Mungu ibariki Tanzania
Sidhani kuna asiyejua nguvu ya kiti cha urais/ufalme/umalkia/amiri jeshi mkuu.
Sidhani kama wanayoyafanya hawajui matokeo yake.
Sidhani kama walikua na ushauri na wakakosa au kushindwa kumshauri nje ya hadhara.
Tuendelee kuliombea taifa letu amani tukijua katika kila nchi kuna muwakilishi wa Mungu ambaye ni mtawala mkuu/ Mfalme/Rais wa nchi hiyo.
Kwakuwa taratibu za kumpata zilikua sahihi, na kwakuwa tumeamriwa na Mungu kuwa watii. Hatuna budi kuwa watii huku tukimuomba Mungu usiku na mchana kwaajili ya ustawi, amani na mafanikio ya Rais na taifa letu; huku tukipeleka haja zetu nyingine zisizokuwa na hila kwa Mungu tukiwa safi.
Kwa tunaamini chochote Rais anachokifanya kipo anachokijua na kukiamini; basi na sisi tuendelee kuomba ili Mungu amuongoze kwa maono na ndoto atufikishe pale tunapohitaji
Katika hili sakata wapo wanaotoa ushauri mzuri au pongezi nyingi kwa Rais lakini ni wenye hila ndani yao na muda utasema. Maadui unaowajua ni bora zaidi ya marafiki usiowajua na ukadhani ni marafiki kumbe wana jambo lao.
Wapo wanaoongea lugha mbovu/dharau/chuki/dhihaka dhidi ya Rais sababu wanaumia kwa yeye kuwa kwenye hicho kiti na wanaona hastahili. Hawana mpango kabisa wa kumsaidia Rais wanatamani watumie nguvu zao binafsi kuonyesha misimamo yao kwamba wako bora zaidi. Ila tuu wanajisahau kwamba hawana hiyo mamlaka.
Wapo wanaoongea na kukosoa kwa nguvu bila mipaka sababu wanaamini kwamba mambo yanayofanyika sio sahihi na hayawapendezi ila wanahisi hawana nafasi ya kusikilizwa. Lakini wanasahau SSH ndio Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania. Busara ni bora kuliko nguvu, wangeangalia njia bora yenye maslahi ya taifa ingekua bora zaidi.
Watanzania tumuombee Rais. Tumuombee apate watu sahihi wa kutafsiri kile anachotaka kufanya, na apate wasaidizi wa kukifanya kwa usahihi uleule uliotafsiriwa. Mungu ni mwema sana kwetu na ataendelea kututendea mema kadri tunavyomuomba kadri ya nia zetu njema ukamilifu wetu mbele zake.
Yohana 16:23-24
"Katika siku hiyo hamtaniuliza neno lolote. Amin, amin nawaambia, kama mkimwomba Baba jambo lolote kwa jina langu, yeye atawapa. Mpaka sasa hamjaomba jambo lolote kwa Jina langu. Ombeni nanyi mtapewa, ili furaha yenu ipate kuwa kamili."