya kusoma kitabu,ambao ndio msingi wake
Nanyaro EJ
Ni zamu ya Iran kufutwa duniani![]()
Hii wameitolea na movie kabisa.
🤣Ni zamu ya Iran kufutwa duniani